MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,172
- 23,975
Kwa wasiofahamu vizuri, ombwe ni utupu wa kutokuwa na kitu kwa kipindi fulani, yawezekana ikawa ni mawazo, vitu au hali fulani.
Mwanafilosofia kutoka Ugiriki aliyeitwa Aristotle aliwahi kusema, “horror vacui (nature abhors vacuum)”, hii ina maana kuwa haiba ya kidunia haikubali ombwe litokee bila kujazwa.
Kuibuka kwa Tundu Lissu ndani ya CHADEMA kama ndiye ‘’nembo’’ ya CHADEMA katika kipindi hiki cha utawala wa awamu ya tano sio kama kimekuja kwa bahati mbaya au nzuri bali ni kwa sababu mazingira ya CHADEMA kwa sasa yana ombwe la viongozi wakuu na mwelekeo wa chama kifalsafa.
Ieleweke kuwa vyama vya siasa ni watu na watu ndio hutoa viongozi lakini kama watu wameshindwa kutoa viongozi makini na weledi wenye kujaza ombwe la uongozi bora basi nature (asili) itatumia nafasi hiyo kutoa kiongozi wa wakati huo hata kama hafai katika mazingira endelevu.
Kuibuka kwa Tundu Lissu kama kinara katika siasa za CHADEMA kunatoa angalizo kwa viongozi wakuu wa CHADEMA kuwa hawatoshi kwa mazingira ya siasa za sasa.
Yanayotokea ndani ya CHADEMA kwa sasa yananikumbusha yaliyotokea wakati wa utawala wa Mzee Mwinyi wakati CCM na serikali yake inahangaika na mivutano ya kiitikadi na kifalsafa kuhusu mwelekeo wake.
Kundi kubwa ndani ya CCM lilikuwa bado linaishi katika ndoto na maisha ya dhana ya uchumi ulio chini ya msingi wa Ujamaa na Kujitegemea wakati kundi dogo la viongozi wakuu walikuwa wameamua kuingia katika dhana ya uchumi wa soko huria bila kuwa na misingi ya katiba na sheria iliyo imara katika kupambana na ‘’ombwe’’ la mpito wa kisiasa na kiuchumi.
Mivutano hii ilileta misukosuko ya Kiuongozi na kutikisika kwa Muungano iliyomfanya Mwl. Nyerere mwaka 1993 kuandika kitabu kinachoitwa Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania. Katika kitabu hicho Mw. Nyerere alisema, hulka huchukia ombwe akitumia maneno ya Aristotle , ‘’Nature abhors a vacuum’’, Mwl. Nyerere aliezea zaidi na kusema, ‘’hata siasa huchukia ombwe. Kama uongozi ni mbovu, upo kama haupo, au upo kwa maslahi ya wenyewe, watatokea watu waujaze uwazi uliopo; hauwezi kuachwa wazi hivi hivi. Lakini uongozi mbovu ni kama mzoga, una tabia ya kukaribisha mafisi na mainzi’’.
Mivutano ya CCM wakati wa utawala wa Rais Mwinyi haina tofauti na kinachoendelea kwa sasa ndani ya CHADEMA. CHADEMA ya sasa haijui vizuri mwelekeo wake kifalsafa kutokana na mivutano ya kiungozi iliyoanza baada ya Lowassa na genge lake kutua CHADEMA.
Uongozi wa CHADEMA kwa sasa ni mbovu, upo kama haupo na upo kwa maslahi ya watu wachache. Kutokana na ‘’Ombwe’’ hili ndio maana kwa sasa limeanza kujazwa na Tundu Lissu. Tundu Lissu sio kwamba ni kiongozi mwenye ueledi na shupavu bali ‘’ombwe’’ linamuona ni afadhari ya uongozi uliopo!
Uongozi wa Juu wa CHADEMA umeanza kuwa mbovu siku ambayo walimkaribisha Lowassa na genge lake na Dkt. Slaa kuachia nafasi ya Katibu Mkuu.
Unapomuona Mwenyekiti Mbowe na Katibu wa CHADEMA Taifa, Mashinji ambao ndio viongozi wakuu wa chama wanakuwa wafungua mlango wa gari la Lowassa ili Lowassa ashuke au apande lazima utajiuliza maswali mengi kuhusu nafasi ya viongozi wakuu katika chama na hatima ya chama.
Tundu Lissu hakuweza kuibuka wakati wa uongozi wa Dkt. Slaa kwa sababu ‘’Ombwe’’ la uongozi lilijazwa vizuri na Dkt. Slaa. Masuala yote yanayohusu dira/mwenendo wa CHADEMA na hoja kuhusu mwenendo wa serikali zilijibiwa na Dkt. Slaa kwa weledi na hekima ya juu kama Mtendaji Mkuu wa CHADEMA. Hata pale Tundu Lissu alipojaribu kuleta siasa za uanaharakati alipigwa stop na wazee ndani ya CHADEMA.
Nakumbuka wakati wa mchakato wa Katiba Mpya aliibuka na kusema ''Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu''. Hapo hapo Mzee Edwin Mtei akaibuka na kumpiga stop akimwambia, ‘’ With all due respect to Hon. Tindu Lissu, this smacks BAD TASTE’’
Alichokisema Tundu Lissu kuhusu Mwl. Nyerere unaweza kusoma hapa;
GONGA LINK>>Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu
Alichokisema Mzee Edwin Mtei kuhusu Tundu Lissu unaweza kusoma hapa;
GONGA LINK>>Mzee Edwin Mtei asikitishwa na alaani kitendo cha Tundu Lissu kumtukana Baba wa Taifa, Mwl. Nyerere
Maoni na mwelekeo wa Tundu Lissu kwa sasa umekuwa ndio dira/mtazamo wa CHADEMA kama chama/taasisi. Suala lolote linalohusu dira/mtazamo wa CHADEMA anayeulizwa na kutoa maoni ni Tundu Lissu badala ya Mwenyekiti au Katibu Mkuu ambaye Katiba ya CHADEMA inamtambua kuwa ni Mtendaji Mkuu wa CHADEMA.
Tundu Lissu is relishing a new role while damaging CHADEMA fundamental principles and structure in long run!
Tundu Lissu kusimama na kuanza kutoa madai ya ubaguzi huku akituhumu na kutaja majina ya viongozi wakuu wa taasisi nyeti za nchi kama JWTZ, Polisi, DPP, Jaji Mkuu na Mwanasheria Mkuu wa serikali halafu anasema wameteuliwa na Rais kwa sababu wanatoka katika kanda ya Ziwa anayotoka Rais na sio kwa sababu ya fani zao, weledi na utendaji kazi inaweza kuwafurahisha na kuzikonga nyoyo za baadhi ya watu lakini hapo hapo anawafanya watu wa kanda hiyo na pia wenye fikra pana wamuangalie kwa jicho lingine!
Ubovu wa uongozi na kukosa mwelekeo makini unawafanya baadhi ya wanachama na wapenzi wa CHADEMA kuanza kusema ‘’Tundu Lissu for President in 2020’’ huku wengine wakisema, Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dkt. Mashinji waachie ngazi.
Maneno ya baadhi ya watu kudai Tundu Lissu awe mgombea Urais 2010 yamemfanya Edward Lowassa atoe tamko kuwa atagombea tena nafasi ya Rais wa Tanzania mwaka 2020!
Kuibuka kwa Tundu Lissu kunairudisha CHADEMA kuanza tena siasa za uanaharakati kwa sababu Tundu Lissu ni mwanaharakati na sio statesman. Siasa za uanaharakati mara nyingi hufanywa na chama ambacho ndio kinaingia kwenye ulingo wa kisiasa. Hizi ni siasa zenye msingi wa kukitambulisha na kukieneza chama ambacho bado ni kipya katika macho na masikio ya wananchi wengi.
CHADEMA ya sasa ilishavuka hatua ya siasa za kianaharakati. Watu wenye uwezo kifikra, kiuchumi na kiuongozi wanaisikiliza kwa makini na kuchukua kwa uzito zaidi kila kile CHADEMA inachokisema na kukitenda. Hili ndilo kundi muhimu sana katika mstakabali wa taifa lolote. Huwezi kulikuta kwenye siasa za uanaharakati.
CHADEMA kurudi kwenye siasa za uanaharaki ni kurudi nyuma kisiasa na hii inaonyesha ni jinsi gani imepiga hatua za kinyume nyume tokea Dkt. Slaa ajiondoe kama Katibu Mkuu.