Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,398
Kuna wanawake ambao wanaitwa wana kisirani na wanyonyaji. Wanawake wa aina hii ndani ya ndoa zao ni vituko vitupu, na mara nyingi kama wameolewa na wanaume waliojitambua ndoa zao huwa hazidumu.
Mara zote mke wa aina anataka kuona mumewe akimhangaikia kupita kiasi na bado asiridhike. Ni vigumu kutabiri mienendo ya tabia zao. Kama anahitaji kufanyiwa jambo na mumewe na anahisi mumewe haweze kumtimizia, anaweza kuamka akiwa na furaha tele, lakini ikifika jioni utamkuta amenuna tu. Na mumewe atakapomuuliza sababu ya kununa, anaweza mkujibu "hamna kitu" , anachotafuta hapo ni kubembelezwa ili apate mahali pa kunzia.
Kwa kuwa anajua kuwa mumewe anamjali, atasema shida yake. " Yaani hela unayoniachia ya matumizi hapa nyumbani haitoshi kabisa na ninapata tabu sana kupanga bajeti". Tayari ujumbe umefika, lakini kwa namna ambayo itamfanya mume dhamira zimshitaki. Mume kwa kushtakiwa na dhamira ataongeza fedha. Kama ni mke aliyejiajiri au kuajiriwa anaweza kusingizia kuwa siku hizi biashara hakuna kabisa na hapati mapato ya kutosha au mshahara anaolipwa hautoshi na anafanya kazi, ile basi tu.
Na kauli kama hizi ni za kutarajiwa sana, "Waume wengine wanawasaidia wake zao kama mshahara au mapato hayatoshi, mimi ndivyo ninavyojua".Anachotaka ni kumfanya mumewe ahisi kwamba, yeye kama mume ameshindwa wajibu wake na kwamba, kuna wanaume bora zaidi huko nje ambao wanaweza kuwasaidia wake zao pale wanapokuwa na mshahara mdogo au mapato madogo katika biashara zao.
Wanawake wa aina hii huwa hawajiamini kabisa, na hutaka kuonekana ni wa maana, wana uwezo, wanajua na wanatambuliwa. Wanaweza kuwa na kisirani cha hasira za ziada, wambea sana, na wakati mwingine hupenda kujilinganisha sana.Hawana subira kabisa, wakitaka jambo lao wanataka litimizwe wakati huo huo, ni wasingiziaji wazuri, wakanushaji wa waziwazi wa mambo waliyofanya au kusema.
Ni watu wenye kero mwanzo mwisho.Pia wanakuwa na upendo wa bandia, pale wanapohitaji kitu kutoka kwa waume zao, watatenda yale ambayo hawayatendi. Atajifanya kumpokea mumewe akitoka kazini, kumuuliza angependa kula kitu gani, kumpangia au kumtafutia nguo za kuvaa asubuhi.
Siku zote hafanyi hivyo, bali hufanya yote hayo pale anapohitaji kitu kutoka kwa mumewe. Utakuta ni mtu wa mbinu na ujanjaujanja tu. Hasa kukiwa na wageni ndio ataonesha anampenda sana mumewe. Hata kama alikuwa hamvui soksi akitoka kazini , kukiwa na wageni atafanya hivyo. Ni wanafiki wa upendo kupindukia.
Itaendelea......................