Kuingia kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa sio suluhisho la matatizo ya Zanzibar

aleesha

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
776
1,121
Binafsi naomba nisikubalieni na wewe (ACT kukukubali kujiunga SUK) kwa sababu zifuatazo. Imeandikwa na Abdulrahman A. Mohamed. Huu ni uchaguzi wa tano, na kwa msimamo wa CUF/ACT miaka yote CCM haishindi. Katika chaguzi 5 au 6 zilizopita (ukiwemo huu) baada ya CCM kuingia madarakani (sio kabla) wamekuwa wakipendekeza suluhisho, sasa tupitie masuluhisho yaliyopita: A. MUAFAKA Muafaka huu wa 1995 ulisimamiwa na viongozi wa Commonweaalth na kufikia makubaliano.

CUF/ACT ilitekeleza makubaliano yote ya muafaka, CCM ilikiuka makubaliano mengi ya muafaka, kwa mfano waliovunjiwa nyumba na kuharibiwa mali zao walitakiwa kupewa fiidia, mpaka leo hakuna aliyepewa fidia. B. KAMATI YA MARIDHIANO Kamati hii iliundwa kuondoa tofauti kati ya Wazanzibari, wajumbe wa CCM walikuwa Marehemu Mzee Moyo, Mansour na Riyami, na CCM walikuwemo kina Jusa. Muda mfupi baada ya kamati hii kuonekana kupata mafanikio, katibu mkuu wa CCM Wakati huo Philip Mangula alitangaza kutoitambua kamati ile iliyoleta tija kubwa kwa juu ya madai ya Zanzibar katika katika Mpya iliyokuwa ikijadiliwa wakati ule, mpaka CCM Zanzibar wakawa wanataka serikali 3.

Mwisho wa yote ni kuwa CCM iliwashawishi wanachama wao kurudi kwenye msimamo wa serikali 2 kuelekea 1, Masour, Marehemu Mzee Moyo, Riyami na Mwanasheria Mkuu wa Wakati huo ndio viongozi wanne pekee waliondelea na msimamo wa kuitetea Zanzibar na hivyo wakalazimika kutoka CCM. Na huu ndio ukawa mwisho wa madai ya Zanzibar, katiba Mpya “ikavunjika” na hakuna lililokuwa.


C. SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA Lengo la serikali ya umoja wa kitaifa lilikuwa ni kuondoa tofauti za kichama (partisanship) kwa maslahi ya Zanzibar. Nakumbuka Maalim katika hotuba yake alisema IMESHINDA ZANZIBAR, HAIKUSHINDA CUF WALA CCM. CUF wakakubali CCM iendelee kutawala kwa makubaliano mengi ikiwa ni pamoja na kuuundwa kwa tume huru ya uchaguzi na mambo mengine mengi. Nizungumzie hili la tume huru. Kweli tume huru iliundwa uchaguzi ukafanyika, huu ni uchaguzi wa 2015, Wakati kura zinaendelea kuhesibawa ilidhihirika kuwa CCM inashindwa, Jecha alitangaza kufuta uchaguzi.

Baada ya uchaguzi kufutwa, kikaundwa kitengo cha siri na kisicho rasmi cha mazombi, watu wakapigwa, wanawake wakanajisiwa na wengine wakabambikiwa kesi za ajabu ajabu, kina Sheikh Farid wote wako ndani mpaka Leo (Wengi mshaanza kuwasahau) USHINDI WA WAZANZIBARI ALIOUTANGAZA MAALIM SEIF UKAFUTWA. Sasa kwa nini naeleza yote haya. Sababu ni kuwa CCM inaonekana kutaka ushirikiano “Feki” pale wakishamaliza malengo yao ya kuchukua serikali, HII NI HADAA NA SI USHIRIKIANO WA ROHO SAFI. Hivyo basi: 1. Huu ni mtego utakaowanufaisha CCM peke yao ili kuhalalisha utawala wao.

ACT inaingizwa kwenye Serikali kama “KANYA BOYA” na si ushiriki halisi. 2. Kitakapomalizika kipindi cha miaka mitano, wataiba tena, watapiga, wataua, watanajisi wanawake, watawatia watu ndani, kisha watachukua serikali tena. GNU SIO SOLUTION YA MATATIZO YA ZANZIBAR, KAMWE ZANZIBAR HAITOKUWA NA HESHIMA, UTAWALA WA HALALI NA KUONDOKA KWA MADHILA PAERMANENTLY KUPITIA GNU YA UTAWALA WA CCM. 3.

Ni wazi kuwa kama alivyoandika muandika mtoa post GNU/SUK ina manufaa yake, lakini pia ni ukweli usiopingika kuwa manufaa haya huwa ni temporary na sio ya kudumu, Mpaka lini tutaendelea kupendelea temporary solution na ZANZIBAR INAENDELEA KUZAMA? Hata ACT ikiingia kwenye GNU au SUK haya ndio yatakayotokea:

a. ACT haitoweza kutekeleza sera hata moja ya chama chao ndani ya serikali hii. Mathalan ni msimamo wa ACT kuwa na serikali 3 katika muungano na Zanzibar kuwa na mamlaka kamili. Hili halipo na ikibidi CCM watatuua sote kuzuia hili lisitokee.

b. CCM itaendelea na mwenendo wake ule ule kwa Zanzibar. Sote tunaujua.

c. Waliodhulumiwa ndio washadhulumiwa ACT haitoweza kuendelea kutetea haki za waliodhulumiwa wao wakiwa washiriki katika serikali.

d. Kuingia kwenye SUK, symbolically ni KUKUBALIANA NA YOTE YALIYOTOKEA KWENYE UCHAGUZI, KUANZIA MAUAJI MPAKA UPIGAJI WA KURA.

Is it worth it kujiweka hapo kwa umakamo wa rais, wizara mbili na wawakilishi 5? Hebu vuta fikra na muweke aliyeuliwa ni baba yako na aliyebakwa ni mkeo au dada yako au mama yako? Ni nani ambaye angekubali kushirikiana nao baada ya kufanyiwa moja kati ya haya? Wanachofanya CCM ni hichi: nimemuingilia jamaa dada yako au mkeo, nimemuua ndugu yako, nimedhulumu mali zako zote na nimepora nyumba yako (kuiba kwenye uchaguzi) halafu ninakupa banda la uani ukae ndani ya ile ile nyumba yako niliyoipora na wewe unakubali. Hii ndio SUK au GNU.

Kupewa chumba banda la uani ni kuongeza maumivu ya dhulma kwa walioguswa na dhulma ile. Narudia tena: KUINGIA KWENYE SUK SIO SULUHISHO LA MATATIZO YA ZANZIBAR. Nami haya nido mawazo yangu. Nini maoni yako katika hili?
 
Watu wanataka vyeo,awataki kumaliza matatizo ya Zanzibar.kila mwaka wa uchaguzi Seif anataka yeye ndo awe mgombea.akuna mwengine anaefaa ni yeye tu.
 
Kwa wao kutokwenda kujiunga na Serikali kunatatua vipi changamoto za zanzibar?
 
Back
Top Bottom