Kuitikia Simu ya Mh. Raisi kwa Waziri Mpango Kumjibu Bashe na Nape


Songambele

Songambele

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2007
Messages
3,967
Likes
1,452
Points
280
Songambele

Songambele

JF-Expert Member
Joined Nov 20, 2007
3,967 1,452 280
Ndugu wana JF, kwa heshima kubwa kabisa tunafungua mjadala wa kutafuta fedha za kujenga reli standard gauge kwa sekta binafsi na wananchi. Milango imefunguliwa kwa mujibu wa Waziri Mpango ni Kipande cha Reli kuelekea Mpanda na sehemu ilielekezwa na Mh. Raisi, mie siamini kama ile simu ilikuwa kejeli kwa waheshimiwa waliotoa michango yao lakini nimeona fursa na inawezekana kabisa jambo hili likatimia na faida za haraka ni kuwa na Reli; pili kuwajumuhisha wananzengo kwa wao kutoboka moja kwa moja; tatu watapata faida pia kutokana na uwekezaji huo; na masoko yetu ya mitaji kuanza kuchangamkia biashara.

Hapa nazungumzia Tanzania Railway Tax Free bonds kiasi cha kutosha kupeleka reli sio Makutupora kama alivyowahi kupendekeza ZZK bali kuifikisha Kigoma kabisa na kuhitimisha mijadala yote. Hii inaweza kufanyika kwa kuweka bracket za wanunuzi wa bonds 60% those in higher tax bracket na (diaspora na wananzengo) wakamaliza hiyo 40% kukusanya kiasi chote kinacho hitajika tukafunga mijadala.

Shime ndugu wananchi wale wanaoenda kununua viwanja, hisa, kubet, na kucheza bahati nasibu waelekeze pesa zao katika biashara hii ambayo italipa zaidi na ya uhakika kwa watu wote muda wa bonds ukiwa miaka 15 kila mtu atatusua na nchi itakuza biashara zake na nchi jirani haraka zaidi ya ilivyokusudiwa na uchumi kwenda mbio sana.

Wito wangu kwa Mh. Spika asaidie kuunda kamati ya kumvaa raisi na kuikimbilia hii fursa aliyotoa Mh. Raisi kama ilivyokuwa kwa makinikia atupe sie wananchi haraka iwezekananavyo akusanyiwe hizo pesa amalize kazi: Bashe, Nape, Zitto na Sekta Binafsi (TPSF and etal) wawemo katika kamati Ethiopia, India wao wanatumia hizi fursa tuachane na hizi focus za cherehani 4 kiwanda vinapoteza muda wa watu. Watu wafanye serious deep diving kutatua matatizo ya wananchi. kwakuwa bunge linakaaga kama kamati ya chama wanaweza anzisha session ya kukaa nje ya vikao vyao wakajadili jambo hili, wakivua tai, makoti, magwanda na vyama vyao wakiacha nje lazima tutakwenda wakati mwingine tunachoka na business as ussual kila mwenye wazo apewe nafasi aongee off records imani yetu wapo ambao wako vizuri, weledi na wazalendo ebu tuachane na red tapes wakati mwingine tuwe wananzengo.

Watu wamosoko ya mitaji wakihusishwa watasaidia kuweka viwango vya pesa zinazohitajika na size ya chini mpaka ya juu ya uwekezaji katika bonds. Kama watu wana bett na kugamble token tukizielekeza huku tutatusua hata lile la ukanda litaisha lenyewe kumbukeni tuko 50M plus tukishawishi 20% tu wakitoa sh. 500 kwa mwezi tutafika mbaali sana, tuivunje 7 trilion tuigombanie kipandekipande. Tukianzisha Tanzania Railway Financing Corporation na ikasajiliwa katika masoko ya hisa, tutashawishi hata haya mashirika ya hifadhi kuwekeza mitaji huko na by the way hii kitu itaishi miaka dahal. Badala ya kung'ang'ania haya mambo ya TTCL na kushindania vitu walivyoanzisha wengine pamoja na kutumia muda mwingi kudhibiti hapa itakuwa hatua ya kwanza kutengeneza donor country manake mtonyo ukiwa mkubwa tutakopesha wengine kwenda kujenga reli kama ilivyo ndoto ya mkuu.

Hii kitu naileta kwenu kwa brainstorming ili tupunguze stress za kutaka kufanya mambo makubwa kwa pesa za kodi, tutaacha kukamata mifugo ya wafugaji maskini na kuwadhulumu, kuvizia madereva na kunyatia wafanyabiashara wadogo kulipa kodi zisizoendana na biashara zao. Tujenge taasisi zetu kwa mawazo yetu wenyewe zitengeneze pesa halali.
 
Lobapula

Lobapula

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2011
Messages
2,302
Likes
1,452
Points
280
Lobapula

Lobapula

JF-Expert Member
Joined Jun 19, 2011
2,302 1,452 280
Wale wote waliobeza ujenzi wa STG railway rais kawapa fursa adhimu ni wao sasa kujipanga na kuja na solutions sio kukosoa tu kukosoa tu tunategemea Nape, Bashe na Zitto et al watakuja na wawekezaji kutoka sekta binafsi waweze kujenga reli
 
M

mwalimu lyapongoka

Senior Member
Joined
Dec 28, 2016
Messages
174
Likes
203
Points
60
Age
60
M

mwalimu lyapongoka

Senior Member
Joined Dec 28, 2016
174 203 60
Mfano tukicopy mfumo Wa uendeshaji mabasi yaendayo kwa kasi kuna shida hapo?
 
Bams

Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Messages
5,639
Likes
7,446
Points
280
Bams

Bams

JF-Expert Member
Joined Oct 19, 2010
5,639 7,446 280
Wazo ni jema lakini ili kuwekeza, tunahitaji sana confidence na trust kutoka kwa serikali. Japo haisemwi wazi lakini matendo ya serikali yanaashiria uadui mkubwa kati ya serikali (kupitia vyombo vyake kama TRA, Polisi na viongozi kama DCs na RCs) dhidi ya sekta binafsi, na hasa matajiri.

Uhusiano kati ya serikali na wawekezaji umekuwa wa mashaka sana. Uwekezaji wa maana utapatikana kutakapokuwa na kuaminiana. Hakuna mwenye confidence na mazingira yetu ya uwekezaji. Confidence inakuwepo sheria zinapolindwa na kufuatwa. Kwa sasa, kwa kiasi kikubwa sheria zimekuwa kauli za viongozi ambazo zinabadilika kila leo, kila wakati kiongozi anapojisikia kusema - na akisema ni sheria. Je, kuna anayejua kesho na keshokutwa atasema nini? Ndiyo maana ni salama na busara zaidi kuwekeza kwenye vyerahani vinne kuliko kwenye multi billion projects.
 
adden

adden

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Messages
4,688
Likes
6,325
Points
280
adden

adden

JF-Expert Member
Joined Dec 27, 2015
4,688 6,325 280
Wote nimewaelewa sana!
Hili jambo ni nzuri lakini miundombinu bado sio rafiki kwa kuwekeza.watu watahitaji insurance ya serikali iliyo rigid.
 
M

mwana wa africa

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2011
Messages
523
Likes
48
Points
45
Age
41
M

mwana wa africa

JF-Expert Member
Joined Apr 17, 2011
523 48 45
Wazo ni jema lakini ili kuwekeza, tunahitaji sana confidence na trust kutoka kwa serikali. Japo haisemwi wazi lakini matendo ya serikali yanaashiria uadui mkubwa kati ya serikali (kupitia vyombo vyake kama TRA, Polisi na viongozi kama DCs na RCs) dhidi ya sekta binafsi, na hasa matajiri.

Uhusiano kati ya serikali na wawekezaji umekuwa wa mashaka sana. Uwekezaji wa maana utapatikana kutakapokuwa na kuaminiana. Hakuna mwenye confidence na mazingira yetu ya uwekezaji. Confidence inakuwepo sheria zinapolindwa na kufuatwa. Kwa sasa, kwa kiasi kikubwa sheria zimekuwa kauli za viongozi ambazo zinabadilika kila leo, kila wakati kiongozi anapojisikia kusema - na akisema ni sheria. Je, kuna anayejua kesho na keshokutwa atasema nini? Ndiyo maana ni salama na busara zaidi kuwekeza kwenye vyerahani vinne kuliko kwenye multi billion projects.
Umenena kweli comrade. Hakuna mwekezaji ambaye atawekeza Pesa yake kichwa kichwa bila kufanya study ya kutosha juu ya mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na hali ya kisiasa katika nchi, umadhubuti wa sera na sheria etc. Kwa takwimu za juzi juzi zinaonyesha TZ imeshuka kwa nafasi kadhaa hadi 137 kidunia. Masoko ya hisa yamedorora, mzunguko wa fedha upo chini, biashara, mauzo ya nje yapo taabani. Haya yote yanatokea katika kipindi ambacho serikali imebadili na kusimamia mambo kwa namna ambayo hayachochei au kuhamashisha wawekezaji kuweka mitaji yao kwenye miradi ya muda mrefu. Mandela aliweahi kusema " uongozi ni kuwasikiliza watu" hapa ndipo kwenye tatizo.
 

Forum statistics

Threads 1,272,874
Members 490,197
Posts 30,463,189