Kuibuka kwa Tundu Lissu ndani ya dhana ya kujaza ombwe

ufupi ni kwamba yule Binadam ni wa kiwango kingine kaaeni nae mbali,

kazi yenu ni kumsema nyuma ya kibodi tu wakati hata kulegeza kamba za viatu vyake labda mfe mzaliwe upya
Yule ni binadamu wa kiwango kingine kwa watu wa aina yako wewe. Wenye kujielewa wanausikitikia mwelekeo wa CDM.

Ukishindwa kuelewa kwamba sentensi moja inaweza kuipatanisha nchi au kuigombanisha, basi hufai hata kuongea mbele za watu, tena ukiwa mwanasiasa wa chama chenye kusudio la kuongoza nchi.
 
Hoja tatu tu, UKABILA,UKANDA NA UDINI.. Umetumia Elimu yako yote uliyosoma kujibu wakati majibu ni rahisi sana.
 
Mkuu msemajiukweli nimeona mjadala waki wa post namba moja. Nimekubaliana sana na falsafa yako hapo juu, lakini maelezo yako yote yamejikita kwenye dhana pana sana inayoeleweka na wasomi ambao ni wachache na sio wapiga kura kwa uzoefu uliopo. Wananchi walio wengi wanaangalia yule anayeongea anaongea nini, je kinaeagusa hisia zao au la. Nitakupa mfano mzuri, ukija na wimbo wenye bit nzuri hata kama hauna ujumbe mzuri watu wataucheza tu, lakini ukija na wimbo wenye ujumbe maridhiwa bit mbovu utaucheza mwenyewe.

Tuje upande wa Tindu Lissu, ni kweli ana siasa za kiunaharakati hilo halina ubishi ila kuna wakati anaongea ukweli unaogusa watu kama vile leo. Na utakuwa unajidanganya kwamba watanzania walio wengi wanajua tofauti ya siasa na mwanaharakati. Kwa ulinganifu wa kauli hata mkulu hana tofauti sana na kauli za Lisu, kwani hata yeye sio mwanasiasa bali ni mwansharakati ila hiyo haionekani sana kwabi yuko chama kilicho madarakani. Ukichunguza mengi ya mambo yake anayateleza kwa mitazamo na hisia zake ba wala sio kufuata ilani, sheria au katiba. Kibaya zaidi huko chamani hakuna mwenye nguvu ya kumdhibiti. Mfano mrahisi ni hyo ya mwanafunzi mzazi kurudi shule, kwenye ilani iko wazi lakini hajafuata.

Watanzania wengi hatujali ni mwanasiasa au mwanaharakati bali tunajali mtu anaongea nini. Hicho alichokisema Lissu leo kwa sehemu kubwa ni ukweli ulio wazi, na msipotumia busara mkamuachia mkulu amjibu Lissu ndio utajua hata yeye ni mwanaharakati tu. Huu ndio ukweli hayo mengine yote kwenye post yako ni hadithi kama hadithi nyingine.
Sasa wewe mkuu, hivi alichoongea Lisu anaweza kwenda nacho kwa mpiga kura akamwelewa? Kwamba Magu ni mkabila? Hii hoja inamsaidia vipi mtu wa Mbeya kule?

Hii hoja ya Lisu inatofauti gani na ile ya ccm kwamba chadema ni chama cha wachga na ukaskazini? Matokeo yake ccm ikazidi kupotea huko kaskazini.

......
 
Ndg mtoa mada pamoja na kuongea mengi sana lkn umeshindwa kujua kuwa Tundu Lissu anaziba ombwe LA Taifa
Hayo yote aliongea Lissu ni ukweli mtupu na yalipaswa yaongelewe na
_ viongozi wetu wa dini
_ viongozi wasitafu kama Waryoba, Salim Mohammed Salim, Butiku, na wengineyo.
_ wanaharakati na Taasisi mbali mbali za serikali na zisizo za serikali.
Lkn hao wote kimya hivyo kuzusha ombwe ambalo sasa linajazwa na mh. Lissu
Na Lissu anaongea ukweli mtupu
 
Lissu ukimlinganisha na slaa wako..Lissu is far ahead...a million times...slaa wako anayetekwa na unanihii wa mwanamke na hadi kuingizwa katika kupokea rushwa kutoka kwa watesi wake...ameonesha kuwa mtu wa hovyo kulikoni

Lissu sio mtu mwoga....anausema ukweli jinsi ulivyo....hapa ndipo ninyi waoga mnapomwona hana hekima....Lissu sio mnafiki...

cha ajabu lissu huwa hamuwezi kupinga hoja zake..huwa mnakimbilia ku attack personality yake

Ni mjinga tu anayetegemea CHADEMA ifanye jambo wakati wanazuiwa kwa namna zote kufanya siasa....ni upuuzi mtu kuanza kujisifu eti CCM inanawiri...ilihali wanavinyanyasa CHADEMA na CUF na kuvizuia hata kufanya mikutano yao ya ndani.
Wamezuiwa kwa sheria ipi? Wamewahi kufungua shauri mahakamani juu ya hili kama kuna tamko lililo kinyume cha sheria ili mahakama itoe tafsiri?
 
Sasa wewe mkuu, hivi alichoongea Lisu anaweza kwenda nacho kwa mpiga kura akamwelewa? Kwamba Magu ni mkabila? Hii hoja inamsaidia vipi mtu wa Mbeya kule?

Hii hoja ya Lisu inatofauti gani na ile ya ccm kwamba chadema ni chama cha wachga na ukaskazini? Matokeo yake ccm ikazidi kupotea huko kaskazini.

......

Mkuu nadhani hujui aina ya wapiga kura tulionao. Hawaangalii mambo makubwa wao uwezo wao wa kuelewa mambo ni mdogo. Hivyo huo mtazamo wa kutoa kura kwa kabila, dini nk ni kawaida sana. Au unataka mifano? Halafu huyo Lisu wapiga kura wamuelewe wasimuelewe hatujali ili mradi alichozungumza ni kweli kwetu ni sawa. Watakapotokea wapiga kura waelewa wataona hoja ilipo. Kwa mfano huyo Lissu alianza kupigia kelele mikataba ya madini bado wapiga kura hawakumuelewa, lakini ukweli si huu umedhihiri?

Lisu aendelee kuongea ukweli hata kama cdm itakosa kura au kufa haipunguzi ukweli.
 
Wamezuiwa kwa sheria ipi? Wamewahi kufungua shauri mahakamani juu ya hili kama kuna tamko lililo kinyume cha sheria ili mahakama itoe tafsiri?
unajua wewe siku hizi umekuwa na akili mgeuko kama babu yako slaa

CHADEMA imefungfua kesi nyingi sana kuhusu hili...na unajua

upload_2017-7-18_12-35-13.png


Chadema yafungua kesi ya madai mahakama ya mwanza kupinga amri ya polisi kuzuia mikutano ya hadhara
 
Ndg mtoa mada pamoja na kuongea mengi sana lkn umeshindwa kujua kuwa Tundu Lissu anaziba ombwe LA Taifa
Hayo yote aliongea Lissu ni ukweli mtupu na yalipaswa yaongelewe na
_ viongozi wetu wa dini
_ viongozi wasitafu kama Waryoba, Salim Mohammed Salim, Butiku, na wengineyo.
_ wanaharakati na Taasisi mbali mbali za serikali na zisizo za serikali.
Lkn hao wote kimya hivyo kuzusha ombwe ambalo sasa linajazwa na mh. Lissu
Na Lissu anaongea ukweli mtupu

Lissu ni mkweli hata Mungu analijua hilo

Anausema UKWELI ULIVYO
 
Mkuu nadhani hujui aina ya wapiga kura tulionao. Hawaangalii mambo makubwa wao uwezo wao wa kuelewa mambo ni mdogo. Hivyo huo mtazamo wa kutoa kura kwa kabila, dini nk ni kawaida sana. Au unataka mifano? Halafu huyo Lisu wapiga kura wamuelewe wasimuelewe hatujali ili mradi alichozungumza ni kweli kwetu ni sawa. Watakapotokea wapiga kura waelewa wataona hoja ilipo. Kwa mfano huyo Lissu alianza kupigia kelele mikataba ya madini bado wapiga kura hawakumuelewa, lakini ukweli si huu umedhihiri?

Lisu aendelee kuongea ukweli hata kama cdm itakosa kura au kufa haipunguzi ukweli.
Sijaona huo ukweli wa Lisu, na huenda Lisu yeye ndio mkabila!

Ukiona rais anateua mtu alafu mijitu inaanza kuchunguza huyo mteuliwa katokea kanda gani ujue yenyewe ndio imejaa ukabila.

......
 
Wenye akili tulishajua kitambo sana kwamba kuondoka kwa Dr.Slaa itatugharimu sana.nakumbuka ile siku mzee anajiuzuru kuna watu nilibishana nao sana hadi wakaniambia mimi nimeshakuwa mamruki.
 
Sir, i like your clinically executed responses to this group's nonsense. It is true that their understanding is below par, sometimes rushing to comment even without reading the entire article. SHAME.
 
Wenye akili tulishajua kitambo sana kwamba kuondoka kwa Dr.Slaa itatugharimu sana.nakumbuka ile siku mzee anajiuzuru kuna watu nilibishana nao sana hadi wakaniambia mimi nimeshakuwa mamruki.
ACHENI AENDE, CHAMA KITASONGA MBELE TU_BINAFSI NAAMINI KUNA MILIMA NA MABONDE YA KUSHUKA LAKINI HAITUZUII KWENDA MBELE
 
CCM tunashukuru Tundu Lisu anatusemea ingawa ni wa upande wa pili ukweli ndio huo wengi Jamaa ameharibu system za Maisha yetu hakuna biashara zinazoendelea, watumishi hali mbaya, labda wasukuma wana Maisha mazuri, lakini wengi mambo ovyo sana mtaani, watu hasa wa chini wamechoka zaidi
Mkuu hata wasukuma tunalia hali ni ngumu, anaowabeba ndiyo hao watoto wa dada zake lakini wale wasukuma makabwela hali yetu ni ngumu.
 
Huwezi linganisha ccm na chadema.
Tunajua ccm kuwa hamwezi kujenga hoja zaidi mnaegemeaga kwenye majungu kama haya uliyoandika.
Chadema iko imara sana,tofauti na maigizo ya magu.ombwe la uongozi unalosema ni lile ombwe la viongizi wasioongeka,wala kununuliwa na awa ndio viongozi wanaostahili kwenye chama kama chadema.mmetafuta kuwanunua mmeshindwa sasa ni kujenga majungu,ooooh ombwe,ombwe.nenda kaombwe na wewe.

Sent from my itel it1505 using JamiiForums mobile app
 
Kwa wasiofahamu vizuri, ombwe ni utupu wa kutokuwa na kitu kwa kipindi fulani, yawezekana ikawa ni mawazo, vitu au hali fulani.

Mwanafilosofia kutoka Ugiriki aliyeitwa Aristotle aliwahi kusema, “horror vacui (nature abhors vacuum)”, hii ina maana kuwa haiba ya kidunia haikubali ombwe litokee bila kujazwa.

Kuibuka kwa Tundu Lissu ndani ya CHADEMA kama ndiye ‘’nembo’’ ya CHADEMA katika kipindi hiki cha utawala wa awamu ya tano sio kama kimekuja kwa bahati mbaya au nzuri bali ni kwa sababu mazingira ya CHADEMA kwa sasa yana ombwe la viongozi wakuu na mwelekeo wa chama kifalsafa.

Ieleweke kuwa vyama vya siasa ni watu na watu ndio hutoa viongozi lakini kama watu wameshindwa kutoa viongozi makini na weledi wenye kujaza ombwe la uongozi bora basi nature (asili) itatumia nafasi hiyo kutoa kiongozi wa wakati huo hata kama hafai katika mazingira endelevu.

Kuibuka kwa Tundu Lissu kama kinara katika siasa za CHADEMA kunatoa angalizo kwa viongozi wakuu wa CHADEMA kuwa hawatoshi kwa mazingira ya siasa za sasa.

Yanayotokea ndani ya CHADEMA kwa sasa yananikumbusha yaliyotokea wakati wa utawala wa Mzee Mwinyi wakati CCM na serikali yake inahangaika na mivutano ya kiitikadi na kifalsafa kuhusu mwelekeo wake.

Kundi kubwa ndani ya CCM lilikuwa bado linaishi katika ndoto na maisha ya dhana ya uchumi ulio chini ya msingi wa Ujamaa na Kujitegemea wakati kundi dogo la viongozi wakuu walikuwa wameamua kuingia katika dhana ya uchumi wa soko huria bila kuwa na misingi ya katiba na sheria iliyo imara katika kupambana na ‘’ombwe’’ la mpito wa kisiasa na kiuchumi.

Mivutano hii ilileta misukosuko ya Kiuongozi na kutikisika kwa Muungano iliyomfanya Mwl. Nyerere mwaka 1993 kuandika kitabu kinachoitwa Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania. Katika kitabu hicho Mw. Nyerere alisema, hulka huchukia ombwe akitumia maneno ya Aristotle , ‘’Nature abhors a vacuum’’, Mwl. Nyerere aliezea zaidi na kusema, ‘’hata siasa huchukia ombwe. Kama uongozi ni mbovu, upo kama haupo, au upo kwa maslahi ya wenyewe, watatokea watu waujaze uwazi uliopo; hauwezi kuachwa wazi hivi hivi. Lakini uongozi mbovu ni kama mzoga, una tabia ya kukaribisha mafisi na mainzi’’.

Mivutano ya CCM wakati wa utawala wa Rais Mwinyi haina tofauti na kinachoendelea kwa sasa ndani ya CHADEMA. CHADEMA ya sasa haijui vizuri mwelekeo wake kifalsafa kutokana na mivutano ya kiungozi iliyoanza baada ya Lowassa na genge lake kutua CHADEMA.

Uongozi wa CHADEMA kwa sasa ni mbovu, upo kama haupo na upo kwa maslahi ya watu wachache. Kutokana na ‘’Ombwe’’ hili ndio maana kwa sasa limeanza kujazwa na Tundu Lissu. Tundu Lissu sio kwamba ni kiongozi mwenye ueledi na shupavu bali ‘’ombwe’’ linamuona ni afadhari ya uongozi uliopo!

Unapomuona Mwenyekiti Mbowe na Katibu wa CHADEMA Taifa, Mashinji ambao ndio viongozi wakuu wa chama wanakuwa wafungua mlango wa gari la Lowassa ili Lowassa ashuke au apande lazima utajiuliza maswali mengi kuhusu nafasi ya viongozi wakuu katika chama na hatima ya chama.

Tundu Lissu hakuweza kuibuka wakati wa uongozi wa Dkt. Slaa kwa sababu ‘’Ombwe’’ la uongozi lilijazwa vizuri na Dkt. Slaa. Masuala yote yanayohusu dira/mwenendo wa CHADEMA na hoja kuhusu mwenendo wa serikali zilijibiwa na Dkt. Slaa kwa weledi na hekima ya juu kama Mtendaji Mkuu wa CHADEMA. Hata pale Tundu Lissu alipojaribu kuleta siasa za uanaharakati alipigwa stop na wazee ndani ya CHADEMA.

Nakumbuka wakati wa mchakato wa Katiba Mpya aliibuka na kusema ''Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu''. Hapo hapo Mzee Edwin Mtei akaibuka na kumpiga stop akimwambia, ‘’ With all due respect to Hon. Tindu Lissu, this smacks BAD TASTE’’

Alichokisema Tundu Lissu kuhusu Mwl. Nyerere unaweza kusoma hapa;
GONGA LINK>>Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu

Alichokisema Mzee Edwin Mtei kuhusu Tundu Lissu unaweza kusoma hapa;
GONGA LINK>>Mzee Edwin Mtei asikitishwa na alaani kitendo cha Tundu Lissu kumtukana Baba wa Taifa, Mwl. Nyerere

Maoni na mwelekeo wa Tundu Lissu kwa sasa umekuwa ndio dira/mtazamo wa CHADEMA kama chama/taasisi. Suala lolote linalohusu dira/mtazamo wa CHADEMA anayeulizwa na kutoa maoni ni Tundu Lissu badala ya Mwenyekiti au Katibu Mkuu ambaye Katiba ya CHADEMA inamtambua kuwa ni Mtendaji Mkuu wa CHADEMA.

Tundu Lissu is relishing a new role while damaging CHADEMA fundamental principles and structure in long run!

Tundu Lissu kusimama na kuanza kutoa madai ya ubaguzi huku akituhumu na kutaja majina ya viongozi wakuu wa taasisi nyeti za nchi kama JWTZ, Polisi, DPP, Jaji Mkuu na Mwanasheria Mkuu wa serikali halafu anasema wameteuliwa na Rais kwa sababu wanatoka katika kanda ya Ziwa anayotoka Rais na sio kwa sababu ya fani zao, weledi na utendaji kazi inaweza kuwafurahisha na kuzikonga nyoyo za baadhi ya watu lakini hapo hapo anawafanya watu wa kanda hiyo na pia wenye fikra pana wamuangalie kwa jicho lingine!

Ubovu wa uongozi na kukosa mwelekeo makini unawafanya baadhi ya wanachama na wapenzi wa CHADEMA kuanza kusema ‘’Tundu Lissu for President in 2020’’ huku wengine wakisema, Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dkt. Mashinji waachie ngazi.

Maneno ya baadhi ya watu kudai Tundu Lissu awe mgombea Urais 2010 yamemfanya Edward Lowassa atoe tamko kuwa atagombea tena nafasi ya Rais wa Tanzania mwaka 2020!

Kuibuka kwa Tundu Lissu kunairudisha CHADEMA kuanza tena siasa za uanaharakati kwa sababu Tundu Lissu ni mwanaharakati na sio statesman. Siasa za uanaharakati mara nyingi hufanywa na chama ambacho ndio kinaingia kwenye ulingo wa kisiasa. Hizi ni siasa zenye msingi wa kukitambulisha na kukieneza chama ambacho bado ni kipya katika macho na masikio ya wananchi wengi.

CHADEMA ya sasa ilishavuka hatua ya siasa za kianaharakati. Watu wenye uwezo kifikra, kiuchumi na kiuongozi wanaisikiliza kwa makini na kuchukua kwa uzito zaidi kila kile CHADEMA inachokisema na kukitenda. Hili ndilo kundi muhimu sana katika mstakabali wa taifa lolote. Huwezi kulikuta kwenye siasa za uanaharakati.

CHADEMA kurudi kwenye siasa za uanaharaki ni kurudi nyuma kisiasa na hii inaonyesha ni jinsi gani imepiga hatua za kinyume nyume tokea Dkt. Slaa ajiondoe kama Katibu Mkuu.
Good that you have seen the light, Lissu is going to be President of Tz come 2020, kindly convey this message to juma ponda maharage that when ascended to power we will hold him accountable for all his deeds.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom