Kuibiwa pakawepo pa kushtaki, kuna unafuu lakini kuibiwa..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuibiwa pakawepo pa kushtaki, kuna unafuu lakini kuibiwa.....

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Judgement, Apr 26, 2012.

 1. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #1
  Apr 26, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Wapendwa, unapoibiwa ukakosa pa kushtaki inauma maradufu.
  Nakumbuka zamani pale soko la Ilala wafanya biashara wa Kuku walikua wakiwapaka Kuku wagonjwa Pilipili ya unga katika ile sehemu ya nyuma ya (kutolea waste products)
  Kuku wale wagonjwa wakishapakwa pilipili wakiwekwa bandani hua hawasinzii tena! Huchangamka kwa kurukaruka kwa muasho wa pilipili,
  maana ya kutoa mfano huu ni kuwajuvya walau wizi wa namna hii wa kufichwa ulikua pia na unafuu, unaibiwa hujioni.
  Wizi wa sasa unauma mno! Unaibiwa huku unaona!
  Wala huna namna ya kuukwepa.
  Unataka utaibiwa hutaki utaibiwa!
  Makampuni ya simu VODA. AIRTEL, TIGO n.k unanunua crdt za computer kisha hutozwi kwa namna utumiavyo.
  Unaambiwa tumia hizo crdt within 1 , 2 or 5 days.
  Zikisha siku hizo hata kama voucher yao hujaitumia imekula kwako.
  Umejirusha sijui JIRUSHE, CHEKA mambo ni yaleyale!
  Umetuma msg ika'rebound salio limeenda!
  Unafungua internate ika'search kisha isifungue 0.29 kb inaliwa!
  Tunaibiwa hata pumbazo hawahitaji !
  Pa kushtaki hakuna!
  I n a u m a s a n a!
   
 2. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #2
  Apr 26, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Pole baby wangu.
   
 3. Mtalingolo

  Mtalingolo JF-Expert Member

  #3
  Apr 26, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,188
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Inauma sana mkuu, unakuta mtu unapigiwa simu bt ukiangalia salio limepungua kwako.
   
 4. Brown ad

  Brown ad JF-Expert Member

  #4
  Apr 26, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 347
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Ni kweli inauma sana kuna tabia ipo katika masoko makubwa mtu anakuja na bidhaa kwa yenye thamani kama tsh 10000 yeye anakuambia uumpe 3500 ukishachukua anakufuata tena anakuambia ameghairi so anakurudishia hela yako sasa baada ya muda ndo unakuja kutahamaki umerejeshewa karatasi japo ni ndogo lakini inauma mtu kukufanya mjinga na hauna pa kushitaki!
   
 5. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #5
  Apr 26, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Senkyu Totoz!
   
 6. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #6
  Apr 26, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Na hasa BROWN wizi wa style uisemayo hua upo mipakani ktk kubadili pesa, Namanga, Sirari, Horohoro ni mfano.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #7
  Apr 26, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mie nililizwa k'koo kwa stahili hii ya nguo bei kubwa ninunue, ile kulipa mara jamaa anabadilika eti nimuongeze pesa, kukataa akanirudishia pesa zangu, kumbe nishaumizwa! kudadeki!
  Nimekoma kununua nguo za mkononi!

   
 8. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #8
  Apr 26, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Mkuu Michael Scofield, usiniambie!
  Pale Sirari boder nilichange laki moja ya buku ten-ten nyekundu 10 kabla ya hizi noti mpya hazijawa establish,
  akanipatia K'sh ile nataka kuondoka kanifata mkuku,
  "Muheshimiwa nimekosea hesabu (akimaanisha amenipigia hesabu below actual day rate) .
  Nikamwambia haya piga upya , alipopiga ikaonekana nimuongezee Tsh (akifanya hivyo aim yake ni kukupanikisha ili ujae povu uvunje biashara)
  na kweli mtu mzima nikazomokwa! Sasa hapo kwenye kurudishiana ndipo unapofungwa bao!
  Zingatia ilikua ni usiku kama wa saa 1 .30- kwenda saa mbili, mi nikampa Ksh zake zilezile, yeye kumbe kanipa elfu tano-tano , noti 10 equv, elfu 50!
  Kisicho riziki hakiliki, nilipokujashtuka dakika 10 anyau! Nikasema acha nijaribu kumsamamba kwakua muda wa gari ulikua bado.
  Hamad sijamfumania kunako grocery anakula kinywaji. Cha kwanza nilianza nae kichwa na ngumi 3 za adabu.
  Nikamwambia unanipa hela yng au tuendeleze mchapo?
  Fasta akanipa 50 namie kona.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...