Nini maana ya "Kuishi Vizuri na Watu"? Je, ni sahihi kuenenda ndivyo sivyo ili kujijengea taswira njema katika jamii?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
S.hikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums.

Ndugu zangu watanzania eti;

Nini maana ya "Kuishi Vizuri na Watu"? Je, ni sahihi kuenenda ndivyo sivyo ili ujijengee taswira njema katika jamii?

Kuna siku moja mwezi wa August mwaka huu wa 2020 nikiwa nimemaliza mizunguko yangu huko Kariakoo kabla sijapanda gari za kunileta huku Kivule nikasema ngoja niende nikawatembelee na kuwasalimu jamaa na marafiki zangu ambao nilikuwa ninakaa nao kule maeneo ya Mtoni Mtongani.

Basi mimi huuuyooooo mpaka machinga complex, nikapanda gari ya kuelekea Mbagala. Nikaenda salama tu, na gari ilipofika kituo cha Mtoni Mtongani nikashuka zangu, kisha nikavuka barabara na kutembea kama mwendo wa dakika 15 hivi mpaka mtaani nilipokuwa ninaishi zamani.

Ile kufika tu nikakutana na washkaji zangu wa zamani wengi tu, wengine nilisoma nao shule ya msingi ila wamechoka balaa. Wanakula unga, wanavuta bangi too much na kunywa gongo.

Wakaanza kuniuliza maswali mengi sana kama vile " Alex, siku hizi unapiga mishe gani kamanda, vp umeoa, yule mdogo wako yupo wapi?" kwa kweli tuliongea na kucheka kwa kukumbushana mambo ya zamani mpaka ikawa raha. Sasa ulipofika muda wa mimi kuondoka washkaji wakanibana sana, wakawa wanasema siwezi kuondoka bila kuwaachia chochote kitu kwa maana wao wana arosto ile mbaya.

Lazima niwaachie kwanja kidogo hata kama ni 5,000 tu wakapige machozi ya simba (gongo), ganja (bangi) na wida/ngada ili wapate stimu kwa maana mwana amewatimbia maskani na tulikuwa hatujaonana mwaka kama wa 6 hivi.

Wale jamaa licha ya kwamba tulipiga story na kucheka sana, niliwageuzia kibao pale pale na kuwachana "black and white" kwamba siwezi kuwapa pesa waende kunywa gongo au kuvutia bangi" na hawakuamini macho yao.

Mimi niliwaambia ninaweza kuwapa pesa katika masuala ya msingi tu kama vile matibabu au rambirambi ya msiba na sio pesa ya kwenda kunywea gongo au kununua ngada/wida. Kwa kiroho upande ikabidi waniache na mimi huuuyoooooo nikaondoka zangu kwenda kusalimiana na majirani zangu wengine wa zamani alafu nikarudi kituoni kupanda daladala ya kutoka Mbagala kwenda Gongo la Mboto kisha Kivule.

Weeks chache kadhaa mbele nikaanza kupokea SMS za kuniponda kutoka kwa baadhi ya watu wanaonifahamu (inaonekana wale jamaa waliwasimulia jirani zangu wa zamani kuhusu kuwanyima pesa) kuwa eti mimi Alex sijui kuishi vizuri na watu na ninapaswa kujifunza hiyo tabia njema ya kuishi vizuri na watu kwa maana kuna siku nitapata matatizo na nitakosa wa kunisaidia. Eti wana jamiiforums;

Ipi ni tafsiri halisi na maana nzuri ya hii kauli maarufu "Kuishi Vizuri na Watu"? Je, ni sahihi kuenenda vibaya ili ujijengee taswira njema katika jamii?

Ningewapa hawa jamaa pesa ya kunununlia gongo na bangi ndio kuishi vizuri na watu?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO. MUNGU IBARIKI NCHI YANGU.
 
Ungewapa tu upite hivi
Kuhusu matumizi ungewaachia wao si ya kwao umeshawapa

Sent using Jamii Forums mobile app
Laiti kama angewapa hao jamaa pesa ya kununulia gongo na bangi, kuna baadhi ya watu wangesema kuwa Soldier HAJUI KUISHI VIZURI NA WATU kwa maana umewapa rafiki zake pesa ya kwenda kununulia sumu.

Yaaani kwa ufupi ni kwamba amesaidia uhalifu kutendeka.
 
Sidhani kama ulifanya kitu sahihi, ni vema ungewapatia tu hiyo 5k mzee.

Vipi baada ya kuwanyima umewasaidia kuacha hizo tabia?


Let's meet at the top, cheers 🍻
 
Ungewapa tu upite hivi
Kuhusu matumizi ungewaachia wao si ya kwao umeshawapa
Kuhusu matumizi ni kwamba walikwishasema kuwa wanataka kwenda kunywa gongo na kuvuta bangi.

Hauoni kwamba kuishi vizuri na watu (roho nzuri) ni lazima kuwe na limit/redline?
 
Back
Top Bottom