Kuimarika uhusiano wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuimarika uhusiano wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Discussion in 'International Forum' started by mdau wetu, May 19, 2011.

 1. m

  mdau wetu JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 548
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuimarika uhusiano wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar [​IMG]Kampuni ya Iran ya Amvaj Buraq inayotengeneza boti za Faiba, imefikia makubaliano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kujenga chelezo kwa ajili ya matengenezo ya boti zinazosafiri katika pwani ya Afrika Mashariki.
  Hayo yameelezwa na kiongozi wa ujumbe wa kampuni hiyo Kepteni Ali Muhammadi wakati alipofanya mazungumzo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi jijini Dar es Salaam.
  Kepteni Muhammadi amefafanua kuwa, mbali na kujengwa chelezo hicho, taasisi zinazohusika na uwekezaji nazo zitapatiwa fursa ya kukutana ili kuandaa utaratibu wa makubaliano ya kuanzishwa miradi mingine mbalimbali kati ya Iran na Zanzibar.
  Kwa upande wake, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameelezea kufurahishwa kwake na utekelezaji wa haraka wa makubaliano yaliyofikiwa kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
  Mikataba hiyo ilifikiwa wakati wa safari ya Balozi Seif Iddi nchini Iran.

  Kwa hisani ya Idhaa ya Kiswahili ya Radio Tehran, Iran (kiswahili.irib.ir)
   
 2. Yusomwasha

  Yusomwasha JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2015
  Joined: Dec 5, 2014
  Messages: 2,131
  Likes Received: 621
  Trophy Points: 280
  safi sana
   
 3. Yusomwasha

  Yusomwasha JF-Expert Member

  #3
  Jun 21, 2015
  Joined: Dec 5, 2014
  Messages: 2,131
  Likes Received: 621
  Trophy Points: 280
  israel hata kikombe hawawezi kutengeneza
   
Loading...