Mdudu halisi
JF-Expert Member
- May 7, 2014
- 2,730
- 4,768
Ndg zangu wana JF,
Natumaini nyote ni wazima wa afya njema.
Naomba nitumie nafasi hii kuwafahamisha watanzania wenzangu kwamba kwa mwenendo huu wanaouonesha Chama Cha Mapinduzi katika kipindi hiki cha cha Awamu ya Nne, ni dhahiri ya kwamba Wapinzani wana safari ndefu ya kuhakikisha wanaingia Ikulu. Katika uhalisia wake CCM imeendelea kukubalika vijijini na mijini hasa kutokana na utekelezaji usio wa kubabaisha wa ilani yake ya uchaguzi.
Mifano halisi ya hivi karibuni inayoonesha ni jinsi gani wananchi wamejenga moyo wa matumaini kwa chama hiki ni vile kilivyoweza kujizolea kura lukuki katika chaguzi za Madiwani katika kata 27 pamoja na chaguzi ndogo za wabunge zilizofanyika katika jimbo la Kalenga na Chalinze.
Lakini kama hiyo haitoshi, wananchi wamekuwa wakijitokeza kwa wingi katika mikutano mbalimbali ya CCM inayoendelea kote nchini, mfano mzuri ni mikutano ambayo Katibu Mkuu, Comrade Abdulrahiman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Mh. Nape Nnauye wameifanya katika mikoa ya Tabora na Singida ilivyohudhuriwa na wananchi wengi wapenda maendeleo
. Mahudhurio haya ni yamethibitisha kwamba watanzania wengi wana imani na Chama Cha Mapinduzi na kwamba ndicho kitakachowakomboa toka kwenye lindi la umaskini.
Comrade Kinana na Nape walikuwa katika ziara ya kukagua uhai wa chama pamoja na kukagua utekekelezaji wa ilani ya uchaguzi ambapo wamekagua utekelekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya za mikoa Tabora na Singida.
Si vibaya pia tukajikumbusha mafanikio haya yaliyopatikana chini ya utawala huu makini wa Chama Cha Mapinduzi;
Kwanza ni ujenzi wa misingi imara ya kiuchumi. Hapa, watanzania wamejionea ubora na uimara wa miundo mbinu, kwa mfano barabara zimeboreshwa kiasi ambacho wafanyabiashara wanauwezo wa kusafirisha bidhaa zao kutoka na kwenda kokote hapa Tanzania bila usumbufu wowote unaosababishwa na ubovu wa barabara hivyo unaweza kujipatia bidhaa yoyote ukiwa popote Tanzania hata kama ni kule kijijini Mbaha, kando kando ya ziwa Nyasa.
Reli nayo imeimarishwa kwa kufanyiwa ukarabati na sasa unaweza kusafiri kwa treni toka Dar kwenda Kigoma kwa muda wa siku mbili tu tofauti na kipindi cha nyuma ambapo ilichukua muda wa siku tatu kutoka Dar kwenda Kigoma. Viwanja vya ndege vya Kigoma na Mtwara vimefanyiwa ukarabati mkubwa ikiwa ni katika kuhakikisha usafiri wa anga unaimarika.
Mafanikio mengine ya CCM ni pamoja na kuondoa kero ya ukosefu wa maji safi na salama kwa wananchi wa maeneo mbalimbali nchini, na hapa tumeshuhudia uanzishwaji wa mradi mkubwa wa maji wa ziwa Victoria ili kuondoa kero ya maji kwa wakazi wa mikoa ya kanda ya ziwa. Katika sekta ya Elimu, serikali ya Chama Cha Mapinduzi imefanikiwa sana kupitia Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) na ule uliohusisha Elimu ya Sekondari (MMES).
Katika kipindi cha kuanzia mwaka 2002 watoto wengi waliohitimu elimu ya msingi wameweza kujiunga na elimu ya sekondari na hivyo kuhakikisha kwamba suala la kupata elimu ni haki ya kila mtoto. Pia kumekuwa na ongezeko la vijana wanaojiunga na Elimu ya Juu, huku Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ikibeba jukumu kubwa la kutoa mikopo kwa ajili ya kugharimia mafunzo na kuhakikisha kwamba vijana wote wanaojiunga na kiwango hicho cha elimu wanahitimu masomo yao.
Pia CCM imefanikiwa kuimarisha utawala bora kwa kuweka na kujenga misingi imara ya kiuongozi na kiutawala kwa kuhakikisha viongozi wanawajibika ipasavyo kwa wananchi. Kiongozi anapokosea huchukuliwa hatua za kinidhamu ama zile za kisheria na pale anapofanya vizuri hupongezwa. Katika kulitekeleza hili, tumeshuhudia viongozi mbalimbali wakipongezwa na huku wengine wakiwajibishwa kutokana na makosa mbalimbali waliyofanya.
Mfano, kuna kesi zinaendelea mahakamani kuhusiana na matumizi mabaya ya madaraka na ambapo wahusika wake ni vigogo kadhaa waliopata kuhudumu kwenye serikali ya Chama Cha Mapinduzi.
Lakini kuimarika kwa miundo mbinu kama vile majengo mbalimbali kwa ajili ya makazi ya watu na ofisi mbalimbali za idara za serikali na mashirika ya umma ni mafanikio mengine ambayo CCM wamejipatia katika kipindi chote cha utawala wao.