Kuishi Dar Sasa Inakuwa Kero Sana Toka Kwa Wanasiasa na Wengine

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Dar bwana siku hizi taabu tupu. Yaani hapa ndipo kila mwanasiasa, polisi na wengine wanataka kujionyesha, ili waandikwe kwenye magazeti au watu wawaone ni wachapa kazi. Kuna usumbufu kutoka kila kona, kuanzia kwa Raisi, Mawaziri, MKuu wa Mkoa, Makatibu Wakuu, Polisi nk

Yaani utakuta mara leo ziara ya kushitukiza ya Raisi, Kesho ya Waziri, kesho kutwa Katibu Mkuu. Mara ooh karipoti Polisi sijui umeonekana kwenye Facebook unafanya kitu mbaya, mara polisi wamekusimamisha kwa nini umepita hii mitaa ya huku kwa changudoa usiku huu, sijui usafi wa mwezi, mara shoga zetu muwatafute - yote Dar tu!. Yaani hapo hatujaongelea kero za foleni barabarani kwa sababu Raisi au Waziri Mkuu anapita.

Inakuwa kama vile Tanzania ni Dar es Salaam tu, wala sio pamoja na mikoani. Mara nyingine najiuliza hata kama viongozi au mawaziri na polisi wanakumbuka kama Tanzania ni zaidi ya Dar es Salaam wanapoongea au kufanya mambo, pamoja na Raisi.

Naona kama wenzetu mikoani mmetulia sana. Unga mnabwia mnavyotaka bila usumbufu, foleni za mara moja moja, hakuna ziara za kushitukiza makazini nyie mnazisikia redioni tu!
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Nasikia ngada imepanda bei maradufu
 
tapatalk_jpeg_1487171261816.jpg
 
Back
Top Bottom