Kuingia kwenye ndoa ukiwa na miaka chini ya 25 ni sawa na kuoka disko saa 3 usiku

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,596
154,853
Hebu fikiria,
umetoka kwenye maisha ya kuchungwa na baba na mama, hali kadhalika hujafurahia maisha na wala huyajui kwani ulikuwa masomoni kwa muda wote.
Halafu ghafla unaingia kwenye kifungo kingine cha ndoa, hii ni sawa kabisa na kuingia kwenye disco la kukeshasaa mbili na nusu usiku na kisha kutoka saa tatu usiku.
Ili uwe kijana uliye mkamilifu, ni lazima uenjoy maisha yako mwenyewe na uhuru wako binafsi.
 
na wanasema ETI ukifikisha miaka 27 hujaolewa huolewi tena

ko its only 2 years hapo

Umeona eeeee lakin kuolewa mapema napo raha unafaidi mapenzi bado mkiwa vijana, sasa wanataka tuolewe tukiwa na miaka 60 kama yule bib wa CCM jamani hata kumkatikia mume tabu,,
Raha ya ndoa damu iwe inachemka banaa
 
lengo likiwa kwenda disco na kucheza mziki wala haina tabu, Ila kama unaenda uonekane..
 
Hapa Napata shida kuelewa akili zetu watz zikoje. Mtu zaidi ya miaka 20 bado anajiona mtoto tuuu????.miaka hiyo ya kujijengea maisha Kijana anawaza Disco, pombe na uzinzi???? Kaaaazi Kweli kweli
 
Hebu fikiria,
umetoka kwenye maisha ya kuchungwa na baba na mama, hali kadhalika hujafurahia maisha na wala huyajui kwani ulikuwa masomoni kwa muda wote.
Halafu ghafla unaingia kwenye kifungo kingine cha ndoa, hii ni sawa kabisa na kuingia kwenye disco la kukeshasaa mbili na nusu usiku na kisha kutoka saa tatu usiku.
Ili uwe kijana uliye mkamilifu, ni lazima uenjoy maisha yako mwenyewe na uhuru wako binafsi.

kweli aisee,presha za ndoa cpend kabisa
 
Kiufupi ni vizuri sana lakini. Mfano unapata mtoto wako wa kwanza wa halali wa ndoa ndani ya 25, it means mtoto anapo graduate wewe utakuwa una 45 kwahiyo unakuwa hujastaafu na una uwezo mkubwa sana wa kuwa mchango mkubwa sana kwake na kwa wanao watakaofuata.
 
Hebu fikiria,
umetoka kwenye maisha ya kuchungwa na baba na mama, hali kadhalika hujafurahia maisha na wala huyajui kwani ulikuwa masomoni kwa muda wote.
Halafu ghafla unaingia kwenye kifungo kingine cha ndoa, hii ni sawa kabisa na kuingia kwenye disco la kukeshasaa mbili na nusu usiku na kisha kutoka saa tatu usiku.
Ili uwe kijana uliye mkamilifu, ni lazima uenjoy maisha yako mwenyewe na uhuru wako binafsi.

watoto wa getikali shida kweli kweli....wenzako disco tumeenjoy sana tukiwa u 18 hadi sasa tumechoka
 
Back
Top Bottom