Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,437
- 113,445
Wanabodi,
Salaam.
Kuanzia leo, hadi tarehe 24 October, kwa siku hizi 30+ zilizobakia kabla ya kufanyika uchaguzi, nitajitolea kutoa makala za uhamasishaji ili wana jf tujitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura. Makala hizi zitakuwa ni makala elimishi, ili kuwasaidia Watanzania wenzetu ambao bado wamelala, waamke ili wakachague kwa kufanye informed decision, yaani wachague kwa sababu ya kuchagua, na sio kuchagua kwa mazoea tuu!, kuchagua kwa mazoea tuu mimi nimekuita ni ignorance!.
Declaration of Interest
Naomba ku declare interest kuwa japo mimi ni mwandishi wa habari, maadili ya uandishi wa habari, yanatuelekeza sisi waandishi wa habari, tusishiriki kwenye partisan politics, hivyo mimi pia nina chama changu moyoni mwangu, na nina upande ninao support lakini bado naweza kuwa objective, na impartial bila kuegemea chama changu au upande wangu.
Is CCM Fooling Us Around?
Kuna msemo usemao "You can fool some people for some time, but you can't fool all the people all the times!".
Ikitokea kuna watu ambao wote wanakuwa fooled all the times, then watu hawa watakuwa ni a bunch of fools and ignorants!. Jee sisi Watanzania wote ni a bunch of fools and ignorants?.
CCM has been fooling us all for all the times kwa ahadi na ahadi zisizotekelezeka, na siku zote bado tunaichagua tena na tena. Miaka mitano ikifika, huja na visingizio hivi na vile vya kwanini ahadi hizo hazikutekelezwa, na kila baada ya miaka 5, huja na ahadi mpya kibao, zenye matumaini mengine mapya. Kipindi cha uchaguzi kinafika bila ahadi za zamani kutimizwa, hatuambiwi sababu kwa nini hazikutimizwa, bali tunaletewa ahadi mpya, na tunaichagua CCM tena na tena!. Jee kujiuliza kama sisi Watanzania ni ignorants au tumelogwa ni kutukana?!.
Hii ni mada ni kufuatia mada yangu ya Jee Watanzania ni ignorants au tumelogwa? bandiko hili lilimgusa dada yangu Juliana Shonza , sijui kwa nini alishindwa kuchangia bandiko lile, ila na yeye akanzisha bandiko lake,Watanzania sio wajinga; tumekusikia, tumetafakari kujibu bandiko langu na hii ni sehemu tuu ya majibu yake
Naomba nianze kwa kukuonya, kuna tofauti kubwa kati ya ignorance na utaahira, mimi nimesema Watanzania tunaichagua CCM kwa ignorance, naomba uliombee msamaha hili la kuwatukana watu ni mataahira kabla 'karma' ya utaahira haijakushukia, haswa kwa kuzingatia wewe bado ni binti mdogo, mbichi ndio kwanza unajiandaa kuingia kwenye ujenzi wa familia!. Omba tuu hata kimoyo moyo Mungu akuepushie mbali tukano hilo la kutukana watu mataahira!.
Naomba niweke in points format, ili iwe rahisi kuchangia kwa kujibu hoja au kupangua hoja kwa hoja na sio hoja kwa viroja!.
Namalizia kwa kukumbushia lile swali la msingi, baada ya kusoma haya, kweli bado kuna watu wataichagua CCM?, na iwapo wataichagua tena CCM, kuichagua huku CCM, jee ni kielelezo cha kufanyika kwa informed decision au ni uthibitisho wa muendelezo wa ignorance ya Watanzania kuendelea kujichagulia tuu kwa mazoea?!.
Tafakari kwa makini, fikia maamuzi ya busara, hakikisha Tarehe 25 October, unajitokeza kifua mbele, kwenda kuitumia haki yako ya kidemokrasia kuamua hatima ya nchi hii kwa kupiga kura.
Nawatakia Jumatatu Njema.
Paskali

Nimesoma andiko la PASCO wa JF kuhusu kile anachodai ni UJINGA wa watanzania, kwa kuendelea kuichagua CCM ambayo kwa mawazo ya PASCO ni chama kibaya.
Naomba kumthibitishia kuwa MIMI na watanzania sio wajinga, tunatambua jema na ovu, tunatambua nani ni mbaya na nani ni mwema..yawezekana yeye ameshindwa kutambua, hivyo nitazungumzia juu yangu na Watanzania wenzangu ambao kwa Miaka zaidi ya 50 sasa tumeendelea kuiamini CCM.
CCM imeendelea kuwa CHAMA kinachojitathimini na kinachojiimarisha siku hadi siku, sipingi wala sisemi kuwa CCM haijawahi kukosea, haina makosa na haijaaribu katika utawala wake..hapana na nikisema hivyo nitakuwa mnafiki, lakini tunaiona CCM ikijivua gamba katika new style, ikikataa kuwakumbatia mafisadi na kwa mara ya nyingine tena ikipata mgombea BILA RUSHWA, BILA HILA na BILA MTANDAO...hivyo kama PASCO unaamini kuwa CCM ni ile ile, yenye watu wale wale na sera zile zile basi PASCO wewe sio PASCO yule ninayemjua ambae huwa anaandika baada ya kufikiria, it seems contrary to my experience., perhaps U have personally and intentionally decides to do wrong and u seemed to know full well of ur decision.
Ama kuhusu msisitizo wako kuwa tukijilinganisha na nchi zingine ambazo zilipata uhuru katika miaka hiyo takriban 50 iliyopita kuwa wengi wamepiga hatua katika maendeleo, lazima ufanye comparison ya workload yetu na wao katika miaka hiyo 50...tumefanya nini interm of African Liberation which is the true factor kwa ku-slow down kwetu katika kupata Maendeleo ya haraka..
Kama unadhani ELIMU yako iliyokupa kiburi cha kuona Watanzania wote ni mataahira ndio msingi wa Maendeleo ambayo Mwalimu and the rest walifikiria then U are wrong..U are as IGNORANT better than any of Us..Arrogance is ignorance with an attitude..
Naomba nianze kwa kukuonya, kuna tofauti kubwa kati ya ignorance na utaahira, mimi nimesema Watanzania tunaichagua CCM kwa ignorance, naomba uliombee msamaha hili la kuwatukana watu ni mataahira kabla 'karma' ya utaahira haijakushukia, haswa kwa kuzingatia wewe bado ni binti mdogo, mbichi ndio kwanza unajiandaa kuingia kwenye ujenzi wa familia!. Omba tuu hata kimoyo moyo Mungu akuepushie mbali tukano hilo la kutukana watu mataahira!.
Naomba niweke in points format, ili iwe rahisi kuchangia kwa kujibu hoja au kupangua hoja kwa hoja na sio hoja kwa viroja!.
- Tulipopata uhuru ile miaka ya 60, tulikuwa na maadui wakubwa watatu, ujinga, umasikini na maradhi!, tulikuwa na all the resources to make this country move forward, watu, ardhi, siasa safi, na uongozi bora, tena ilisemwa, fedha sii msingi bali ni matokeo!, tulikuwa na udongo wenye rutuba, vyanzo lukuki vya maji, mali asili, utalii, utajiri mkubwa wa madini, etc, etc, in short we had everything, na wenzetu tuliopata nao uhuru, had nothing compared!, leo wenzetu have everything and sisi not only we have nothing!, bali umasikini umeongezeka mara dufu!, tulikua tuna object poverty sasa tuna stinking poverty!, ni umasikini uliotopea, kila siku ni afadhli ya jana!. Ujinga umeongezaka maradufu!, wakati wa Nyerere, there was a time litaracy level yetu ilikua juu, hadi wazee walifundishwa elimu ya watu wazima na elimu ya kujua kusoma na kuandika katika elimu ya ngumbaru!, leo mwanafunzi anamaliza darasa la saba hajui kusoma wala kuandika!. Maradhi ndio usiseme!, lakini leo sio tuu bado tuna wale maadui watatu, bali sasa tumeaongeza na maadui wengine wawili zaidi ambao hawa ni CCM's own making!, rushwa na ufisadi!.
- Nakubalina na wewe Baba wa Taifa hili, Mwalimu Nyerere amelifanyia makubwa taifa hili, na pia ni kweli mchango wa Tanzania katika ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika na Vita vya Kagera, vimechangia kururudisha nyuma maendeleo yetu, but to what extence?!.
- Mwalimu Nyerere alifika mahali, akakubali makosa, akakiri kufanya kosa sii kosa, kosa ni kurudia kosa, hivyo kwangu tatizo sio Mwalimu bali hawa waliomfuatia sio tuu kwa kurudia makosa bali kuongeza na makosa mengine mapya ya kijinga kabisa!, ujinga huu ndio ignorance ninayoizungumza mimi, mjinga, akikupa sababu za kijinga na wewe ukaendelea kumchagua, wewe unaemchagua ndio mjinga kabisa!. Hivyo nimeuliza Jee sisi Watanzania wote ni wajinga ki hivyo?. Are we all that ignorants?!.
- Mimi sio miongoni mwa lile kundi wanaosema CCM, haijafanya kitu, kuna mengi tuu mazuri CCM imefanya, na nimeyasema humu,Miongoni Mwa Mazuri ya CCM, but it is not enough!, uzuri wangu, mazuri ya CCM nimeyakubali na kuyataja humu, ila pia mabaya ya CCM na madudu ya CCM nimeyataja!,Mapungufu ya CCM: A Constructive Criticisim!, madudu ni mengi zaidi kuliko mazuri, hivyo nimeuliza,does CCM deserve kupewa another chance?, au kupumzishwa ni halali?! ila tukiamua kuipumzisha, nikashauri na tuipumzishe kwa upendo na amani.
- CCM imefanya mismanagement kubwa ya resources za nchi hii for too long!, sasa nchi yetu imefikia stage tunona pride raisi wetu kupanda ndege kusafiri kwenda ulaya kutembeza bakuli!, wakati tuna utajiri mkubwa wa maliasili na rasimali za kutosha kutufanya kuweza kujitegemea!, kitendo cha Tanzania kuwa bado ni taifa omba omba!, its just unacceptable and it is a shame!.
- Rushwa ya petty corruption is an order of the day!, kiasi kwamba baadhi yetu ukikamatwa na kosa la traffic, kuliko kusubiria hiyo notification ya bila risiti, bora mmalizane hapo hapo na kusave time!. Hata kujiandikisha tuu kwenye daftari ya kudumu la wapiga kura, I had to do something!, nakiri sikuombwa chochote na yoyote, bali nilipofanya time management ya kuamka saa 10 alfajiri ili kuwahi foleni, na kushinda siku nzima kituoni, nika opt kuitumia ile dawa ya 'penye uzia!'. Mwanzo rushwa ilikua siri, sasa ni mambo hadharani, wazi wazi!, Trafick hawaendi tena kupokelea pembeni au uchochoroni kwa kujificha, bali wameihalalisha wazi wazi kwa kutembea na vitabu fake vya notification, unaandikiwa na kuambiwa risiti uipitie baadae!.
- The grand corruption ndio usiseme, sisi tulio sekta binafsi tunajua, ili ushinde tender unapaswa kufanya nini!. Manunuzi ya umma ni kwa kickback za kueleweka!, ile ya Rada imerudishwa kwa uadilifu tuu wa Waingereza tena kwa taarifa yako tuu, kama hujui, ule mgao wa Change ulikua ni vijisenti tuu, laiti Watanzania wangesikia wale wazee 'wanene' wa kule top walivuta ngapi, hata kusubiria tuu hadi mwaka wa uchaguzi ufike ndipo wafanye mabadiliko, watu wangeona mbali!, wangemarch streets moja kwa moja hadi kwenye ile nyumba pale, kwenda kuwafurusha na kuwatoa baru!. CCM waishukuru sana BAE kwa kuyahifadhi majina ya waliolipwa hizo kickbacks na badala yake kukubali kulipa faini ya non-disclosure ndio hicho kinachoitwa change ya Rada!.
- Ufisadi ni kila kona, mfano mdogo ni ununuzi wa ndege ya rais bei yake imeonekana wazi ni bilioni 18 tuu!, ajenti analeta bili ya bilioni 43 serikali inaonyeshwa hadi bei halisi ya kiwandani, lakini bado inaendelea tuu kulipa!, only the fools and the ignorants ndio wataamini there was no kickbacks hadi kule the highest office!. Ajenti wa ndege hiyo ndio huyo huyo ajenti wa rada, ndio huyo huyo ajenti wa zile helcopter mbovu, ndie ajenti wa magari ya jeshi mtumba na vifa vya kivita viwivyofanya kazi!, na siku za sherehe za Ikulu, ukiondoa magari ya viongozi wakuu wa kitaifa ambao magari yao ndio huruhusiwa kupaki ndani ya Ikulu, gari la ajenti huyu, Red Ferrarri, ndilo hupaki ndani ya Ikulu tena pale garden ili kila mtu alione na kumtambua yuko karibu na familia ya rais, hata magari ya mawaziri na mabalozi hupaki nje!, ni ignorant tuu pakee ndiye atakayeamini 'jamaa' hahusiki.
- Serikali ya CCM, haina vipaumbele muhimu bali inendeshwa kwa matukio!, tangu tumepata uhuru ujinga ulikua ni adui namba moja, tumefanya nini kuinua elimu yetu!, CCM imewekeza on ignorance na inaitumia hiyo ignorance kama mtaji wake wa ushindi, na ukiangalia maeneo yenye low literacy level, hizo ndizo ngome za CCM!, mkoa wenye the highest literacy level ni ya Kanda ya Kaskazini, angalia hali ya CCM!, kwa watu waelewa hawadanganyiki tena!, na ikitokea CCM ikashinda hata jimbo moja, then labda Upareni kwenye umasikini na Simanjiro kwenye ujinga!.
- Mzigo mkubwa unaotuongezea umasikini huu ni gharama kubwa za uendeshaji wa serikali, nchi yetu ni ndogo tuu tena masikini wa kutupwa, lakini yenye serikali kubwa for nothing!, kinchi kidogo tuu kama Tanzania kuwa na mawaziri 54!, huku linchi likubwa na tajiri kama Marekani wana mawaziri 6 tuu!, huu kama sio ujinga ni nini?!. Tukiwa na mfumo mzuri hata ma DC ni redundant, just a wastege of resources!, Tuna baadhi ya idara zinazojitegemea, hazina kichwa wala miguu mfano baada ya kuwa na Vizazi na Vifo halafu tunaanzisha NIDA kufanya kitu kile kile ambacho kingefanywa vizuri zaidi na Vizazi na Vifo!.
- Madini tumetoa bure!, na gesi pia tunatoa bure!. Gesi asili: Is it "day light robbery?!"- watanzania tunaibiwa Mchana Kweupe! .
- Handling ya issue ya Escrow, ni kielelezo cha ignorance ya hali ya juu!.Escrow: Jee Watanzania ni Ignorants? au Tumelogwa?!.
- Hakuna ubishi kuwa siku zote, CCM imekuwa ikishinda chaguzi mbalimbali ka mbinu tuu na mtaji wao mkubwa wa ushindi ni kuitumia ignorance ya "watu" ambao CCM imewekeza!.
- Hakuna ubishi kuwa CCM kama chama, kimechoka, dalili zote za chama kichovu kinachosubiri kifo, tayari, zimeisha jitokeza kwa CCM, kinachosubiriwa sasa its only a matter of time ni lini kitaangwa rasmi, hiyo October 25 is the day of the judgement!, yaani it is Judgment Day!. CCM Imechokwa, Mtazamo: CCM imechokwa mpaka basi!
- Hakuna ubishi kuwa wengi wa hao "watu", wamekuwa wakiichagua CCM sio kwa sababu wanaipenda sana!, (waipende kwa lipi?), la hasha!, "watu" wamekuwa wakiichagua CCM kwa mazoea tuu! kufuatia ignorance yao!.
- Hakuna ubishi, kuwa wengi wa hao "watu" waliokuwa wakiichagua CCM kwa ignorance ya mazoea tuu, sasa wameamka kutoka katika usingizi wameichoka, hivyo October 25, hawatachagua tena chama kwa mazoea, bali watachagua chama kwa "sababu"!.
- Tatizo kubwa la Watanzania au adui mkubwa wa Tanzania sio CCM, CCM is just a vehicle, haikujiweka hapo ilipo, imewekwa, kwa ignorance yetu, hivyo tatizo sio CCM iliyowekwa, bali tatizo ni sisi, wale walioiweka CCM hapo ilipo!. That simply means, tatizo ni sisi Watanzania tulioiweka CCM madarakani kwa ignorance yetu, and it plays games on us again and again na sisi tukiendelea kuiweka madarakani again and again and again na sitashangaa kama hata October 25, hawa ignorants ambao hawajabadilika kama ni wengi kuliko walioamka, then sitashangaa wakiirudisha tena CCM ikulu ya Magogoni!, huku kutakua ni uthibitisho wa ignorance!.
- Chaguzi nyingine zote, CCM imekuwa ikichaguliwa kwa walkover victory kwa ignorance tuu kwa sababu we had no choice to choose from, uchaguzi wa mwaka huu, tuna altenative, we have a choice kati ya kuichagua CCM au kuipiga chini!, watu tutaingia kwenye uchaguzi with choice na sio walk over kama mazoea, hivyo CCM ikichaguliwa tena, then hiyo ndio itakua choice yetu tumechagua tena kwa sababu na sio kwa mazoea ya ujinga (ignorance)!.