Kuibuka kwa suala la bandari ya Bagamoyo ni uthibitisho kuwa Kikwete ndo anaeongoza nchi kwa sasa!

Wewe iyo mikataba aliyoingia hayati umewahi kuiona? Una uhakika gani kama sio ya upigaji? Mambo mangapi amesema ambayo yamekuja kuwa sio kweli?

Aliwahi kutuambia ndege zimetengeneza faida ya deal milion kumi na nne juzi CAG anasema ndege zimeingiza hasara kwa miaka 5 mfululuzo. Utamwamini vipi mtu kama huyu?
Unahakika gani kama CAG anasema ukweli?! Kwa nini usifikirie kuwa tunaweza kuwa tunapigwa... Kwa kuonyeshwa hasara na watu waka pindisha kuwa zao?
 
Kikwete hana uchungu na Tz. Alishatupiga gesi asilia ya Mtwara.
ALIKABIDHI BANDALI YETU YA DAR ES SALAAM KWA HOME SHOPPING CENTRE NA KUMPA UBALOZI MDOGO MWANA FAMILIA WA HOME SHOPPING CENTRE HUKO CHINA!!! Mama Samia LAZIMA AWE MUANGALIFU SANA NA HUYU MTU AMA SIVYO ATAUWEKA URAIS WAKE REHANI!!!
 
ALIKABIDHI BANDALI YETU YA DAR ES SALAAM KWA HOME SHOPPING CENTRE NA KUMPA UBALOZI MDOGO MWANA FAMILIA WA HOME SHOPPING CENTRE HUKO CHINA!!! Mama Samia LAZIMA AWE MUANGALIFU SANA NA HUYU MTU AMA SIVYO ATAUWEKA URAIS WAKE REHANI!!!
Nchi iliuzwa kwa wachina ili kumuokoa mwanaye Ridhiwani. Sasa Mama Samia akimchekea tu huyu mjomba wa msoga atavuna mabua.
 
Tatizo raia tunatoa hukumu kama vile tunajua vopengele vya mkataba. Kwa nini huo mkataba usipelekwe bungeni ukajadiliwe?
Huu utaratibu wa kuifanya mikataba yote ya nchi siri ndio maana tunapigwa kila mahali.

Yani ripoti za CAG zingekuwa zinawekwa wazi bila kuhaririwa na Rais tungekimbiana humu. Viongozi wanajificha kwenye miradi ya miundombinu kumbe ndio wanaipiga nchi hatari.
Spika ndugai alinyamaza kimya wakati JIWE lipo hai, sasa mwendazake kaondoka ndugai anasema JIWE alishauriwa vibaya

Sasa kwa akili yako kwa bunge lile la ndugai ukipeleka mkataba wa bandari ukajadiliwe utaambiwa ukweli au utazuiliwa kijenga?

Kwanin kama ni bandari wasijenge huko mtwara kwenye kina cha asilia cha maji?

Tatizo la nchi hii akili ndogo iñaongoza akili kubwa
 
Hivi karibuni kumeibuka suala la bandari ya bagamoyo ambayo mh. Hayati JPM alilikataa kwa kuwa mkataba wake ulikuwa wa kinyonyaji.

Hivi karibuni suala hilo limeibuka tena upya na spika wa bunge ameonekana kulikingia kifua na kudiriki kusema kuwa Mh Rais alishauriwa vibaya.

Je, Mh Ndugai ameamua kuwa kibaraka wa mabeberu baada ya hayati kututoka? Au ni mpango mkakati wa Mh. JK ambaye ndo muasisi wa mradi huo kutumia bunge kuuhuisha mradi huo.

Ni dhahiri kuwa JK aliutamani sana mradi huo ili aache legacy kwa watu wake wa Bagamoyo. Kwa kuwa inasemekana ndo mshauri mkubwa kwa mama SSH ataitumia nafasi hiyo kikamilifu kuurudisha!

Hitimisho: Kwa kuwa mkataba huo una sintofahamu kadhaa ni vyema basi ukapitiwa upya ili kuepuka ulaghai wa wachina. Ni aibu kubwa kwa viongozi wetu wa karne ya 21 kuingia kwenye bogus treaties km kina Mangungo wa msowero!
Mangungo hakuingia mkataba wa kulaghai, bali alidanganywa
 
Kabla ya lolote. Tafuta ili ripoti ya huu mradi uisome.

Magu alitulisha matango pori.

Na huu mradi sasa una fanywa Msumbiji.
Huu uwekezaji mkataba wake upelekwe bungeni uwekwe wazi hatujui Nani mkweli waungaji mkono walitakiwa waunge mkono wakati Magufuli yu hai.hivi hawa viongozi,wabunge ,spika Ndugai ulishindwaje kutetea mradi kama huu ambau waliamini hauna tatizo ambao ungeleta mapinduzi makubwa ya uchumi.Mh Ndugai & Co wekeni wazi.
NASHAURI watanzania kwa hili tuwezke pembeni tofauti zetu hata wale walioumizwa na hata wapendwa wao kuuwawa nyakati za mwendazake ,tudai uwazi.
Maana mwendazake alituambia mengi ikiwa misamaha ya Kodi kwa miaka mingihaturuhusuwi kudai chochote,hatutaruhusiw kuendeleza bandari zetu toka kaskazini mpaka kusini mengine mengi!
Kama asemayo Ndugai kweli ni mambo mangapi maouvu alimwachia mwendazake kufanya huku alipiga makofi na kukenyua meno,Ndugai ni aibu ya taifa,bunge lako ni fedhea kuu ulipaswa kujiuzulu .uliambiwa bunge ni muhimu uhuru lakini ukuacha kujipendekeza,leo si unajipendekeza kwa wenye nguvu wanaotoka huo mradi?
Kwa maslahi mapana na kuondoa utata mkataba ujadiriwe bungeni
Tunadai viongozi wetu waseme ukweli bila kujali matumbo yao waliunga mkono mateso makubwa kwetu leo wanabadilika hao ni wasalit kwa watanzania kama viongozi wa mihimili ya bunge/ mahakama wanashindwa kusimamia haki Nani atajaribu?Lissu alipopigwa risasi alikuwa na madaraka ya kikatiba angalu kulipa sehemu ya matibabu yake alifanya Nini jamani?huyu ni muovu ameshiriki uovu anajioedekeza kwa mama Rais Samia
.mh RAIS wambie mkataba uwe wazi wasikutumie.
 
Hata kama amefariki lazima tuseme ili waliopo wajifunze

1. Alikuwa mtu mwenye roho mbaya, mshenzi, muuaji na aliyependa kuona watu wenye maendeleo au waliotofautiana nae wakiteseka sana. Mfano wa haya ni kwa vile walivyowafanyia Manji, Erick Kabendera, Ben saanane, Rwabaje, Mama yake Erick Kabendera, Mdude Nyangali, Zacharia na watu wengine wengi

2. Alikuwa mtu Mbinafsi sana, aliyependa sifa zote zirudi kwake. Alipenda kusifiwa, kuonekana yeye ni bora kuliko wenzake. Hata kwenye hotuba zake alipenda kujionesha ni yeye zaidi na wala sio wenzake. Rejea hotuba alizokuwa akisema bila yeye miradi haitofanikiwa. Aliwapa vyeo bila aibu watu waliokuwa wakimsifu yeye binafsi. Mf. Katambi, Sabaya, kafulila, Mrema, Babu

3. Alikuwa mkabila na mbaguzi wa kikanda aliyetukuka. Kwenye awamu yake alijaza watu wa kanda ya ziwa hasa wasukuma na mapandikizi wenzake kutoka Rwanda na Burundi kwenye nafasi nyeti serikalini. Bashiru, Kakoko, Doto James na wengineo wengi ni mifano michache tu. Hawa watu walikuwa hawagusiki na waliweza kufanya lolote lile kwa jina lake na yeye hakusema lolote. Hawa watu waliweza hata kuwadharau waziwazi Waziri Mkuu na Makamu wa Rais na wala hawakujali mfumo wa utendaji serikalini. Waliweza kupiga simu au kupita moja Kwa moja ikulu hadi kwa Magufuli bila kupita kwa waziri, waziri mkuu au hata Makamu wa Rais.

4. Kwa kujua kwake kuwa ni kweli aliharibu uchumi wa nchi kwa sera zake mbaya, aliwekeza sana kwenye propaganda za kujitangaza sana kupitia vyombo vya Habari ili kuwa brainwash watu wasiofikiri vizuri. Tv zote, magazeti, blogu na hata viongozi wa dini aliwatumia kumtangaza yeye muda wote na kumsifu yeye muda wote ili aonekane ni Bora kuliko wenzake. Ofisi za Taifa zilifanywa kutengeneza data za uongo ili aonekane anafanya vizuri kumbe nchi ilikuwa inaenda pabaya sana. Rejea taarifa aliyotoaga kuwa ATCL inapata faida ya bil 28.

5. Aliwadharau sana wenzake. Na alifanya kila jitihada wenzake waonekane watu wasiofaa ( hasa viongozi waliopita). Aliishi nao kiunafiki akiwatumia vijana wake Kama Msiba, Sabaya , Makonda na Aly Happi kuwatukana na kuwatisha ili aharibu taswira yao kwa jamii na ajitengeneze kuwa ni Bora kuliko wao.

6. Alianzisha mambo ili kuwakomoa watu waliokuwa tofauti nae. As Kofi niwemugizi, Aidan Eyakuze, Yusuph Manji ni wachache kwenye hii list, walianza kuhojiwa uraia, wakanyang’anywa passport na kupewa kesi mbalimbali ili kukomolewa kutokana na kutofautiana nae.

7. Kwa sera zake mbovu, aliharibu kwa kiasi kikubwa uchumi hivyo kupelekea kuwepo tatizo kubwa la ajira . Ili kujiokoa na Tatizo hili Kwa kuwapumbaza watanzania wajinga alianzisha utaratibu wa kujifanya kuwa karibu na Mama lishe na bodaboda huku akisema kuwa wanaruhusiwa kufanya Biashara popote pale. Alifanya hili Kwa sababu alijua kabisa kuwa ameharibu uchumi wa Tanzania na amesababisha watu wengi kukosa ajira. Kuepuka lawama akataka kuifanya nchi nzima kuwa nchi ya wachuuzi huku akiharibu mipango miji na kusababisha walipa kodi wapungue kwa kasi.

8. Kutokana na kuwa na sera mbovu za kiuchumi huku akiiba Mali za watanzania Kwa kigezo cha uzalendo, akiogopa kupinduliwa na jeshi na wasaidizi wake, aliamua kufuatilia maongezi ya wasaidizi wake wote akiwemo Makamu wa Raisi , Mawaziri na viongozi wa Ccm. Alikuwa hadi meseji zao anasoma na alivyo mshamba alikiri hadharani kuwa anafuatilia mawasiliano ya watu. Alianzisha pia utaratibu wa wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama kuwa nae popote pale anapokuwepo. Huu utaratibu ulikuja kuonekana katika awamu ya 5 tu maana Kwa awamu ya 1 hadi ya 4 haikuwai kutokea wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na spika na Jaji mkuu kuambatana na Rais popote pale anapokuwa.

9. Alikuwa muuaji
Niliwai bishia watu wengi kwenye hili ila nilikuja kuthibitisha alipokuja tamka hadharani kuwa huwezi kuwa msaliti alafu uka survive na baada ya hotuba yake iyo Tundu Lissu alikuja kushambuliwa kwa Risasi 38 huku 16 zikiingia mwilini wake.

10. Alijiona ni Bora kuliko mtu yeyote yule na alitaka neno lake ndo liwe mwisho. Alisema hadharani kuwa hashauriki na kila mtu aliyekuwa akimshauri alimchukulia kama adui yake. Siku za mwisho za uhai wake alitofautiana na kupingana Hadi na viongozi wa dini wa kanisa katoliki ambao waliamua kushauri nchi kuchukua hatua tofauti dhidi ya corona.

Mungu fundi sana! Alale anapostahili mwendazake.
Kweli alale anapostahili
 
Hivi karibuni kumeibuka suala la bandari ya bagamoyo ambayo mh. Hayati JPM alilikataa kwa kuwa mkataba wake ulikuwa wa kinyonyaji.

Hivi karibuni suala hilo limeibuka tena upya na spika wa bunge ameonekana kulikingia kifua na kudiriki kusema kuwa Mh Rais alishauriwa vibaya.

Je, Mh Ndugai ameamua kuwa kibaraka wa mabeberu baada ya hayati kututoka? Au ni mpango mkakati wa Mh. JK ambaye ndo muasisi wa mradi huo kutumia bunge kuuhuisha mradi huo.

Ni dhahiri kuwa JK aliutamani sana mradi huo ili aache legacy kwa watu wake wa Bagamoyo. Kwa kuwa inasemekana ndo mshauri mkubwa kwa mama SSH ataitumia nafasi hiyo kikamilifu kuurudisha!

Hitimisho: Kwa kuwa mkataba huo una sintofahamu kadhaa ni vyema basi ukapitiwa upya ili kuepuka ulaghai wa wachina. Ni aibu kubwa kwa viongozi wetu wa karne ya 21 kuingia kwenye bogus treaties km kina Mangungo wa msowero!
Muhimu mikataba yote iwekwe wazi
 
Kabla ya lolote. Tafuta ili ripoti ya huu mradi uisome.

Magu alitulisha matango pori.

Na huu mradi sasa una fanywa Msumbiji.
Hatutaki ripoti ya mradi.

Tunataka mkataba wa mradi.

Ndugai anasema uongo wa wazi wazi kwamba Rais JPM alidanganywa. JPM alikuwa hajui kusoma kilichoandikwa kwenye mkataba ?

Waziri mtia saini, Mary Nagu, alisema mkataba ulipitiwa na cabinet.

JPM aliuona mkataba akiwa kwenye cabinet ya JK. Kwa hiyo JPM alidanganywa na nani, na waziri mwenzake aliyekuwa amekaa pembeni yake kwenye cabinet ???
 
Back
Top Bottom