Kuingilia sekta binafsi kwenye biashara, basi futeni soko huria

chizcom

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
7,581
15,720
Ni kichekesho sana kusikia mtu akishtaki hospitali isiyo ya Serikali kuwa wana bei. Basi V8 na Passo ziwe bei sawa na tupeleke polisi japani kuwashitaki maana yote ni magari.

Tunajua soko huria kila mtu anapanga bei yake kutokana na sera ya private service sector (PSS) kulingana na huduma na mpaka kimefika pale, serikali jukumu lao ni kodi ambayo taasisi yenu TRA kuleta hesabu zenu inatakiwa kutozwa vipi.

Suala ambalo nimeshangaa kuishutumu tena kufungua jalada kama si la “hujumu uchumi” maana hakuna zaidi ya hilo. Kutaka kulinganisha hospitali zenu na za watu binafsi ziwe sawa ningependa kuona labda mmekuta Muhimbili ilo suala mkataamaki maana hii si private sector service.
 
Wanatafuta mahali pengine pa kupiga fedha kwa 'kuongea'na DPP kwani ile singo ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha haimpati mtu tena.
 
Wanashindwa kuondoa 6% ya riba kweny bodi ya mikopo, wanashindwa kuondoa makato ya wizi ya 2% wanayo katwa Wafanyakazi kila mwezi kutoka vyama vya Wafanyakazi! wanaenda kupambana na hiyo Hospitali!!

Kwani hao wagonjwa wanalazimishwa kutibiwa huko? Si wanavutiwa kwenda huko kutokana na huduma bora zitolewazo!! Kuna wakati Serikali nayo inatakiwa kupunguza mihemko. Sidhani kama kuna Mtanzania atakaye kubali kwenda kutibiwa Hospitali yenye gharama kubwa na kuacha ile yenye gharama za kawaida.
 
Ila kwa hapo Agakhani wanatafuta vita kama vile vya sukari na korosho ambavyo tulishindwa
 
Sector binafsi ipo hoi!
7654.jpg
 
walianza shule sasa wanaingia sekta afya, dawa ni kuboresha huduma za umma huwezi kulazimisha mtu aende sekta binafsi wakati ana uwezo na hali kilaanajua madudu ya sekta za umma
 
Kuna huduma lazmima serikali ifanye regulation vinginevyo mtatunyonya sana. Ni kama tu inavyoregulate bei ya energy
 
Back
Top Bottom