Kuishi na mwanamke mjamzito ni zaidi ya gereza

IJIGHA NDIO HOME

JF-Expert Member
Jul 13, 2019
748
769
Wakuu habari zetu, mimi ni kijana nimeoa takribani miaka miwili iliopita, nashukuru Mungu mwaka huu kajifungua salama.sasa kimbembe nilichokutana nacho alipokuwa mjamzito siji kusahau kuna siku nilitoka kazini nafika tu home namkuta anaanda msosi ile namsalimia tu za kushinda mwenzangu kakausha nikaongea mara ya pili kimya basi nikaondoka nikaenda kujipumzisha. Alipomaliza kupika akala naye kaja kulala hata kuniita msosi tayari hakuna.

Nikaamka nikaenda kula nikarudi kulala kimya kimya kesho yake asubuhi wakati najiandaa kwenda job akasema usiporudi na matunda utahama nyumba hii daa nilipandwa na hasira sikimjibu jioni niliporudi nikamnunulia alivyoagiza nikamletea muda mwingine anatumia amri nikampikie alikuwa mkali acha tu.

Lakini sasa hivi toka ajifungue kawa mpole kama sio yule na mimi nilimwekea tu akijifungua akija kunizingua hasira nimvuluga kweli.

Kama kuna yoyote aliyewahi kukumbwa na kashia kama hii asimulie
 
Usumbufu huwa unakuwa mwezi wa kwanza mpaka wa nne hiyo miezi mingine usumbufu unakuwa sio Mkubwa kama miezi hiyo lakini si kwa wote wengine siyo wasumbufu wengine anakupenda mpaka unaweza kuomba aendelee kuwa na mimba cha msingi nikumvumilia kwa kutambua kuwa ni ya kitambo tu, siyo ndo iwe sababu ya kumtesa au kumtafutia mchepuko
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom