Kuikana Dowans bila kuchukua hatua yoyote ni usaliti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuikana Dowans bila kuchukua hatua yoyote ni usaliti

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Wacha1, Feb 16, 2011.

 1. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #1
  Feb 16, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Hatua ya rais JK kuikana Dowans na kutokuwawajibisha watendaji wake ni kielelezo tosha kwamba yeye mwenyewe binafsi ni mfaidika wa sakata lote hili la kampuni ya kufua umeme.

  Kama angekuwa hahusiki EL, RA na Chenge wasingekuwa wabunge leo hii. Je, anafikiria nini hasa kama sio kuona Tanzania ni shamba lake la kuchuma na kujilimbikizia mali? Kila kukicha anawatumia rafiki zake kutaka kujitajirisha, hivi hii ndio kazi aliyokuwa analilia kwa miaka yote hii, shirika la umeme Tanesco limekuwa kama mpira ambao unatupwa kila mahali ili mradi yeye na maswaiba wake waweze kunufaika kwa mgongo wa chupa huku walala hoi wakitaabika. Iweje basi shirika hili kongwe washindwe kununua mitambo na wategemee kampuni za mfukoni za JK? Sio kweli kwamba Tanesco hawana wajuzi wa kufanya haya mambo bali wanakwamisha na jitihadi za makusudi za rais pamoja na makuwadi wake. Tanesco waliweza kwa muda mrefu kupanga mikakati ambayo ndiyo ingeweza kulikwamua hili taifa katika maafa tuliyonayo.

  Jitihada za JK ni kuona njia kuu za uchumi zinamilikiwa na makampuni yake hewa ambayo yanafanya kila jitihada kuwahadaa wanachi, angalia TTCL, TRL, makampuni ya madini nk.

  Imefika wakati Watanzania kuamua kusuka ama kunyoa, kuchagua kuburuzwa na wajinga ambao wanafikiria hii ni nchi yao pekee au kubadilisha tena kwa haraka sana mfumo mzima wa utawala. Kama unalalamika unaona maisha ni magumu fikiria kodi yako jinsi inavyochezewa na Spika wa Bunge ambaye amewekwa pale kutetea maslahi ya EL, RA, Chenge na JK.
   
Loading...