Kuikomboa CCM: Watanzania huu ni wakati wa maamuzi magumu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuikomboa CCM: Watanzania huu ni wakati wa maamuzi magumu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by W. J. Malecela, Dec 1, 2011.

 1. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #1
  Dec 1, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - CCM ni lazima ijivue magamba ili kushinda kwa kishindo Mwaka 2015, ni lazima ifike mahali Lowassa na Chenge waondolewe katika nafasi zozote za uongozi wa chama. Lengo la CCM ni lazima liwe ku-invest more in Waheshimiwa kama Januari Makamba, Nape under Supervision ya Wazee kama Sitta, Mwakyembe, na Mwandosya hapa the goal ni kutawala 50 more years. Kwa sababu by then the Nyerere generation itakuwa imekwisha, tutakua na wananchi wasiomjua Mwalimu kabisaa ndipo for the first time CCM tutaanza kupigania kura kwa jasho, my point ni kwamba CCM for that goal haiwezi kuwekeza kwenye mafisadi kina Lowassa.

  - CCM ni lazima ijivue kwa sababu kama hawajivui, then Ninawashauri Waheshimiwa Nape na Sitta wajitoe na kuivunja CCM kwa sababu tupo wengi ambao tunalijali hili taifa tutajiunga nao, Lowassa na mihela yake yote hawezi kuanzisha chama cha siasa, he knows that kwamba ni Dead end, na akitoka CCM anajua kwamba CCM haiwezi kuvunjika, lakini for sure 100%, Waheshimiwa Nape na Sitta wakitoka CCM inavunjika vipande, Je Mh. JK yuko radhi kuona CCM inavunjika under his watch? No! So hawa magamba ni lazima waondoke soon as possible or else!

  - People this is our Nation na saa ya kuhesabiwa ni sasa, hatuwezi kukaa pembeni kuwaachia mafisadi watuamulie the National agenda, kwanza tuliambiwa Rostam hawezi kuguswa cause ana siri nyingi sana za Mkuu wa Kaya, lakini akavuliwa sasa ni wakati muafaka na Lowassa, Chenge na wengine wengi wakavuliwa, we understand the campaign ya Mafisadi kununua watu wengi kila kona ya taifa, ninasema Wenyeviti wote wa CCM Mikoa kuacha Mheshimiwa Makongoro, na Makatibu wao waondolewe na ikibidi wafukuzwe Chama, wote ni compromise wa Lowassa, Wamenunuliwa tayari. Kuondoka kwa mafisadi wote hakumalizi matatizo yote ya CCM, lakini kunafungua njia ya kujipanga kelekea kwenye utawala wa Respect of the Law!

  - Lowassa hajatununua wananchi wote, ninawajua a lot of my friends walionunuliwa tayari shame on you, wewe ndugu yangu ninayesikia umenunuliwa na Shillingi Millioni 100 hivi karibuni na kwamba siku hizi unapewa habari za kuandika na Tanzania Daima, I am shocked na ninakuja soon ninataka tukae uso kwa uso uniangaliae usoni uniambie kwamba hii habari sio kweli, ninajua kwamba Wabunge 75% ya Wabunge wa CCM wamenunuliwa tayari wakiongozwa na Kagasheki ambaye hutamba sana bungeni kwamba hakuna wa kumgusa Lowassa, maaan! you are dead wrong!

  - CCM this is my promise to you, siku Lowassa akipitishwa kugombea Urais nitachukua Bunduki na kuingia msituni and I mean it not in my watch, nilipooona maisha yamekua magumu bongo nilikimbilia Ubaharia, na nilipooona hamsikii vilio vya wananchi nilishiriki kuanzisha kiboko yenu JF, now I am ready kuingia Msituni maana enough is enough!

  MUNGU IBARIKI TANZANIA!

  William @...NYC,USA: Mutuz Le Baharia!
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Dec 1, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,468
  Trophy Points: 280
  its like LOWASSA NDIE RAIS AU MWENYEKITI WA CCM NOW
  too sad kwa kweli.....
   
 3. BBJ

  BBJ JF-Expert Member

  #3
  Dec 2, 2011
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 1,183
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Dah!Mkuu angalia,huyo EL inasemekana anamtandao mkubwa sana,anaweza kukuangamiza hata ukiwa hukohuko.
   
 4. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #4
  Dec 2, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,819
  Likes Received: 36,929
  Trophy Points: 280
  Aisee shuhuli pevu bado inaendelea...:spy:
   
 5. T

  Topical JF-Expert Member

  #5
  Dec 2, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  sasa anayetaka kuchukua bunduki anatangaza??? lol

  Mimi si mshabiki wa lowassa lakini kwanini msifukuze kwenye hadi mchukue bunduki??

  Something must be wrong?
   
 6. Jaluo_Nyeupe

  Jaluo_Nyeupe JF-Expert Member

  #6
  Dec 2, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 2,269
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Hivi ni kweli Mh. Lowasa hagusiki kabisa ndani ya chama hadi itumike bunduki?
   
 7. Kiwi

  Kiwi JF-Expert Member

  #7
  Dec 2, 2011
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 1,009
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Sikio la kufa halisikii dawa. ccm imefikia mwisho wake. Kama ambavyo utawala wa warumi ulifika mahali ukaanguka kwa 'self destruction', chama cha magamba kinaelekea huko. Chama kimekiuka miiko iliyojiwekea. Kimelivunja Azimio la Arusha na misingi yake ya usawa wa binadamu. Kimewageuka wakulima na wafanyakazi ambao ndiyo rasilmali ya chama hicho. Kina lipi jipya litakalofanya leo ili kijikomboe? Hata wakitoka Chenge, Lowassa na mafisadi wengine uliowataja hakitapona.

  Siku CCM ilipoanzishwa 5.2.1977, ninakumbuka jinsi tulivyoshangilia sana. Baada ya TANU na ASP kuungana na kuunda chama kimoja tulifikiri sasa Tanzania kweli itaendelea. Chama cha Mapinduzi, chama cha wakulima na wafanyakazi. Alama zake ni jembe na nyumba. Wafanyakazi na wakulima ndio wenye chama, na ndio walio wengi Tanzania. Nani atakayekiyumbisha. Leo chama kimejaa wezi wasio na haya, wanaoiba mchana mweupe tena kwa 'ridhaa' ya wakulima na wafanyakazi hao hao. Kuna watu wanaridhika na pilau, T shirt na vitenge, ingawa hawana maji, hospitali, shule, nyumba nzuri, hakuna walimu, madaktari, gari za kubeba wagonjwa, barabara, umeme, mishahara hawalipwi n.k. Lakini hao hao wamejaa uwanja wa taifa kuwaona mafisadi wanapokea mwenge eti wa Uhuru, wanasherehekea miaka 50 eti ya Uhuru! Bado tu kuna wanaofikiria ya kuwa kuna chama? Amini usiamini, hao wote waliokusanyika na wanaoendelea kukusanyika kwenye hizo sherehe ni asilimia ndogo sana ya watanzania. Hao hawataweza kukiokoa chama cha magamba hata wakijiuzulu wajumbe wote wa NEC!
   
 8. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #8
  Dec 2, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Well ni lazima kuweka all the options mezani ili wanaohusika waelewe kwamba wakati wa mchezo umekwisha na no way tutachezeana tena kwenye Urais ujao!

  William @..NYC,USA: Mutuz Le Baharia!
   
 9. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #9
  Dec 2, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,468
  Trophy Points: 280
  yaaani ile barabara ambayo gari letu lilikuwa lipo na dereva alikuwa Nyerere 'hatuijui hata ilipo'
  sasa gari linakwenda mbio mno,hatujui dereva hasa ni nani,tunagombania nani awe dereva mwaka 2015
  na njia wala hatujui ni barabara ipi tunayopita..

  mungu atulinde kwa kweli....
   
 10. Noti mpya tz

  Noti mpya tz JF-Expert Member

  #10
  Dec 2, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Duh, kaka William kwa hili mi nakuunga mkono 100% na binafsi nasikitisa sana na mmoja wa waandishi wa makala ktk gazeti la TZ Daima sidhani kama wewe ulimaanisha huyo ila kwangu mimi huyu bwana nilikuwa namheshim sana na kwangu alikuwa ni mwandishi bora wa makala lakini kwa sasa baada ya kuwa amepata chake kwa hao mabwana zake amekuwa kama dodoki linalotoa uchafu mwilini linaubeba lenyewe.
  Najua ccm hawamwezi Lowassa sasa nasubiri wamlete kwenu wananchi sisi tutamuweza tu, pesa zake haziwezi kutununua wote ataishia na hao walio tayari kupeleka ubongo wao likizo kwa sh 100ml na kuanza kubwabwaja magazetini kama vichaa hawa nao siku yao iko mlangoni maana hawatabak salama.
   
 11. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #11
  Dec 2, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,613
  Likes Received: 2,006
  Trophy Points: 280
  He is too powerfull and has proven to be so.

  CCM haimwezi EL, i can almost bet ma life on that.
   
 12. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #12
  Dec 2, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,631
  Trophy Points: 280
  Mkuu William kwa heshima yako na ya jina lako, humu forum tunakuheshimu for who you are not what you are, sasa na wewe unapojiingiza kwenye hizi siasa za maji taka, utajivunjia bure heshima yako na kuturudisha kwenye kumbukumbu za uchafu wa majina makubwa!.

  Niliwahi kuuliza na leo nauliza tena, hivi Lowassa na Chenge makosa yao ni yepi hadi kustahili kusulubishwa ?!.

  Kama kuna wana CCM wana mpaka kesi mahakamani mlisimama kuwaombea kura wananchi ndio wakawapiga chini!, leo mna moral authority gani ya kuwanyooshea vidole Chenge na Lawassa ambao hawajashitakiwa kwa lolote?!.

  Mkuu William, una taarifa kwenye baadhi ya maeneo, CCM inashinda sio kwa sababu inapendwa sana, bali kwa mazoea tuu na ku capitalize on ignorance ya Watanzania!.

  Mnajipa matumaini mkiziba viraka hilo pakacha lenu litaacha kuvuja hivyo mtatawala miaka 50 mingine!.

  By now Watanzania are not as ignorant as they used to be, hivyo mtaji mkubwa ndio huo umeanza kuondoka, mikao ya Kaskazini walishaamka, kanda ya ziwa ndio hao wameamka, mikoa yenye low literacy level kama Dodoma, Singida na mikoa ya Kusini, itachukua muda zaidi lakini hatimaye watafika mahali watalibwaga pakacha la CCM na kulipiga chini puu!.

  Tatizo kubwa linalotukabili Watanzania, hatuna serious opposition parties zenye serious strategies na kutuletea ukombozi toka kwenye ukoloni wa chama dola!. Vyama vyenyewe vya upinzani ndio hivi, kelele nyingi, matendo sifuri!.

  Tusubiri katiba mpya ili hata sisi tusio na vyama tupate forun ya kuwafungua macho Watanzania ili mshuhudie 2015 mtabakiwa na viti vingapi ndipo uje tena humu na hizo ndoto zako za miaka 50 ijayo!.
   
 13. umkhonto

  umkhonto Member

  #13
  Dec 2, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  @William,kama akipitishwa kugombea kwanini usipigie kura chama kingine au mtu mwingine,kwa kuanzia,pigania uchaguzi huru,na haki ya watu kuchaguliwa kama vile mgombea binafsi,halafu akiwanunua CCM wakamteua agombee,wewe pigia kura yako Chadema,ili ashindwe uchaguzi,kama atanunua na mfumo wa uchaguzi hapo tutaenda wote kupigana,na wala sio msituni,bunduki barabarani,lakini ujue CCM sio mwisho wa options kwa nchi yetu,kuna vyama vingine kabla ya kuingia kwenye armed struggle....
   
 14. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #14
  Dec 2, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,290
  Likes Received: 1,444
  Trophy Points: 280
  Cant wait to see Tz developing and flying economy under Pres Lowassa
   
 15. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #15
  Dec 2, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Mkuu William,seem as if kuna personal interests hapa...napata wakati mgumu kidogo kuunganisha dot na dot...sina hakika km tumefika mahali pa kuingia msituni no matter una chuki kiasi gani na huyu bwana...time will tell!
   
 16. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #16
  Dec 2, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,631
  Trophy Points: 280
  Jmushi sio CCM hawamwezi EL bali kama ni uchafu CCM ni wachafu wote na kama ni uwezo wa organization, mass na resources mobilization hakuna anaemzidi EL, ni bahati mbaya tuu JK ndie rais ila hapa tulipo ndipo alipotufikisha na hii ndio proof ya uwezo wake!. EL ni habari nyingine, angekuwepo, tusingekuwa hapa tulipo, tungekuwa mbali sana kwani hata mvua, tungetengeneza!.
   
 17. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #17
  Dec 2, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,613
  Likes Received: 2,006
  Trophy Points: 280
  Mkuu tupo ukurasa mmoja tu,ukiondoa hiyo highlight/bold,basi maelezo yako yana conclude exactly kinyume na hapo kwenye bold,yani sawa kabisa na bandiko langu uliloloquote.

  Kwa kifupi sababu hizo ndo haswa kwanini hawamwezi.
   
 18. Noti mpya tz

  Noti mpya tz JF-Expert Member

  #18
  Dec 2, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  EL tuhuma zake zipo juu ya ubao na huhitaji kuuliza just direct yar eyes on the board utaona si huyo tu tatzo la ccm ya sasa ni kwamba imeachwa ikamalizwa na kansa na sasa hakuna sehem iliyo salama, yaani ni sawa na wanandoa wanaopishana ndani kwenda nje ya ndoa. Leo utasikia EL fisadi, kesho, Sitta ni msaliti kesho kutwa fisadi papa na mtondogoo JK ndo mwenye richmond, kweli bado mnafikiria kuendelea kutawala? watz sasa hawataki kutawaliwa wanataka viongozi bora.
   
 19. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #19
  Dec 2, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,613
  Likes Received: 2,006
  Trophy Points: 280
  Well said mkuu.
   
 20. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #20
  Dec 2, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Mwehu si Muhokota makopo. Umeniacha hoi kakangu. Nape ndie kiongozi bora kwa maoni yako?
   
Loading...