Kuingia kwenye siku

Jewel

Senior Member
May 1, 2008
176
62
Nina binti mwenye miaka 18 mwezi huu kapata tatizo la kuingia kwenye siku zake mara 3 ndani ya mwezi mmoja je tatizo hili laweza kutokana na nini? haijawahi kumtokea hapo kabla
 
Kuna sababu nyingi sana zinazofanya mwanamke aone siku zake kuliko ilivyo kawaida yake. Hata hivyo kwa kuwa umeutaja umri wake japo hujasema kama aliwahi pata mimba basi nitataja chache. Na hizi chache nitazingatia sana umri wake. Na hapa nina maniisha kuwa sababu ya kuona damu ya mwezi zaidi ya ilivyo kawaida kwa mtu inatofautiana na amri wa mtu mwenyewe.

Sababu ya kwanza yaweza kuwa ujauzito, ikiwa mimba hiyo imetokea abortion na hakupatwa matibabu, au gestationa trophobalastic disease, au placenta pravea.
Sababu ya pili yaweza kuwa kapata uambukizo (cervicitis, au endrometritis) but hizo kutakuwa na dalili zingine kama maumivu chini ya kitovu pamoja na kutokwa na uchafu na wakati mwingine uchafu huo huwa na harufu.
Sababu ya tatu ni matumizi ya dawa za majira kama vipandikizi, au Depo au vidonge. Na kwa vidonge ni pale anapomeza vidonge bila ya kufuata mpango. Tumeona watoto wa umri huo wakiwa na bleeding ya mara kwa mara kwasababu vidonge hivyo hawavimezi ipasavyo!!!. wanameza wakikutana na mwanaume tu hivyo kusababisha hormonal interruption !!!! Na hasa wale watoto wa geti kali!!!!
Sababu nyingine ni msongo wa mawazo (stress) pamoja na nyingine nyingi.
Cha kufanya chunguza kama ana mimba, ni rahisi waweza nunua kipimo kile cha mkoja kutoka duka la dawa lolote na mkupima mimba. Kama hana mimba chunguza kwa makini kama anameza vidonge vya majira.
Kama uchunguzi huo haukugundua kitu basi mpeleke Hospitali kwa sababu uchunguzi mwingine huwezi ufanya wewe mwenyewe.
 
Nashukuru sana kwa majibu hana mimba na wala hajawi kupata mimba pia anasema na tumbo linamuuma .Tahnks again kwa majibu
 
haka kamegeuzwa muhimbili kadogo,watu wanaacha kwenda hospitali wanataka ushauri!
 
Back
Top Bottom