Kuinua Hali Ya Maisha Ya Watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuinua Hali Ya Maisha Ya Watanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by polloz, Mar 6, 2006.

 1. p

  polloz New Member

  #1
  Mar 6, 2006
  Joined: Mar 5, 2006
  Messages: 4
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Huu ni wakati wa kuhinua uchumi wa nchi yetu TANZANIA.

  Lazima Serilikali hitumie kila mbinu kuhinua hali ya maisha ya wananchi.

  Kwa sasa hivi Tanzania uchumi wetu mkubwa unatokana na kilimo.

  Kwahiyo serikali lazima hitafute njia zingine zaidi kuhingiza mapato na hajira zaidi.

  Nafikiri tatizo kubwa zaidi ktk nchi yetu ni hajira kuwepo na mikutano namna la kutatua tatizo hilo.

  Sasa hivi tuna wasomi na wanauchumi lazima wakae pamoja nakufafanua na jinsi ya kuwasidia wananchi .
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Mar 6, 2006
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kwanza napenda kuwashukuru ndugu zangu kwa maoni yenu juu ya hili swala. nadhani tatizo letu kubwa hasa nchi maskini ni kuchanganya maswala haya mawili:- Siasa na Uchumi.

  Hata kama wenzetu nchi zilizoendelea wao huchanganya basi utakuta siasa huingizwa tu pale panapoonekana kuna faida kwao ya kiuchumi. Uchumi ndio sura ya nchi, uchumi ndio kiwiliwiwli na na roho ya nchi kwa hiyo maamuzi yote ya siasa lazima yawe ktk kuijenga afya ya taifa na sio kinyume.

  Ni kosa kubwa kuwa walafi yaani hatuchagui kinachoingia mwilini mwetu na pia ni kosa kubwa kutokula chakula bora (chenye nutrition) kwa sababu ya imani inayotokana na dhana.

  Poloz,
  Nakubaliana na wewe, binafsi swala la ajira lina uzito mkubwa sana kwa nchi yetu. na kulingana na mfano mdogo wa mwili hapo juu, sidhani kama kati yetu kuna mmoja wetu anayeweza kuwepo hapa na kuyazungumzia haya kama hana kazi! Ni matokeo ya hizo ajira tumeweza kuchagua nini tunachotaka kula ama kuujenga mwili wetu kwa chakula cha aina gani?.... chaguo la chakula halikutangulia kabisa mfuko wetu..yaani mapato yetu.

  Kuna mbinu nyingi sana ambazo nashindwa kuelewa kwa nini viongozi (siasa) na wataalam (wachumi) wetu wameshindwa kabisa kuyatatua maswala haya kulingana na mazingira yetu. Sidhani kama elimu yao imeishia ktk kapu la taka na sasa kinachotumika ni ulafi na ubinafsi.

  Hata hivyo nitazidi kuchangia zaidi mada hii kila tunavyozidi kusonga mbele maanake mwanga wa mwenge wetu wa uhuru bado upo isipokuwa tunaupuuza na kutumia artificial theories ktk pango hili lenye kiza - Utandawazi.
   
 3. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #3
  Dec 28, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Ndugu Willo, uliyasema maneno hayo takriban miaka mitatu iliyopita, unfortunately bado yako sahihi. Serikali haijafanya mabadiliko yoyote kujua jukumu lake katika kuiendeleza nchi hii.
   
 4. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #4
  Dec 28, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu naona kila mtu anaanza kutambua ukweli kuwa na sera hizi tulizonazo hatutafika popote tutaendelea kudumaa tu. Unaweza kujiuliza swali moja lakini usipate jibu. Toka Mwinyi aingie madarakani mpaka leo GDP yetu imepanda sana lakini maisha ya mtanzania yako chini kuliko ilivyokuwa mwaka 1970, ukiangalia kwa undani utaona kuwa tatizo kubwa liko kwenye utekelezaji wa sera za CCM na uozo uliko serikalini. Viongozi wengi hawana nia thabiti ya kuendeleza nchi, ila wana nia thabiti ya kujiendeleza wao, kitu ambacho wamefanikiwa sana.
   
Loading...