Kuisafisha CHADEMA na tuhuma za 'usanii' na rushwa ya ngono, Wajumbe Kamati Kuu wajitokeze ku-declare interests

domokaya

JF-Expert Member
Apr 22, 2010
3,545
1,719
Sintofahamu inayoendelea katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimegubikwa na sarakasi na nadharia nyingi. Moja ikiwa viongozi wa kamati kuu wanafanya usanii kwa kujidai kuwafukuza wabunge wale 19 uanachama wakati walifahamu fika mchezo mzima na walikuwa wakifahamu wale wabunge wakishaapishwa wataendelea kubaki na ubunge hivyo wao kama wajumbe wa kamati kuu na 'waume' wa waheshimiwa wabunge wale watanufaika na ubunge wao, hivyo kujifanya kuwafukuza wakati matunda ya ubunge wanayala ni usanii.

CHADEMA, kwa muda mrefu Sasa imekuwa ikishutumiwa kufanya teuzi za viti maalum kwa viongozi wakuu kupewa rushwa ya ngono. Je, inawezekana rushwa ya ngono ndiyo iliyopelekea 'ndoa' hizo kutokea au zilitokea tu kwa misingi ya kibinadamu?

Sasa umefika wakati wa wajumbe wa kamati kuu, akina Salum Mwalimu na wenzake kutoka hadharani ku-declare interests ili umma ufahamu kwa hakika usafi wao na kuondoa minong'ono na manung'uniko kuwa inakuwaje mume asifahamu mkewe kaenda kuapishwa wakati wanaishi nyumba moja?

Ugomvi wa Salum Mwalimu na Mbunge Sugu katika viti maalum baada ya uchaguzi mkuu wa 2015 kuisha kunalazimisha wajumbe wa kamati kuu kutoka mbele ya hadhara kuonesha usafi wao kama wao ni wasafi.

Umefika muda Chadema wafunguke kuhusu tuhuma za mapenzi, unyanyasaji kijinsia na rushwa ya ngono ndani ya chama.
 
Chadema kama taasisi haiwezi Kuwa na tuhuma za Ngono, watu wanaweza Kuwa nazo!
Watu wanaunda taasisi. Tabia za watu ndani ya taasisi zinafanya organization culture (tabia ya taasisi) Kama taasisi hiyo watu wake wanaishi kiunyumba bila kuoana, kama taasisi hiyo watu wake wana mahusiano ya wazi ya kingono pasipo kuwa wachumba, Kama taasisi hiyo utoaji wa fursa ni wa upendeleo kwa misingi ya ngono, basi kuna uwezekano jamii, umma ukaitambua taasisi hiyo ni ya kingono. Lakini Kama taasisi ina viashiria kama hivyo, basi taasisi hiyo inaweza kutuhumiwa kwa rushwa ya ngono.

Kama watuhumiwa wapo, na yanayotuhumiwa nayo si Kweli. Ikiwa taasisi inayoitumikia inawajibika kwenda mbele ya umma na kuweka ukweli wa mambo ili kusafisha taswira ya taasisi hiyo.
 
Mlitegemea jana akina Mdee watawalipua akina Mbowe lakini ikabuma! Sasa mmeanza tuhuma zisizo na mkia wala kichwa!
Hayo mambo ya mahusiano ni mambo ya chumbani wewe unataka watu wajitokeze hadharani kutafta kitu gani?
Je ni wapi katiba ya nchi au CHADEMA imekataza mahusiano ya watu wazima? Mbona hata ndani ya CCM kuna makada wengi tu wa kike mahawara zao wako CHADEMA? Au hukumsikia katibu mkuu mstaafu wa CCM akiweka hadharani hilo?
Kwa CHADEMA makda wakike wakiwa na mahusiano ni rushwa ya ngono lakini kwa CCM ni uzalendo ati!???
 
Watu wanaunda taasisi. Tabia za watu ndani ya taasisi zinafanya organization culture (tabia ya taasisi) Kama taasisi hiyo watu wake wanaishi kiunyumba bila kuoana, kama taasisi hiyo watu wake wana mahusiano ya wazi ya kingono pasipo kuwa wachumba, Kama taasisi hiyo utoaji wa fursa ni wa upendeleo kwa misingi ya ngono, basi kuna uwezekano jamii, umma ukaitambua taasisi hiyo ni ya kingono. Lakini Kama taasisi ina viashiria kama hivyo, basi taasisi hiyo inaweza kutuhumiwa kwa rushwa ya ngono. Kama watuhumiwa wapo, na yanayotuhumiwa nayo si Kweli. Ikiwa taasisi inayoitumikia inawajibika kwenda mbele ya umma na kuweka ukweli wa mambo ili kusafisha taswira ya taasisi hiyo.
na misingi ya taasisi ndiyo hubomoa na kujenga kwani tamaduni za watu ndo damu inayofanya taasisi ikae mda mrefu...
 
Mlitegemea jana akina Mdee watawalipua akina Mbowe lakini ikabuma! Sasa mmeanza tuhuma zisizo na mkia wala kichwa!
Hayo mambo ya mahusiano ni mambo ya chumbani wewe unataka watu wajitokeze hadharani kutafta kitu gani?
Je ni wapi katiba ya nchi au CHADEMA imekataza mahusiano ya watu wazima? Mbona hata ndani ya CCM kuna makada wengi tu wa kike mahawara zao wako CHADEMA? Au hukumsikia katibu mkuu mstaafu wa CCM akiweka hadharani hilo?
Kwa CHADEMA makda wakike wakiwa na mahusiano ni rushwa ya ngono lakini kwa CCM ni uzalendo ati!???
lini mwenyekiti anaachia damu changa kuongoza ni kama kalewa madaraka na kufanya chama kama taasisi ya familia
 
Kama yeye kaandika maneno yote kashindwa kujua point hii basi katika ccm kuna watu wajinga wengi sana
kama nawewe umeshindwa kujua kama taasisi inaundwa na watu, basi ni mjinga kuliko hata huyo aliechangia mada.
 
We mtoa hoja, ulishwahi kuombwa rushwa ya ngono na viongozi wa CDM? kama Yes, basi toa ushahidi hapa.
 
Sintofahamu inayoendelea katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimegubikwa na sarakasi na nadharia nyingi. Moja ikiwa viongozi wa kamati kuu wanafanya usanii kwa kujidai kuwafukuza wabunge wale 19 uanachama wakati walifahamu fika mchezo mzima na walikuwa wakifahamu wale wabunge wakishaapishwa wataendelea kubaki na ubunge hivyo wao kama wajumbe wa kamati kuu na 'waume' wa waheshimiwa wabunge wale watanufaika na ubunge wao, hivyo kujifanya kuwafukuza wakati matunda ya ubunge wanayala ni usanii.

CHADEMA, kwa muda mrefu Sasa imekuwa ikishutumiwa kufanya teuzi za viti maalum kwa viongozi wakuu kupewa rushwa ya ngono. Je, inawezekana rushwa ya ngono ndiyo iliyopelekea 'ndoa' hizo kutokea au zilitokea tu kwa misingi ya kibinadamu?

Sasa umefika wakati wa wajumbe wa kamati kuu, akina Salum Mwalimu na wenzake kutoka hadharani ku-declare interests ili umma ufahamu kwa hakika usafi wao na kuondoa minong'ono na manung'uniko kuwa inakuwaje mume asifahamu mkewe kaenda kuapishwa wakati wanaishi nyumba moja?

Ugomvi wa Salum Mwalimu na Mbunge Sugu katika viti maalum baada ya uchaguzi mkuu wa 2015 kuisha kunalazimisha wajumbe wa kamati kuu kutoka mbele ya hadhara kuonesha usafi wao kama wao ni wasafi.

Umefika muda Chadema wafunguke kuhusu tuhuma za mapenzi, unyanyasaji kijinsia na rushwa ya ngono ndani ya chama.
Wewe mgeni?
Mbona huko Lumumba mambo hayo ya ngono na teuzi ndo kawaida, Ni kama mbuzi-choma vs ugali😋
 
Kweli Chadema ni mti wenye matunda,kwa jinsi unavyoshambuliwa na mawe.

Wanaotawala CCM,wakusanya Kodi,CCM,wenye matumizi mabaya ya pesa ya umma,CCM,wanaonunua Ndege,wakati hata mafuta ya kula na sukari hatuwezi kuzalisha ya kutosha,CCM,walioiba pesa za escrow na kubeba kwenye magunia,CCM,lakini anayesemwa ni Chadema.

Waliopo Madarakani,uwezo wao wa akili ni mdogo sana,Wana Jeshi,la polisi,Jwtz,usalama,mgambo,hazina,wakurugenzi wote wanapokea amri kutoka juu,lakini wanatetemeshwa na chama Cha siasa ambacho hakina hata mgambo!?

Mishuzi inawatokaaaa
 
Back
Top Bottom