Elections 2010 Kuibiwa kura kwa REGIA MTEMA

Remmy

JF-Expert Member
Jun 9, 2009
4,708
2,000
Napenda kutoa masikitiko yangu kwa CCM, JK na NEC kwa kitendo cha kinyama na ukiukwaji wa haki sawa kwa watu wenye ulemavu kupewa fursa ya kuchaguliwa. kitendo cha kumpora jimbo dada huyu aliyepambana na vigingi vingi kwenye kampeni. alifanya kampeni kwa siku 70 non stop kafanya mikutano vijiji 80 kati ya 81 jimboni, kafika hata vijiji ambavyo viongozi wa wilaya na wagombea hawajawahi kufika,usafiri ni wa tazara tu, amepanda kiberenge ili kuvifikia vijiji hivyo,wananchi walimfurahia na kumpenda sana hadi ikatokea kibibi kizee kumpa fedha ya sh 500 kwa furaha ya kufika kwake. hakuangalia ulemavu wake alisonga mbele na amefanikiwa kufanya mikutano 130 wakati wa ccm haikuzidi hata 50. ni mlemavu wa viungo wa kwanza tz kusimama jimboni leo hii mnamuibia kura? wakati wananchi wamemchagua. JK huna moyo? huna huruma? huna ubinadamu kabisa nimekuchukia wewe na NEC, CCM na nimeapa neva in politics na nadhani huko hakuna haki na alaaniwe aliyeleta siasa. na waombeni wanaharakati mteteeni binti huyu wana kilombero wanamlilia. hivi hamna MUNGU? Si muwe mnawateua tu wabunge tujue moja.
 
PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,215
2,000
Napenda kutoa masikitiko yangu kwa CCM, JK na NEC kwa kitendo cha kinyama na ukiukwaji wa haki sawa kwa watu wenye ulemavu kupewa fursa ya kuchaguliwa. kitendo cha kumpora jimbo dada huyu aliyepambana na vigingi vingi kwenye kampeni. alifanya kampeni kwa siku 70 non stop kafanya mikutano vijiji 80 kati ya 81 jimboni, kafika hata vijiji ambavyo viongozi wa wilaya na wagombea hawajawahi kufika,usafiri ni wa tazara tu, amepanda kiberenge ili kuvifikia vijiji hivyo,wananchi walimfurahia na kumpenda sana hadi ikatokea kibibi kizee kumpa fedha ya sh 500 kwa furaha ya kufika kwake. hakuangalia ulemavu wake alisonga mbele na amefanikiwa kufanya mikutano 130 wakati wa ccm haikuzidi hata 50. ni mlemavu wa viungo wa kwanza tz kusimama jimboni leo hii mnamuibia kura? wakati wananchi wamemchagua. JK huna moyo? huna huruma? huna ubinadamu kabisa nimekuchukia wewe na NEC, CCM na nimeapa neva in politics na nadhani huko hakuna haki na alaaniwe aliyeleta siasa. na waombeni wanaharakati mteteeni binti huyu wana kilombero wanamlilia. hivi hamna MUNGU?
Mleta mada naomba usiongezee maneno, hayo tu yamenifanya niachane na keyboard kwa dakika 8!
This is too much of thuggy and vandalism actions...Halafu sikujua kuwa dadaRegia ni Mlemavu!
Kitendo cha kuthubutu tu ni cha ujasiri mno, na alitakiwa asitiliwe vidole kwenye haki yake...
Lakini Mungu yupo, na yuko operational kila iitwayo sekunde!
 
kisu

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
882
250
Nchi imeoza. Hamna Haki. Lakini People Power Haitanyamaza mpaka kieleweke!!!
 
myhem

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
932
500
wakati sisi tunasema IN GOD WE TRUST! wenzetu CCM kichini chini wanasema IN DEVIL SATAN THEY TRUST!
ubinadamu ndani ya ccm ni msamiati.
MUNGU ATAMLIPIA DADA HUYU.
 
Mahesabu

JF-Expert Member
Jan 27, 2008
5,361
2,000
ASUBIRI NEXT 5 YEARS...ILI HAWA WEZI WA KURA TUWADHIBITI.....TUTAWASHIKA KWA MIKONO YETU NA NYAMA YAO TUTAILA.....WOMAN OF SUBSTANCE welcome jamvini tuibomoe cCm mtandaoni......!
 
Mwasi

JF-Expert Member
Feb 12, 2010
249
170
Ni kweli tupu Remmy, inauma sana. Hakuna maneno ya kuelezea. Siamini Tanzania tumefika hapa leo, haki haipo tena ni dhuluma tu.
 
Kishaju

Senior Member
Feb 23, 2008
105
225
Jamani kama inawezekana twawez kusaidia kupitisha michango ya kumsaidia na kuweza kuendesha kesi na pia twaweza kumsaidia aendelee kuwapitia watu wake kila wakati ili ajipange vizuri sana mwaka 2015. Jamani tufanye hivyo kwa yule ambaye yupo karibu naye amfikishie ujumbe na sisi tup tayari kutoa chochote tulicho nacho.
 
Chimunguru

JF-Expert Member
May 3, 2009
10,585
2,000
Ukweli una prevail always, tutawakamata tuu, mungu yupo pamoja nasi CCM Na JK wote wananuka Rushwa na wizi!!!
 
Chimunguru

JF-Expert Member
May 3, 2009
10,585
2,000
Jamani kama inawezekana twawez kusaidia kupitisha michango ya kumsaidia na kuweza kuendesha kesi na pia twaweza kumsaidia aendelee kuwapitia watu wake kila wakati ili ajipange vizuri sana mwaka 2015. Jamani tufanye hivyo kwa yule ambaye yupo karibu naye amfikishie ujumbe na sisi tup tayari kutoa chochote tulicho nacho.

imepita kwangu mkuu, hii itasaidia sana kuwashika hawa mafisadi wa demokrasia
 
Mpita Njia

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
7,004
2,000
Napenda kutoa masikitiko yangu kwa CCM, JK na NEC kwa kitendo cha kinyama na ukiukwaji wa haki sawa kwa watu wenye ulemavu kupewa fursa ya kuchaguliwa. kitendo cha kumpora jimbo dada huyu aliyepambana na vigingi vingi kwenye kampeni. alifanya kampeni kwa siku 70 non stop kafanya mikutano vijiji 80 kati ya 81 jimboni, kafika hata vijiji ambavyo viongozi wa wilaya na wagombea hawajawahi kufika,usafiri ni wa tazara tu, amepanda kiberenge ili kuvifikia vijiji hivyo,wananchi walimfurahia na kumpenda sana hadi ikatokea kibibi kizee kumpa fedha ya sh 500 kwa furaha ya kufika kwake. hakuangalia ulemavu wake alisonga mbele na amefanikiwa kufanya mikutano 130 wakati wa ccm haikuzidi hata 50. ni mlemavu wa viungo wa kwanza tz kusimama jimboni leo hii mnamuibia kura? wakati wananchi wamemchagua. JK huna moyo? huna huruma? huna ubinadamu kabisa nimekuchukia wewe na NEC, CCM na nimeapa neva in politics na nadhani huko hakuna haki na alaaniwe aliyeleta siasa. na waombeni wanaharakati mteteeni binti huyu wana kilombero wanamlilia. hivi hamna MUNGU? Si muwe mnawateua tu wabunge tujue moja.

Unanitoa machozi Remmy!
 
Kilasara

JF-Expert Member
Dec 21, 2008
578
0
Ni jambo la kusikitisha kweli kwamba CCM wakishirikiana na Tume ya Uchaguzi wamethubutu kuchakachua kura za wapiga kura wa jimbo la Kilombero ili kumnyima Regia Mtema ushindi.

Nimemfahamu Regia pale Makao Makuu ya Chadema. Ni msichana mlemavu wa viungo na analazimika kutumia magongo, lakini anaheshimu wazee kweli kweli. Alikwenda haraka haraka ofisini kunitafutia document niliyoomba; na ninavyoelewa alifanya kampeni yake vizuri sana ktk jimbo lake la Kilombero.

Mimi namshauri achambue kura zilizopigwa katika vituo vyote kama zilivyosainiwa na wakala wa vyama, na kubandikwa ktk board nje ya vituo. Kwa vile uchambuzi huu utathibitisha alishinda Mgombea wa CCM, basi aende Mahakamani. Ikithibitika alishinda, ama Mahakama Kuu inaweza kumtangaza ndie mshindi, au itatengua huo uchaguzi wa Mgombea wa CCM na kuamuru uchaguzi urudiwe.

Najua kuna gharama ktk kuendesha kesi kama hii. Lakini pia kuna wanasheria wenye huruma ambao wanaweza kujitolea kwa bei ndogo kusaidia watu kama Regia.

Pole sana Regia. Huu unyama wa hawa wang'ang'anizi wa madaraka utatufikisha mahala pabaya Tanzania.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Remmy

JF-Expert Member
Jun 9, 2009
4,708
2,000
mahesabu si swala la kusubiri 2015, ni kuidai haki ya wananchi kilombero sasa, kuna waliozimia, waliomlilia kwa kumkosa. watandelea kukosa umeme,kununua sukari kwa bei kali.
 
Sikonge

JF-Expert Member
Jan 19, 2008
11,540
2,000
Kijana wa Kigoma pia kashafungua kesi Mahakamani.

Tutabanana tu hadi kieleweke na hawa Mafisadi.

Regia nina imani JOPO zito la Wapenda haki watakubali kumtetea na tena BURE.

Inabidi tukemee UNYAMA huu uliofanywa kwa dada yetu na ukiongeza na ulemavu, duuu!!

Jamaa ni mikatili si kawaida na kweli hata mie nimechoka. Malipo hapahapa duniani.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom