Kuingiza Pesa Mtandaoni Kupitia Blogging: Muongozo Kamili

Kainetics

Senior Member
Jun 20, 2022
131
259
Kainetics - Kuingiza Pesa Mtandaoni Kupitia Blog.jpg

Kama wewe ni kijana ambae umekuwa always interested na kujiingizia pesa online ila kwa bahati mbaya hujawahi taka jaribu maana umekua ukioanisha 'kuingiza pesa mtandaoni' na hizo HYIP Investments, MLM's na hizo App zinapromiss kulipa ukifanya tu task twa ajabu ajabu kwenye simu...

Basi nadhani kitu cha kwanza ambacho tutaanza nacho rasmi ni Blogging. Maana kwenye vitu vyote ntakavyoshare, hiki ndicho nakijua vizuri kuliko hayo mengine. Maana nimeanza toka 2012.

Kabla sijaendelea; hii ni part ya masterclass yangu ya bure inayoendelea kwenye channel yangu ya Telegram. Kama uko Interested waweza jiunga HAPA.

Tutakayoongelea humu ni pamoja na;

✍️ Blogging ni nini: Uzuri na Changamoto Zake

✍️ Baadhi ya misamiati unayopaswa fahamu

✍️ Unawezaje Anzisha Blog Yako

✍️ Namna 5 za uhakika unazo weza tumia kuingiza pesa kupitia blog yako

✍️ Namna ya kudeal na changamoto kadhaa kama SEO kuvuta Visitors(na CPC kama utakuwa unatumia AdSense)

✍️ Maswali na Majibu (Yakiwepo)

Kivyangu vyangu, ninazo blog nne ambazo nna manage na wenzangu watano. Tatu ni za Kingereza na moja ni ya Kiswahili.

Mambo yote nitakayoshauli humu kuanzia selection ya jina, branding kununua hosting na domain, kundika .... Kushare content zako, na kuanza ingiza hela ni mkusanyiko wa yale yote ninayotumia, ambayo kwa namna moja au nyingine yamenisaidia kuingiza walau $450 kwa mwezi kupitia matangazo ya Adsense, kama $255 kwa mwezi kupitia Affiliate Commissions na walau kama Tsh350,000 kwenye blog ya Kiswahili.

** $1 ni sawa na Tsh2,250

NB. Hii sio namna ya kujiingizia pesa kwa haraka, unawekeza muda wako na bidii kwenye ku nourish blog post zako, kuvuta visitors na hizo hela. Ukiwa serious , inaweza kugeuka kuwa kazi yako au hata part time job inayokupa hela ya matumizi mengine mengine: madogo na makubwa.

✍ Blogging Ni Nini?

Hii ndio namna ya kutengeneza pesa mtandaoni ambayo imekuwepo kwa kipindi kirefu mno. Watu ambao wanapenda kuandika, hufungua blog na kuanza kuandika kuhusu mada maalumu wanazo penda, mfano Mahusiano, Biashara, Michezo, Muziki na Habari. Mfano wa baadhi ya Blog maarufu kwa hapa Tanzania ni pamoja na MillardAyo, Bongo5 na Mwananchi.

Ila kumiliki blog, sio mpaka uwe unapenda kuandika. Wengi waaopenda, kama nilivyoelezea hapo juu, hawafungui blog kwa ajili ya fedha bali kama personal space wanako weza ongelea experience zao mbali mbali kwenye maisha ambazo zitakuwa zikifuatiliwa na wale wanaopenda blog husika.

Sio kila blogger utakaekutana nae anafanya hii kitu kwa kuwa anapenda, bali kama biashara. Yaani unaunda blog inakaa sawa kuanza kuingiza pesa nawe unatulizana kwa muda au kuendelea kuweka juhudi kuingiza pesa zaidi. Ila kabla hatujafika huko kote, tuongelee misamiati kadha wa kadha ambayo itabidi ujizoeze likija swala zima la Blogging;

Baadhi ya Misamiati ya Msingi Kwenye Blogging

💸 Website/Tovuti - Ni mjumuiko wa kurasa zaidi ya moja ambazo hupatikana kwenye domain moja mtandaoni zinazomilikuwa na mtu au shirika moja. Mfano Google ni tovuti, au Facebook au Mwananchi.co.tz na hata YouTube.

💸 Blog - Blog ni sehemu au aina ya Tovuti ikiwa ni ukurasa mtandaoni ambako makala zinazoandikwa na muda mwingi huambatana na picha, uwekwa. Kama blog inajitegemea, basi itakuwa na kurasa za ziada kama Contact Us, About Us, Home Page na T& C

💸 Domain - Hii kuilezea kiurahisi, ni kile unachoandika kwenye browser ili kuiacess tovuti fulani. Mfano nikiandika www.youtube.com hio ni domain itakayonipleka kwenye tovuti ya Youtube moja kwa moja.

💸 Domain extension - Domain ina sehemu tatu; prefix, middle na suffix. Sana sana Prefix zote huwa n www. mbayo sio ya lazima. Middle ikiwa jina la tovuti husika na mwisho kabisa Suffix kujulikana kama Domain extension. Hivyo ni ile .com kwenye youtube.com na inaweza kuwa . org/. net/. go. tz/ .one na kadhalika.

Top Level Domains huuzwa kwa almost $8/mwaka. Japo ukiwa unanza, waweza anza na subdomain za bure pia.

💸 Web Hosting Provider - Hizi ni kampuni ambazo hutoa space kwenye server ambako data za blog yako hutunzwa. Zipo kampuni tofauti baadhi ya zile zinazoongoza kuwa BlueHost, Hostgator, NameCheap na Hostinger. Japo zipo za bure kama WordPress, Blogger na InfinityFree.Net ambazo zina faida na changamoto zake pia.

Kwa kawaida Hizi Hosting Plans huanzia walau $2.85/Mwezi.

💸 CMS - Hiki ni kifupisho cha neno Content Management System, ambayo ndio aina ya software utaayoinstall kwenye server ili uweze endesha blog yako. Zipo CMS maarufu kama WordPress, GhostCMS na Blogger. Hizi zote ni za bure kuinstall kwenye host kupitia CPanel.

💸 Ninche - Hii ni kategoria specific ambapo blog yako itakuwa ikijihusisha. Mfano Michezo , Burudani, Mahusiano, Uchumi , nk ni kategoria, ila Ninche ni ile kategoria ndogi ndani ya kategoria kubwa.

Mfano; Burudani>Michezo>Mpira wa Miguu>Mpira wa Miguu wa Kiume> SimbaSC Fan Content

Hapo SimbaSc Fan Content ndio Ninché ikamaanisa utakua ukiongelea habari za Simba tu kwenye blog yako. Hii inakuwa nzuri baadae ukiwa tayari kuanza kuingiza pesa.

Zipo nyingine kibao kama SEO, CTR, CCP, ALD, DA, PA , Liquidity, Backlinking, Copy Writing, GhostvWriting, nk... Ila kwa kuanza nadhani sio mambo unayoapaswa jichanganya nayo.

Unawezaje Kuanzisha Blog Professional?

Well, kwa haraka haraka zipo hatua 5 za msingi unazobidi ufuate lkija swala la kuanzisha blog. Ambazo nitajaribu kuziongelea kwa kifupi.

💳 Initial Planning - Kwenye hii stage utaplan jina la blog yako, blog yako itakuwa ikijuhisha a nini, logo yako itakavyofanana, rangi za msingi za blog yako na target audience yako iko nchi gani, posting schedule yako nk. Baada ya kuyaweka sawa hayo yote inafuata step two.

💳 Backend Setup - Hapa utajihakikishia kununua hsting plan iliyotulia, walau kulipia hata miezi mitatu ya kwanza (@ $2.95/Mwezi) . Kudepend na Provider utake tumia, wengi huambatanisha domain bure au kwa punguzo hadi kama $2 hivi mwaka wa kwanza, hivyo sajili domain kama unavyotaka blog yako iitwe mfano; www.kainetics.one . Ukimaliza, install WordPress kwenye CPanel na utakuwa good to go. Kama haya mambo yote ni mageni, waweza mpea Web Designer mwaminifu akufanyie hizi setup process zote.

💳 Front End Setup - Baada ya kumaliza kuweka sawa mambo ya Cpanel, utarekebisha muonekano wa blog yako(kuweka themes, plugins , logo na color palette itakayo match branding palette yako) Hii ni step ya mhimu pia, maana kufika muda unamaliza, blog inapaswa iwe inavutia na iwe haraka kuload na pia iwe na page za mhimu kama contact page, about page, portfolio na privacy policy. Nashauri kutumia Web Designer pia. (FYI, Waeza nicheck kuhusu hili, pia)

💳 Final Touches - Baada ya hayo yote, utafanya Basic SEO practices kama kuunga blog yako na Google Search Console, Google Analytics, JetPack na Kudownload app ya WordPress kwenye simu yako. Nikipata muda naeza elezea umuhimu wa hayo yote hapo baadae.

💳 Anza Kuandika - Andika post zilizopangiliwa vizuri, zilizoshiba na zinazosomeka kwa kirahisi huku zikiwa na urefu unaoridhisha. Kingine ili uweze ingiza hela ya maana, nashauri blog yako iwe ya kingereza. Ushauri mwingine ni kuwa kama umeamua kuongelea mambo ya mahusiano na mapenzi, usije jiamulia siku moja ukaanza nadika kuhusu UEFA au World Cup. Heshimu Ninche yako. Ushauri wa mwisho, andia vya kutosa, pst walau ziwe 30+ kwnye blog yako nxipo uanze ridhika.

So , baada ya kuyafanya hayo yote, blog yako iko hewan, ina post zilizoandikwa vzuri za kutosha, ina load haraka iwezekanavyo na inavutia, nini kinachofuata? Kuingiza Hela.

Ntajaribu onglea namna za uhakika na halisi uazoweza tumia kuingiza pesa kupitia Blog yako ninazotumia.

Namna Blog Yako Inavyoweza Kukuingia Fedha

Likija swala la Blogging, zipo namna kibao unazoweza tumia kuingiza hela. Kama tulivyosema kuwa blog inaweza kuwa sehemu ya tovuti nyingine, basi possibilities hazina kikomo ila hapa naneda ongelea zile ninazotumia.

🏷 Google Adsense

Kama uliwahi tembelea blog yoyote ile ukawa unakutana na matangazo kwenye makala unayosoma, au ukiwa unawatch video ya Youtube, lile tangazo unalo skip huwekwa na hawa Adsense, na ni subdivision ya Google inayojihusisha na matangazo.

Blog hako ukiwa umeifanyia hayo yote niliyoelezea hapo juu, pamoja na SEO, unaweza apply kuanza kuonesha matangazo kwenye blog yako, na kuanza kulipwa kutoka na genuine clicks au impressions utakazokuwa ukipata.

Mambo unayopaswa kuwa nayo ili kuweza unga Adsense ni email yako, account ya bank utakakopokelea hela na sanduku la posta watakapokutumia Verification PIN(hili unaweza tumia hata la mtu mwingine, la kampuni yenu, shirika au hata kanisa ili mradi upokee hizo PIN)

Baada ya kukubaliwa na blog yako kuanza kuonesha matangazo. Ukiwa consistent, unaweza toa hela yako ya kwanza pale utakapofikisha $100. Na inatumia dakka tano hadi siku kadhaa kuingia, but inaingia.

Blog yenye blog posts walau 30, na average visitors per month kuwa 2,000 , na impressions walau 3.5k, huingiza kati ya $250 hadi $550 kwa mwezi ukitegemeana na ukubwa wa CPC ya Blog yako pamoja na Ninché.

$1 ni sawa na Tsh2,250
Hivyo, $250 ni Tsh562,000 /Mwezi.


Sio hela kidogo kama unaipata kwa mwezi. Ukiondoa matumizi ya bando, na costs za kuanzisha blog, unakuwa na faida ya kama 50% kwa mwezi wa kwanza. Kwa miezi itakayofuatia utakuwa na walau faida ya 90% kama bando hutumii kiholela maana hakuna gharama nyingine mbali na muda unaotumia kuandikia, pamoja na hilo bando.

Kama unayo blog, Adsense waweza ungiwa pia.

Kujibu Maswali Baadhi Niliyoulizwa Kuhusu Blogging/Adsense

Haya ni baadhinya maswali ambayo yanajirudia rudia zaidi ya mara moja.

💰 Kama huna hela unaweza anzisha blog na ikakuingizia pesa?

Inawezekana. Nlielezea kuna free options unazoweza tumia kuandika blog posts mfano blogger na WordPress.com ukijiunga watakupa subdomain na utaweza andika makala zako kawaida.

Ubaya wa hizi, ni kuwa huwezi ziunga kwenye Adsense mfano maana wao wanataka ulink domain na sio subdomain. Kingine creative control inakuwa ndogo kwenye hizo blog za bure, mfano huwezi kuedit themes au twmplates kiundani, na subdomain huwa ndefu mno. Mfano badala ya kuwa na domain simple kama kainetics.one, unajikuta una subdmain ndefu kama kainetics.blogspot.com hata wasomaji wako hawawezi ikariri.

So kama uko serious na blogging sikushauri kuanza na hizo blog za bure.

💰 Unaweza Unga Adsense Kwenye Blog ya Kiswahili?

Unaweza kama una traffic ya kufa mtu, hawajali kama ni ya kiswahili au lah. Japo hela ambayo ungeigiza keenye blog ya kingereza yenye metrics sawa na zako, unaweza jikuta unaingia 7% yake maana cpc huwa ndogo mno. Tuseme bot za google na Algorithim yao haielewi kiswahili 😁😁

💰 Nini Kinaweza Fanya Adsense Ikafungiwa.

Mambo yako mengi, japo wakikufungiwa huwa hawasemi ni kwa sababu gani. Na wanaweza wakakufingia hata kama ulikua na hela bado hujatoa.

Kama ilivyo rahisi kuipata account, ni rahisi kuipoteza, ukianza kupata traffic feki, au no follow links zinazo lead kwako zikianza onekana fake. Pia mambo kama kujipa click za uongo, nk vinaweza kukufutia account.

Twende kwenye namna ya pili unayoweza tumia kuingiza pesa kupitia blog yako. Hii ni hata kama blog yako ni ya Kiswahili.

Naenda ongelea kitu kinaitwa; Membership/Subscription.

🏷 Membership/ Subscription

Unaeza kuwa na blog ambayo imeanza kuwa ina vuta visitors wa kurudi wengi wenginl lakini bado ukawa hujajiridhisha kuiunga Adsense na bado unataka uingize hela.

Option ya pili ni pale unakuta blog yako ninya Kiswahili na unawaza pabda ni jinsi gani inaweza kukuingizia pesa. Unaweza fanya hii Membership au Subscription na mambo yakaenda.

Inafanyeje kazi?

Let's say una blog unapoongelea mambo ya mahusiano, nk. Na watu wameanza kuifuatilia. Kuanza kuingiza hela unaweza anzisha group private la WhatSapp ambako unashare concept za kwenye blog kiundani na kujibu au kutatua matatizo ya wasomaji wako. Yote hayo kwa gharama kidogo tu ya hata Tsh2,000 kwa Mwezi.

Kama yale unayofundisha ni mambo ya msingi na wengi wana uhitaji nayo, mtu kutoa Tsh2,000 sio kesi maana anapata zaidi. Kuwa professional zaidi, waeza tengeneza Lipa Namba yenye jina sawa na la blog yako, ila kama sio shida inaweza tumika namba yako tu ya kawaida.

So let's say blog yako imeanza kuwa na wasomaji 300 kwa mwezi.

Kati ya hao mia tatu , tuseme 40% tu ndo wanauwezo wa kutoa hio 2,000 kwa nwezi.

Hivyo , 40% ya 300 ni 120.

120 × Tsh2,000 ni sawa na 240,000 kwa mwezi. Sio hela kidogo.

Na sio mpaka hata liwe group unako fundisha kitu, inaweza kuwa ni Discussion Groups za Ujasiriamali au Biashara ambako watu wanataka wa discuss mambo ya msingi bila kusumbuliwa na matangazo ya wengine. Na bado utaingiza tu hela.

Hii inafanya kazi kwa asilimia kubwa kama blog yako ni ya Kiswahili...maana ku.a changamoto kwenye kupikea hela kwa watu kutoka nje ya nchi.

Idea ya hayo magroup ni kwamba mtu awe kajiunga kwa kuwa anapenda na ni kitu anachotafuta. Na walau hayo magroup yaendane na topic ya blog yako. Yanaweza kuwa magroup mengi (yaani zaidi ya hata mawili) ilimradi value iwe kubwa.

Ninayo blog ya Kiswahili inayongelea maswala ya mahusiano , na kupitia blog hio ninayo magroup matano ya WhatsApp;

1. La Wanaotafuta Wachumba(Tsh.5,000/Mwezi) . Wanakuwemo watu walau 150 wastani kwa mwezi.

2. Lipo la Maswali na Majibu la Wanawake (Tsh500/Mwezi). Limejaa.

3. Lipo la Maswali na Majibu la Wanaume
(Tsh500/Mwezi). Wanakuwemo 130 average kwa mwezi.

4. Lipo la Simulizi (Tsh1,000/Mwezi). Limejaa.

5. Lipo la Ushauri Nasaha (Tsh.2,000/Mwezi). Average wanakuwemo 80.

Unaweza hata fungua group la vijana wa hovyo na bado watalipa . Mbali na blog, hayo magroup yako unaweza yatangaza kwenye social media na utashangazwa na idadi ya watu watakaojiunga.

Kama hujawahi ifikiria hio, waweza itumia.

Kama unajiuliza naezaje manage blog nne, na hayo magroup ninayosema then napateje muda wa kuandika humu , inawezekana.

Ninaunda blog zangu na kuhakikisha ziko presentable. Content za mwanzo naandika mimi na kufanya SEO then unalipa wengine kuwa wanakuandikia kama topic husika hauijui kiundani; Mfano hio blog ya mahusiano wanaadika wadada wawili na wakaka wawili wenye experience 😊. Magroup yanajiendesha. Kikubwa ni mipango.

Namna nyingine unazoweza tumia kuingiza pesa kupitia blog yako;

💰 Kuuza kitabu/course humo humo ndani ya blog(hapa itakubidi uwe na account ya PayPal inayopokea malipo)

💰Ku incorporate Affiliate links kwenye post zako ambazo utalipwa comissions hao visitors wako wakinunua bidhaa kupitia blog yako.

💰Leaderboard Banner Ads. Huwa kuna ile Space ya kwenye header ambapo tangazo la bango kubwa huweza kuingia. Kama una traffic ya kutosha, unaweza lipisha b8ashara mbaoi mbali kuweka tangazo lao hapo.

💰Sponsored Posts. Hapa ni pale ambapo biashara zinakulipa kuongelea bidhaa zao. Mfano kama utakua na blog inahsiana mambo ya simu mpya na computer na una watu wa kutosha wanao kufuatilia, unaweza lipwa na kampuni kama Tecno, Infinix au Itel kuongelea simu zao kwenye blog yako. Sio mpaka wakulipe kwa hela pia, wanaweza kukupa simu zenyewe.

Itimisho

Hio ndo Blogging kwa Marefu na mapana yake. Japo yapo mambo mengi unayopaswa endelea jifunza kama namna ya kuoata organic traffic, kuandika makala zilizoshiba, kufanya keyword research, kupima d.a na p.a ya blog yako. Na hata kupata do-follow na no-follow links.

Kama kipo kitu sijaongelea au una swali, dukuduku au maoni; karibu.

Nawasilisha.
 
Asante sana kwa kushea maarifa haya bure...

Kwa kuongezea tu: Blogger inabidi uwe creative, ujitangaze na uwe consistent katika kuandika na kupost. Na fanya kila uwezalo uijue hadhira yako vizuri na uipe inachokitaka. Tena uwe mvumilivu maana yaweza kukuchukua muda mpaka uanze kuwa na consistent viewers na kuanza kuona matokeo.
 
~mkuu hongera kwa elimu,vp Google domain and workspace inafanyaje kazi kama unauzoefu nayo?
~blog zako ni zipi tukajifunze
 
Asante sana kwa kushea maarifa haya bure...

Kwa kuongezea tu: Blogger inabidi uwe creative, ujitangaze na uwe consistent katika kuandika na kupost. Na fanya kila uwezalo uijue hadhira yako vizuri na uipe inachokitaka. Tena uwe mvumilivu maana yaweza kukuchukua muda mpaka uanze kuwa na consistent viewers na kuanza kuona matokeo.
Hii ni kweli kabisa.
 
~mkuu hongera kwa elimu,vp Google domain and workspace inafanyaje kazi kama unauzoefu nayo?
~blog zako ni zipi tukajifunze
Blog main ziko 3 za kingereza;

Investsmall.co - Hii inaongelea mambo ya biashara na ujasiriamali na nime target West African viewers. (Adsense yake ndo hio Screenshot ya kwanza)

Freeplugins.in - Idea ya hii nlikuwa nataka sajili domain ya freeplug.in ikawa imechukuliwa so nikaweka hivyo Hii inatarget worldwide, na humu nashare pluins na themes kwa ajili ya WordPress (Adsense yake ndo hio Screenshot ya pili)

Fortmi.com - Hii ndio blog ya tatu, humu naabdika content zinazolenga kufanya business online na ujasiriamali kiujumla. Hii haiko linked na Adsense, bali info links. Naitumia kufanya lead generation na email marketing .

Blog ya Kiswahili nisingependa kuiassociate humu. Maana ni product itokanayo na Teamwork(hii ndo inadeal na kuunganisha hizo premium WhatsApp Groups)

Ya mwisho, ambayo haihusiani na hizo nne, ni hii ya kainetics.one ambayo nimeanzisha kuongelea mambo ya kumake money online, maisha na ujasiriamali, kwa Kiswahili. So unaweza ipitia(Though bado sijamaliza weka content)
 
~mkuu hongera kwa elimu,vp Google domain and workspace inafanyaje kazi kama unauzoefu nayo?
~blog zako ni zipi tukajifunze
Kuhusu Google Domain na Workspace, nisingeshauri kuzitumia in relation to blogging maana ni service zilizoanzishwa kutarget makampuni na corporate entities.

Hio WorkSpace kuboost Workflow ndani ya kampuni kwa kuincorporate premium verions ya hizo Google Products tulizozoea kama GMail Premium, Google Docs, Joomla, Google Meet na Google My Business.

Google Domains ni registration service kama unavyosikia GoDaddy , BlueHost au NameCheap. Kama hutoitumia kwenye mambo related na workflow ya biashara, nk. Itakutesa.
 
Unyama mwingi
Kuunda na mpk kuifikisha hapo blog gharama zake zipoje
Gharama ziategemea na features ambazo utataka blg yako iwe nayo . Ila za msingi kabisa ni ;

$8/Mwaka kwa Ajili ya Domain. (Baadhi ya Webhost wanatoaga offer mwaka wa kwanza una sajili kwa kama $0.99 hadi $2)

$2.95/Mwezi Kwa Ajili ya WebHosting. Ambapo nashauri uanze na walau miezi mitatu, so $8.85

Kama utamlipa Web Designer kumalizia hio Setup ya blog, gharama huchezea kati ya Tsh155,000 hadi Tsh350,000 (Inategemea na unataka nini extra kwenye hio blog yako)

Kama utafanya mwenyewe hio Setup, unaweza tenga kama;

$25 ya Premium Theme
$15 ya Premium Plugin kama Yoast SEO, etc.

Hapo blog inakuwa ready kuanza kutumika kibiashara.

So, ni $2+$8.95+$25+$15 = $50 hivi ukifanya kila kitu mwenyewe. Ambayo ni kama Tsh110,000 hivi.

Au unaweza mlipa IT, ili kupata results zilizotulia ambapo itakugharimu hio $10.95(Domain na Hosting) + Hela ya Web Designer ambayo ina range kwenye Tsh155,000 hadi 350,000. Iliyo vizuri kuanza kutumika Adsense, ikadirie Tsh235,000 .
 
Hiv ipoje kwa mfano ukiwa na website ya mambo ya porno kama xvideo vile huwa wanaingiza kias Cha pesa blog kama zile

Sent from my TECNO KD6 using JamiiForums mobile app
😀😀😀😀

Tovuti za hivyo zina pesa kuliko karibia nyingine zite maana target audience yake ni kubwa na traffic iko constant. Shida ni kwamba nyingi zinaweza kukupelekea kufungwa au kufungiwa maana sheria zake haziko constant. Karibia kila nchi wana guidlelines zao kuhusu NSFW content.

Ila ukitaka ugusie hizo mambo, ni ile kuandika Explicit content ambazo sio R Rated. Labda ushauri kwa wanaume, sijui wadada au wanandoa, etc. Nazo hizo zina traffic nyingi maana vijana wa hovyo ni wengi 😊

Ukishajua utakavyo monetize hio traffic yote unakua umemaliza. (Kama traffic ni wadada sana sana utakuta wana promote cosmetics na kwa wanaume ni hizi mambo za viagra, lengtheners etc.)
 
Back
Top Bottom