Remmy
JF-Expert Member
- Jun 9, 2009
- 4,703
- 1,797
Napenda kutoa masikitiko yangu kwa CCM, JK na NEC kwa kitendo cha kinyama na ukiukwaji wa haki sawa kwa watu wenye ulemavu kupewa fursa ya kuchaguliwa. kitendo cha kumpora jimbo dada huyu aliyepambana na vigingi vingi kwenye kampeni. alifanya kampeni kwa siku 70 non stop kafanya mikutano vijiji 80 kati ya 81 jimboni, kafika hata vijiji ambavyo viongozi wa wilaya na wagombea hawajawahi kufika,usafiri ni wa tazara tu, amepanda kiberenge ili kuvifikia vijiji hivyo,wananchi walimfurahia na kumpenda sana hadi ikatokea kibibi kizee kumpa fedha ya sh 500 kwa furaha ya kufika kwake. hakuangalia ulemavu wake alisonga mbele na amefanikiwa kufanya mikutano 130 wakati wa ccm haikuzidi hata 50. ni mlemavu wa viungo wa kwanza tz kusimama jimboni leo hii mnamuibia kura? wakati wananchi wamemchagua. JK huna moyo? huna huruma? huna ubinadamu kabisa nimekuchukia wewe na NEC, CCM na nimeapa neva in politics na nadhani huko hakuna haki na alaaniwe aliyeleta siasa. na waombeni wanaharakati mteteeni binti huyu wana kilombero wanamlilia. hivi hamna MUNGU? Si muwe mnawateua tu wabunge tujue moja.