Kuibuka Kwa Makundi makubwa ya Kihalifu,Nini kifanyike?

Freeland

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
14,481
10,217
Wadau;

Kumekuwa na wimbi la makundi yaliyoibuka hivi karibuni na kufanya uhalifu wakiwa pampja kama kundi kubwa.Makundi haya yanaundwa na vijana ambao wengi wao wamekata tamaa na maisha.Makundi haya yamejipa majina kama vile Mbwa Mwitu na Panya Road.

Wamekuwa wakibeba silaha za jadi na kuvamia maduka na makazi ya watu na kupora.Makundi haya katika jiji la Dar es salaam yamekuwa tishio kwa usalama wa raia wengine na mali zao.

Lakini.Hili ni tatizo ambalo halipaswi kuangaliwa kwa mwono wa karibu kwamba ni kundi tu la vijana wahalifu....Kuna Core issue ambayo imesababisha kuibuka kwa makundi haya;


  • Ukosefu wa Ajira-Hili ni tatizo kubwa kwa jamii ya vijana wa kitanzania ambalo limeendelea kukua siku hadi siku.Serikali haijaweka mazingira mazuri ya vijana kujiajiri na mazingira mazuri ya vijana kuajiriwa.Imewahi kuamkwa kwamba vijana ni bomu linalosubiri kulipuka....nadhani hizi ndizo dalili za bomu hilo kulipuka.
  • Kukua kwa Gap la walionacho na wasionacho-Kumezidi kuongezeka gap kati ya walionacho na wasionacho.

  1. Ilihali watawala wakijitajirisha kwa migongo ya walalahoi wengi wa kitanzania....
  2. watawala wakijijengea makasri na kuishi kama peponi...
  3. watoto wa wawatawala wakipatiwa elimu nzuri na bora ili kuweza kuwatawala walalahoi walio wengi siku zijazo....
  4. Huku watawala wakijihusisha na biashara za madawa ya kulevya na kujitajirisha kwa kuwamaliza walalahoi ambao ndio wanayatumia madawa hayo kwa sababu wamekata tamaa ya maisha.........
  5. Huku Mikataba mbalimbali ikitolewa kwa njia ya rushwa na watawala kujinufaisha.

Hayo yote yamezidi kuongeza pengo kati ya walionacho na wasionacho.

Kinachotokea wasionacho wanachoka kwa sababu hawana matumaini ya maisha na wala hawaogopi kifo wataanza sasa kujikwapulia mali ambazo watawala wamewaibia....Naam..na hili lazima lifanywe na vijana kwa sababu vijana ndio wenye nguvu.

Lazima kuna kitu kifanyike....Serikali ,jamii kwa ujumla lazima ifanye kitu....
 
Back
Top Bottom