Kuibuka kwa suala la bandari ya Bagamoyo ni uthibitisho kuwa Kikwete ndo anaeongoza nchi kwa sasa!

Duplicate_90

Senior Member
Mar 29, 2020
177
250
Hivi karibuni kumeibuka suala la bandari ya bagamoyo ambayo mh. Hayati JPM alilikataa kwa kuwa mkataba wake ulikuwa wa kinyonyaji.

Hivi karibuni suala hilo limeibuka tena upya na spika wa bunge ameonekana kulikingia kifua na kudiriki kusema kuwa Mh Rais alishauriwa vibaya.

Je, Mh Ndugai ameamua kuwa kibaraka wa mabeberu baada ya hayati kututoka? Au ni mpango mkakati wa Mh. JK ambaye ndo muasisi wa mradi huo kutumia bunge kuuhuisha mradi huo.

Ni dhahiri kuwa JK aliutamani sana mradi huo ili aache legacy kwa watu wake wa Bagamoyo. Kwa kuwa inasemekana ndo mshauri mkubwa kwa mama SSH ataitumia nafasi hiyo kikamilifu kuurudisha!

Hitimisho: Kwa kuwa mkataba huo una sintofahamu kadhaa ni vyema basi ukapitiwa upya ili kuepuka ulaghai wa wachina. Ni aibu kubwa kwa viongozi wetu wa karne ya 21 kuingia kwenye bogus treaties km kina Mangungo wa msowero!
 

DENLSON

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
461
1,000
Wewe iyo mikataba aliyoingia hayati umewahi kuiona? Una uhakika gani kama sio ya upigaji? Mambo mangapi amesema ambayo yamekuja kuwa sio kweli?

Aliwahi kutuambia ndege zimetengeneza faida ya deal milion kumi na nne juzi CAG anasema ndege zimeingiza hasara kwa miaka 5 mfululuzo. Utamwamini vipi mtu kama huyu?
 

Duplicate_90

Senior Member
Mar 29, 2020
177
250
Wewe iyo mikataba aliyoingia hayati umewahi kuiona? Una uhakika gani kama sio ya upigaji? Mambo mangapi amesema ambayo yamekuja kuwa sio kweli?

Aliwahi kutuambia ndege zimetengeneza faida ya deal milion kumi na nne juzi CAG anasema ndege zimeingiza hasara kwa miaka 5 mfululuzo. Utamwamini vipi mtu kama huyu?
Kuna haja ya kuweka mikataba yote wazi ili sisi wenye nchi tuijue kabla ya kupitishwa na serikali
 

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
9,732
2,000
Huko hata kama ulipigwa lakini nchi yako bado unayo ikiwa kamili utayasahau machungu baada ya muda kidogo. Huko kwenye Bandari ya Bagamoyo utapigwa na nchi yako itamegwa kupewa Wachina ambao mnapenda kuwaita "marafiki na ndugu zetu"
Ulishawahi kuomba Mikataba kwenye miradi ya JPM, uwanja wa ndege Chato nk, huko sasa ndio tulikuwa tunapigwa kiume.
 

tamsana

JF-Expert Member
Jan 13, 2012
914
1,000
Tatizo raia tunatoa hukumu kama vile tunajua vopengele vya mkataba. Kwa nini huo mkataba usipelekwe bungeni ukajadiliwe?
Huu utaratibu wa kuifanya mikataba yote ya nchi siri ndio maana tunapigwa kila mahali.

Yani ripoti za CAG zingekuwa zinawekwa wazi bila kuhaririwa na Rais tungekimbiana humu. Viongozi wanajificha kwenye miradi ya miundombinu kumbe ndio wanaipiga nchi hatari.
 

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
6,828
2,000
Mwendazake alihitia ujuaji. Badala ya kulitumia bunge kupata mawazo mazuri yeye akalitumia bunge kupitisha yaliyo yake mazuri
Hata kama amefariki lazima tuseme ili waliopo wajifunze

1. Alikuwa mtu mwenye roho mbaya, mshenzi, muuaji na aliyependa kuona watu wenye maendeleo au waliotofautiana nae wakiteseka sana. Mfano wa haya ni kwa vile walivyowafanyia Manji, Erick Kabendera, Ben saanane, Rwabaje, Mama yake Erick Kabendera, Mdude Nyangali, Zacharia na watu wengine wengi

2. Alikuwa mtu Mbinafsi sana, aliyependa sifa zote zirudi kwake. Alipenda kusifiwa, kuonekana yeye ni bora kuliko wenzake. Hata kwenye hotuba zake alipenda kujionesha ni yeye zaidi na wala sio wenzake. Rejea hotuba alizokuwa akisema bila yeye miradi haitofanikiwa. Aliwapa vyeo bila aibu watu waliokuwa wakimsifu yeye binafsi. Mf. Katambi, Sabaya, kafulila, Mrema, Babu

3. Alikuwa mkabila na mbaguzi wa kikanda aliyetukuka. Kwenye awamu yake alijaza watu wa kanda ya ziwa hasa wasukuma na mapandikizi wenzake kutoka Rwanda na Burundi kwenye nafasi nyeti serikalini. Bashiru, Kakoko, Doto James na wengineo wengi ni mifano michache tu. Hawa watu walikuwa hawagusiki na waliweza kufanya lolote lile kwa jina lake na yeye hakusema lolote. Hawa watu waliweza hata kuwadharau waziwazi Waziri Mkuu na Makamu wa Rais na wala hawakujali mfumo wa utendaji serikalini. Waliweza kupiga simu au kupita moja Kwa moja ikulu hadi kwa Magufuli bila kupita kwa waziri, waziri mkuu au hata Makamu wa Rais.

4. Kwa kujua kwake kuwa ni kweli aliharibu uchumi wa nchi kwa sera zake mbaya, aliwekeza sana kwenye propaganda za kujitangaza sana kupitia vyombo vya Habari ili kuwa brainwash watu wasiofikiri vizuri. Tv zote, magazeti, blogu na hata viongozi wa dini aliwatumia kumtangaza yeye muda wote na kumsifu yeye muda wote ili aonekane ni Bora kuliko wenzake. Ofisi za Taifa zilifanywa kutengeneza data za uongo ili aonekane anafanya vizuri kumbe nchi ilikuwa inaenda pabaya sana. Rejea taarifa aliyotoaga kuwa ATCL inapata faida ya bil 28.

5. Aliwadharau sana wenzake. Na alifanya kila jitihada wenzake waonekane watu wasiofaa ( hasa viongozi waliopita). Aliishi nao kiunafiki akiwatumia vijana wake Kama Msiba, Sabaya , Makonda na Aly Happi kuwatukana na kuwatisha ili aharibu taswira yao kwa jamii na ajitengeneze kuwa ni Bora kuliko wao.

6. Alianzisha mambo ili kuwakomoa watu waliokuwa tofauti nae. As Kofi niwemugizi, Aidan Eyakuze, Yusuph Manji ni wachache kwenye hii list, walianza kuhojiwa uraia, wakanyang’anywa passport na kupewa kesi mbalimbali ili kukomolewa kutokana na kutofautiana nae.

7. Kwa sera zake mbovu, aliharibu kwa kiasi kikubwa uchumi hivyo kupelekea kuwepo tatizo kubwa la ajira . Ili kujiokoa na Tatizo hili Kwa kuwapumbaza watanzania wajinga alianzisha utaratibu wa kujifanya kuwa karibu na Mama lishe na bodaboda huku akisema kuwa wanaruhusiwa kufanya Biashara popote pale. Alifanya hili Kwa sababu alijua kabisa kuwa ameharibu uchumi wa Tanzania na amesababisha watu wengi kukosa ajira. Kuepuka lawama akataka kuifanya nchi nzima kuwa nchi ya wachuuzi huku akiharibu mipango miji na kusababisha walipa kodi wapungue kwa kasi.

8. Kutokana na kuwa na sera mbovu za kiuchumi huku akiiba Mali za watanzania Kwa kigezo cha uzalendo, akiogopa kupinduliwa na jeshi na wasaidizi wake, aliamua kufuatilia maongezi ya wasaidizi wake wote akiwemo Makamu wa Raisi , Mawaziri na viongozi wa Ccm. Alikuwa hadi meseji zao anasoma na alivyo mshamba alikiri hadharani kuwa anafuatilia mawasiliano ya watu. Alianzisha pia utaratibu wa wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama kuwa nae popote pale anapokuwepo. Huu utaratibu ulikuja kuonekana katika awamu ya 5 tu maana Kwa awamu ya 1 hadi ya 4 haikuwai kutokea wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na spika na Jaji mkuu kuambatana na Rais popote pale anapokuwa.

9. Alikuwa muuaji
Niliwai bishia watu wengi kwenye hili ila nilikuja kuthibitisha alipokuja tamka hadharani kuwa huwezi kuwa msaliti alafu uka survive na baada ya hotuba yake iyo Tundu Lissu alikuja kushambuliwa kwa Risasi 38 huku 16 zikiingia mwilini wake.

10. Alijiona ni Bora kuliko mtu yeyote yule na alitaka neno lake ndo liwe mwisho. Alisema hadharani kuwa hashauriki na kila mtu aliyekuwa akimshauri alimchukulia kama adui yake. Siku za mwisho za uhai wake alitofautiana na kupingana Hadi na viongozi wa dini wa kanisa katoliki ambao waliamua kushauri nchi kuchukua hatua tofauti dhidi ya corona.

Mungu fundi sana! Alale anapostahili mwendazake.
 

Maghayo

JF-Expert Member
Oct 5, 2014
6,242
2,000
Sijawahi kumkubali Kikwete. Nashangaaga sana wanaomsifu humu. Tangu amsaliti Rais Lowassa namchukia sana jamaa.
 

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
2,557
2,000
Tatizo raia tunatoa hukumu kama vile tunajua vopengele vya mkataba. Kwa nini huo mkataba usipelekwe bungeni ukajadiliwe?
Huu utaratibu wa kuifanya mikataba yote ya nchi siri ndio maana tunapigwa kila mahali.
Yani ripoti za CAG zingekuwa zinawekwa wazi bila kuhaririwa na Rais tungekimbiana humu. Viongozi wanajificha kwenye miradi ya miundombinu kumbe ndio wanaipiga nchi hatari.
Mikataba ni ya ccm,bunge ni la ccm,tutakutana 2025
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom