Kuingizwa mjini wakati wa kununua nyumba na viwanja! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuingizwa mjini wakati wa kununua nyumba na viwanja!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ubungoubungo, Mar 22, 2010.

 1. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #1
  Mar 22, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Samahani wakubwa, niliuwa na swali naomba kuuliza mnisaidie humu ndani, najua humu kuna wanasheria, ma estate agents, na watu wengine wengi wenye uzoefu tofautitofauti.

  NIFANYEJE ILI NISIINGIZWE MJINI, pindi ninapotaka kununua nyumba au kiwanja Tz?, ni vitu gani ninatakiwa kuhakikisha kuwa navyo, na kuwa na uhakika kuwa hicho kitu ninachonunua siyo scam. wengi hapa tume save vijisent kidogo, na tunataka kununua nyumba na viwanja, ila uwoga wajameni kuingizwa mjini. naomba mwenye uzoefu atueleze nini cha kuzingatia ili iwasaidie na wengine wengu humu ndani. asante.
   
 2. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Duh! wengi wameliwa katika jambo hili, ndo maana kesi za kushindania nyumba na viwanja hata haziishi. visa na mikasa, fitina kila siku kwasababu mtu anang'ang'ania kiwanja au nyumba ambayo aliingizwa mkenge. nafikiri discussion hii itasaidia wengi, including mimi mwenyewe. prego kwa mwenye kuleta mada.
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  Mar 22, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  jambo kubwa ni kuwa usiwaamini viongozi wa serikali za mitaa. Uthibitisho kuhusu kiwanja uupate kutoka kwa maofisa wa wizara. Watu wenmgi wanadanganyika kuwa kuna sehemu hazijapimwa. Inaweza kuwa kweli lakini watu wa ardhi wana details za karibu maeneo yote. Kuna watu wana mashamba wakidhani kuwa ni yao lakini taarifa zilizopo wizarani zinaonyesha kuwa hizo ni open space. Kuna wengine wanaishi maeneo bila kujua kuwa yamepimwa na taarifa zake zipo wizarani na hivyo wanayauza kama mashamba ya maeneo yasiyopimwa lakini kume yamepimwa. kwa hiyo usiwaamini sana local government officials pamoja na madalali au hata muuza kiwanja mwenyewe
   
 4. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Kuingizwa mjini watati wa kununua nyumba na viwanja!!!!

  watati! nadhani ulimaanisha WAKATI?
   
 5. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kutokana na maelezo yako inaonekana uko nje ya nchi na najua umesevu vijisenti vya kutosha. Sasa nakushauri ukanunue viwanja sehemu zilizopimwa. Waweza kununua kiwanja kwa mtu na unapompa pesa naye anakukabidhi "original documents" zote za umilikaji wa hicho kiwanja na ufanye "process" ya ku-"transfer ownership" kwa kupitia kwa mwanasheria. Na kama unataka kununua nyumba, kanunue kwenye mashirika kama vile NSSF au NHC tena ni bei nafuu kuliko kwa watu binafsi. Hapo utakuwa umeepuka mambo ya "kuingizwa mjini".
   
 6. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #6
  Mar 22, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  nyumba zenyewe za National housing ziko wapi wajemeni, na mimi natamani ninunue kamoja
   
 7. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #7
  Mar 22, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Gonga HAPA kwa taarifa zaidi
   
 8. Nyati

  Nyati JF-Expert Member

  #8
  Mar 22, 2010
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 2,044
  Likes Received: 383
  Trophy Points: 180
  Uwe makini hata Wizarani kuna genge la kuibia watu ambao wanafanya dili na wezi hao, ingawa sasa hivi wamepungua sana. Kuhusu kuingizwa mjini inabidi uwe makini na uombe. Unaweza pewa doc halisi lakini baadae akaja mtu akadai ni mali yake. Hivyo njia rahisi ni kuhusisha mawakili ambao watambana vilivyo muuzaji na kupata ukweli. Pia kama kimepimwa lazima ufanye "Official Search" wewe mwenyewe usitume mtu yeyote hasa madalali waepuke kabisa. Nenda wizarani, lipia shilingi 5,000/= wakupe stakabadhi kwa jina lako halafu subiri wiki mbili hivi nenda kachukue taarifa rasmi, kama una haraka waweza kuwatip wakufanyie haraka

  Ukishakuwa na uhakika mwambie muuzaji uende nyumbani kwake kabisa. Mshutukize kuwa unataka document yeyote yenye jina lake, siyo hati, kama ni kitambuklisho fanya utafiti wa kazini kwake. then compare, kama kuna tofauti usikubali hadithi zozote tambaa. Kama hakuna ndipo uende kwa wakili muandikishane. Mimi nilikoswa koswa ndiyo maana nakuonya ndugu yangu. Nusu Nivalishwe mkenge Millioni nane nikajagundua ni kiwanja cha ofisa mmoja yupo nje. Pia jamaa yangu alinunua na kupewa docs halisi kabisa akaanza kujenga wakati nyumba imefikia kwenye mtambao wa panya akaja mwenyewe bahatisha nani Afande mwenye nyota zake ambaye alihamishiwa mikoani mwaka mmoja uliopita. Akavunja na jamaa akalia tu. uwe makini !!!!
   
 9. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #9
  Mar 22, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Kubali gharama ya kuwa na mwansheria wako kama consultant kwa maswala kama hayo, vinginevyo mtauziwa watu watano kiwanja kimoja.
   
 10. Abraham

  Abraham Senior Member

  #10
  Mar 22, 2010
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 115
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nashauri kabla ya kukabidhiana pesa na hizo documents kama hati ya kiwanja n.k tafadhali fanya title search pale wizara ya ardhi uone na kujiridhisha kuwa hicho kiwanja kiko kwa jina lake pale ardhi... maana mjini hapa unaweza ukapewa hata hati then ukajakuta ni batili at the end of the day na huyo bwaba/bibi aliyekuuzia unaweza usimpate tena kama sio hata jina alikupa jina feki.
   
 11. Abraham

  Abraham Senior Member

  #11
  Mar 22, 2010
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 115
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nashauri kabla ya kukabidhiana pesa na hizo documents kama hati ya kiwanja n.k tafadhali fanya title search pale wizara ya ardhi uone na kujiridhisha kuwa hicho kiwanja kiko kwa jina lake pale ardhi... maana mjini hapa unaweza ukapewa hata hati then ukajakuta ni batili at the end of the day na huyo bwaba/bibi aliyekuuzia unaweza usimpate tena kama sio hata jina alikupa jina feki.
   
 12. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #12
  Mar 22, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  tunafaidi wengi hapa wajameni. asanteni.
   
 13. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #13
  Mar 22, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  kama kuna wanasheria hapo tunaomba mtusaidie wajameni, safi sana kwa mtoa mada inatusaidia wengi humu
   
 14. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #14
  Mar 22, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  nashukuru sana wajameni. naomba ushauri zaidi lakini. hasa wa kisheria.
   
 15. m

  major mkandala Member

  #15
  Mar 22, 2010
  Joined: Mar 6, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
 16. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #16
  Mar 22, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  uyu si mganga wa kienyeji huyu, manake haifunguki lakin nahisi ni kitu kama dr. manyuki vile, what is this website for sir?
   
Loading...