Kuibiwa na dawa ya kumfanya mtu kusema ukweli

From Sir With Love

JF-Expert Member
Sep 13, 2010
2,076
3,797
Kuna jamaa yangu tunafanya naye kazi alipatwa na kisa cha kuibiwa hela zake kwenye ATM.

Baada ya uchunguzi na taarifa za msichana wake pamoja na kumbukumbu kidogo, iligundulika mara ya mwisho alikuwa baa na akaja jamaa mgeni akakaa kwenye meza aliyokaa. Baada ya muda wakazoeana na jamaa mgeni akamnunulia pombe kwa staili ya kuzungusha.

Baada ya muda akaja binti ambaye ni msichana wa siku nyingi wa jamaa yangu ambaye walikuwa na miadi.

Kwa sababu jamaa yangu na yule binti wana urafiki wa siku nyingi, binti alishindwa kumwelewa jamaa yake kwa jinsi alivyokuwa anamjibu yule jamaa mgeni kwa adabu nyingi kama wanafahamiana siku nyingi ilhali jamaa yake hana marafiki hiyo sehemu.

Inaonekana yule jamaa mgeni alivyo mwona mdada amekuja akajua picha itaungua na akamwomba jamaa wahame kiwanja.

Lakini kibaya zaidi kila kitu alichokuwa anasema jamaa mgeni, rafiki yangu alikuwa anamsikiliza sana kuliko msichana wake.

Baadaye yule jamaa mgeni alimshauri jamaa yangu amwambie msichana wake aondoke ili wastarehe vizuri. Na kweli akamfukuza.

Baadaye ndiyo jamaa yangu katika kukumbuka akagundua walienda mpaka kwenye ATM na jamaa mgeni ila hakumbuki vizuri kilichotokea.

Jamaa yangu aliibiwa milioni 2 kwa siku mbili mpaka siku ya tatu aliposhtuka hana ATM card yake na kwenda kuripoti.

Ni kweli kuna dawa ya kukufanya useme ukweli bila shuruti?

HEBU IFAHAMU HII DAWA

Sodium thiopental ni dawa iliyovumbuliwa miaka ya 1930 ikiwa ni dawa ya tabaka la barbiturates.

Matumizi ya hii dawa mwanzoni yalikuwa ni kumpa mtu usingizi wakati wa upasuaji, lakini kama vile Viagra ilivyogunduliwa bila kutarajia ndivyo thiopental ilivyogunduliwa kama ‘dawa ya kusema ukweli’

Dawa zenye tabaka la barbiturates hufanya mawasiliano kati ya ubongo na uti wa mgongo yawe ya taratibu sana na hatimaye huleta usinginzi ikiwa ya kiwango kikubwa.

Dawa hii hutumiwa sana na majasusi ili kujua taarifa za mtekwa kwa upande wa pili.

KWANINI ITUMIWE KUMFANYA MTU ASEME UKWELI?

Thiopental huingia mwilini na kufanya kazi baada ya sekunde 40.

Dawa ya Thiopental humfanya mtu azungumze bila kusita na asikumbuke alichokisema baadaye, haya hufanyika wakati mtu yupo katikatika ya kupoteza fahamu na kuwa na ufahamu.

Wataalam hufananisha Thiopental na pombe. Waswahili wanasema ukitaka kujua siri za mtu basi anywe pombe. Hii ni kwa sababu pombe hupunguza kasi ya kufikiri na hivyo inakuwa rahisi kusema ukweli kuliko kudanganya. Kudanganya hutumia nguvu nyingi za kufikiri.

Mwandishi wa maswala ya sayansi wa BBC Michael Mosley, aliijaribu hii dawa chini ya uangalizi wa madakatari bingwa kwa kutaka kudanganya akiwa amechomwa Thiopental lakini dose ilipoongezwa ikabidi aseme ukweli.

Can a drug make you tell the truth? - BBC News
 
Kuna Watu waongo sana. Ukimwekea dawa hiyo atasema uongo mwingi kuliko ukweli kwa sababu hatumii nguvu nyingi kufikiri kusema uongo.

Nasikia origin ya dawa ni South Amerika
 
bongo inapatika na wapi mkuu

Hata sijui Bongo inapatikana wapi na hata ningejua nisingekwambia.
Kuna nyakati baadhi ya Watu walilalamika kuibiwa kwa mtindo huo. Sina hakika kama malighafi
ilikwisha.

Ila kuwa makini, ukiuchezea vibaya unaweza kukuua hata mwenyewe, ni type ya madawa ya kulevya
very expensive.
 
Back
Top Bottom