Kuipigia Kura Djibout Badala ya Kenya ni unafiki mkubwa, Kenya tunafanya nae biashara hao wengine vipi?

chotera

JF-Expert Member
May 19, 2016
6,300
15,018
Wakuu,

Haya mambo mimi siyajui lakini tumeanikwa na hatuna namna tena. Hivi kweli Djibout ambae naona hatupo nae EAC wala SADC ndio tumpigie kura yaani tumeshindwa mawazo hadi na Burundi? Kweli diplomasia yetu iko mashakani na imeanguka.

Binafsi sijaona sababu ya sisi kwenda kinyume na jumuia yetu ya Afrika mashariki hii si sawa kwa ujirani hata kama tuna ugomvi nao tusingepeleka kuaibika huko, hatukumpigia kura na ameshinda kwa kura nyingi hii ni aibu kubwa.

Tutaruka ruka lakini tumetia aibu na kuisaliti EAC.
 
Kuna chuki za kushangaza sana kutoka hii Serikali yetu na baadhi ya Watanzania kwa Wakenya. Hawa tuko nao kwenye Jumuiya moja na pia ni majirani zetu wa karibu mno ukilinganisha na Djibouti.

Hii kura ingekuwa ni kuwaonyesha Kenya kwamba kushinda kwao ni kushinda kwa Watanzania na hivyo miaka ya usoni nao watuunge mkono. Kama kweli kura ya Tanzania ilienda kwa Djibouti huo ni UPUUZI wa hali ya juu.
 
Niliona sehemu habari picha, sikuelewa vizuri, nikajua jf itawekwa na maelezo kiundani...
Umeweka habari hapa ila umeizungumzia kana kwamba kila yule anaijua hii inshu...
waweza elezea....
Ni kura gani?
Unamchagua nani?
Mwenye vigezo gani?
Imehusisha nchi gani?
Ina manufaa gani?..

Kama hutojali weka habari kana kwamba hakuna anayeijua kiundani japo najua wapo ila ni kwa msaada kwa wengine....
Kinyume na hapo watu watachangia kwa kuvutia upande wako kumbe kuna jambo la kuelewa,
Pengine hata kuna vigezo vya kuchaguliwa hio Djbout.
 
Mbona tuliwapatia Tausi, bado tunawapenda hao ndugu zetu na majirani zetu. Tausi ni bora kuliko hiyo kura.

Tulijua watashinda tu bila kura yetu na ukumbuke Djibout ilituomba tuipigie lakini Kenya haikutuomba, sasa aombaye na asiyeomba wampa nani??!!------ that is my take.🤣
 
IMG_5470.JPG
hapo ndio tumefika kwa sasa
 
Kuna chuki za kushangaza sana kutoka hii Serikali yetu na baadhi ya Watanzania kwa Wakenya. Hawa tuko nao kwenye Jumuiya moja na pia ni majirani zetu wa karibu mno ukilinganisha na Djibouti. Hii kura ingekuwa no kuwaonyesha Kenya kwamba kushinda kwao ni kushinda kwa Watanzania na hivyo miaka ya usoni nao watuunge mkono. Kama kweli kura ya Tanzania ilienda kwa Djibouti huo ni UPUUZI wa hali ya juu.
Tusimlaumu aliyepiga kura, hakuelewa Kiingereza alifikri kura zitakuwa za siri kwamba hatajulikana hata akimpigia Djibouti, sasa Kenya atajuaje? Ila ki ukweli tumeaibika mchana kweupe! Wazungu hawana siri!
 
Biashara imesimama kati yetu, na mgomvi ni kenya katunyima biashara ya mabilioni kwa wivu wake wa "ye anaugua si hatuugui,ye kafungia raia na kuwatesa, si tunadunda kitaa" sasa kumnyima kura ya ulinzi na usalama mnaona tumemuonea, KENYA NI JIRANI MWENYE CHOKOCHOKO
 
19 Reactions
Reply
Back
Top Bottom