Kuigawanya Serikali ya CCM katika awamu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuigawanya Serikali ya CCM katika awamu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Semenya, Jan 4, 2010.

 1. Semenya

  Semenya JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2010
  Joined: Sep 5, 2009
  Messages: 572
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 35
  Kumekua na tabia ya watu wengi,kuzitofautisha awamu za serikali ya CCM katika awamu ya 1,2,3na ya 4.

  hii ilichagizwa sana na mkuu wa sasa [JK], pale alipoiita awamu ya 4 ni ya nguvu mpya kasi mpya na ari mpya, kwangu mimi akiwa na nia yakujitenganisha na kujiweka katika pahala tofauti na viongozi wenzake.

  Jambo hili me naliona ni mwanzo wa mpasuko mkubwa ndani ya CCM na pia hata baadhi ya wananchi, pale wanapojaribu kuzilinganisha serikali hizo 4 tofauti.

  lakuzingatia hapa hakuna cha awamu yote ni seriklali ya CCM, iwe kama nchi zinazopigiwa upatu kuendelea kidemokrasia kuwa wao hawatofautishi awamu bali wanatofautisha chama.

  uwozo alioufanya Nyerere, Mwinyi na Mkapa yoote ni ya CCM, na si kujifanya kujitenganisha na kujiita awamu ya 4, kama tulivyowahi kusikia mmoja wa viongozi wa CCM akisema 'matatizo ya umeme wamerithi awamu ya 3'. huu ni udanganyifu na kutaka kuonakana bora kuliko mwingine wakati wote kundi lenu ni lilelile.

  Ni vyema kusema serikali ya CCM kuliko kuigawanya katika awamu eti tu kuna watu wanataka kukimbia lawama na kujifanya wao bora zaidi.
   
 2. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2010
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Now You're talking.
   
 3. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160

  Semenya, yeye Mwenyewe JK ndiyo kwa kwanza kuzigawa awamu hizi wakati anahutubia bunge la Jamhuri baada tu ya kutawazwa urais. sasa mi ndo nikaamuuliza kama umegawa awamu 4, hii yako we umefanya nini kwa miaka hii 4 uliyokaa pale Nyumba nyeupe? "Maisha bora kwa kila mtanzania?

  Nilikuwa na maana kwamba kwa ujumla wake Serikali ya CCM imeshidwa kabisa kuwatumikia wananchi wake hakuna cha awamu ambayo itajisifu imefanya vizuri kwa ujumla. haya leo hii tunaambiwa kina mama wanakufa kwa kukosa huduma kwenye wodi za kujifungulia lakini at the same time BOT taasisi ya Umma inakarabati nyumba mbili kwa 3b.... tumelaaniwa au?

  kwa mtindo huu hatuendelei kamwe tutatawaliwa milele - (Ukoloni mamboleo).
   
 4. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #4
  Jan 4, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  LAKINI MKUU!
  mbona ben nae alikuwa na slogan yake ya UKWELI NA UWAZI........
   
 5. K

  Kwaminchi Senior Member

  #5
  Jan 4, 2010
  Joined: Dec 30, 2007
  Messages: 154
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Katika vitu vibovu ambavyo tumerithi kutoka TANU/CCM ni ujinga na uwoga. Ujinga wenyewe si wa kusoma shule ni ule wa kutotambua haki zetu na tunapozitambua hatujui jinsi ya kuzipata na tunapozipata hatujui kuzidumisha wala kuzistawisha. Uwoga ni ule wa kutokuwa na ujasiri wa kuthubutu.

  Ndani ya CCM kuna kikundi cha watu wachache wajanja, wanakula nchi kwa kujipangia awamu za kushika madaraka na kuitafuna nchi. Sisi awamu hii na sisi awamu ile. Ukisikia CCM ina wenyewe na wenyewe ndio sisi, basi ujue hao sisi ni hao wajanja wachache. Wengine wote wanaojiita CCM hao ni ngazi tu ya wajanja wachache kupandia nyadhifa zao, hawajijui masikini. Wao ni CCM wa kukimbiza mwenge na kupewa pipi pindi uchaguzi unapowadia. Kazi yao kubwa ni ile ya kufagilia.

  Vyama vingi na katiba ya chama kimoja yenye viraka ni kiini macho, kama ilivyo ngonjera ya awamu nyingi za serikali ile ile ya CCM. Hakuna serikali tofauti nchini mwetu, tangu ile ya 1961. Siku zote na miaka yote tumetawaliwa na TANU/CCM baada ya kuondoka tawala za wakoloni. Kama kuna wasiosadiki, nawaomba wachukue nyama iliyooza waitie katika friji mpya kila baada ya miaka mitano, waone kama nyama hiyo itaacha kuoza.

  Hakuna cha awamu ya Nyerere, Mkapa, Mwinyi wala ya Kikwete, awamu zote ni za TANU/CCM. Tukiendeleza ujinga na uwoga serikali itabaki hiyo hiyo ya wajanja wachache milele na kazi yetu itabaki vile vile, ya kupiga mayowe. Kudhani kuwa serikali ya awamu ya tano itakuwa tofauti ni dhana ya fisi, kungojea mkono wa mtu anayetembea utadondoka.

  Sijui ujinga huu utatuondoka lini na ule ujasiri wa kuthubutu kuiondoa TANU/CCM madarakani utatufikia mwaka gani, labda mwaka huu wa 2010.
   
 6. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #6
  Jan 4, 2010
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35

  Ni kweli kabisa Mkuu. Sasa saidia wasiojua. Je, wabadili fridge kwa kuweka nyama wapi?
   
Loading...