Kuibadili gesi asilia kuwa petroli na dizeli kunaweza punguza gharama tunazotumia kuagiza mafuta kutoka nje

Meneja si kipindi hiki Nchemba akiwa mkuu wa Finance. Tozo nyingine unaweza kuta anajiimarisha empire yake next time ajichoree zile alama zake hadi kwenye majumba ya watu na nguzo za umeme!
Mm navyoona labda ndio mapato pekee yanayoweza kukusanywa kirahisi na serikali ndio maana bei zinaongezeka.
 
Kuibadili gesi asilia yetu kuwa mafuta ya petroli na dizeli kunaweza punguza gharama tunazotumia kuagiza mafuta hayo kutoka mataifa ya nje​

Ni hivi wakuu,

Gesi asilia imeundwa kwa kampoundi zinazoitwa methane (CH4). Kampaundi ziyo zina kaboni moja na hydrojeni nne.

Petroli imeundwa kwa kampoundi zenye kaboni kuanzia 6 hadi 12.

Dizeli imeundwa kwa kampaundi zenye kaboni kuanzia 12 hadi 20.

Mafuta ya taa yameundwa kwa kampaundi zenye kaboni kuanzia 9 mpaka 16.

Mafuta ya ndege yameundwa kwa kampaundi zenye kaboni kuanzia 9 mpaka 16.

Wakati wa kuibadili gesi asilia kuwa mafuta, hapo kinachofanyika ni kufanya miungano ya kikemikali kuzibadili hizo kampaundi za methane zenye kaboni moja zilizomo ndani ya gesi asilia kutupatia kampaundi zenye kaboni kuanzia sita hadi 20 na zaidi ambazo zinapatikana kwenye mafuta.

Kisha kinachofanyika baada ya hapo ni kufanya utenganisho wa kikemikali kupata petroli, dizeli, mafuta ya taa, LPG, na prodakti zingine.

Hatua ya kwanza gesi asilia inabidilishwa kuwa kaboni monoksaidi na hydrojeni gesi.

Hatua ya pili monoksaidi na hyrojeni ziaungana kutengeneza kampaundi zenye kaboni nyingi na hydrogeni nyingi.

Hatua ya tatu kampaundi zenye kaboni nyingi na hydrojeni zilizotengenezwa zinatenganishwa kutoa petroli, dizeli, mafuta ya taa, mafuta ya injini, nk.

Njia nyingine niya kutengeneza petroli moja kwa moja.

Hapa hatua ya kwanza gesi asilia inabadilishwa kuwa koboni monoksaidi na hydrojeni.

Hatua ya pili kaboni monoksaidi na hydrojeni zinaunganishwa kutengeneza methanol.

Hatua ya tatu methanol inabadilishwa kuwa petroli.

Hivi ndivyo wenzetu CHINA, SOUTH AFRICA, na mataifa mengine wanavyoibadilisha gesi asilia kutengeneza mafuta.

Hii ndio tunaita natural gas value chain to get valueble products. Au Natural Gas utilization.

Kwenye Tanzania Natural Gas Utilization Master Plan ya Wizara ya Nishati 2016 hadi 2045 hivi viwanda vyote vipo. Na hesabu zilishapigwa kilichobaki ni utekelezaji tu.
Kwa mujibu wa uelewa wangu mdogo wa Chemistry uko sahihi sana mkuu,shida inakuja kwamba hata kama huo mpango wanao kwenye makaratasi,utekelezaji unahitaji watanzania wenye fani husika ambao tunao ila KAZI NI KUTOKUWA TAYARI KWA MAMLAKA ZINAZOHUSIKA KUWASHIRIKISHA kwenye huo utekelezaji ! Hivyo mipango itaendelea kuwepo tu miaka nenda rudi .Ninawafahamu vijana kadhaa waliopata ufaulu mzuri sana miaka ile(Maarufu kama Tanzania one) ambao walipelekwa nje kusomea mafuta na gesi lakini waliporudi nchini waliambiwa nafasi za ajira kwao Zina watu tayari.Hivi sasa wameshaondoka baadhi wako Angola na nchini kadhaa walikobahatika kupata ajira kwenye makampuni ya kimataifa ya mafuta. Hatujapata kiongozi atakayethubutu kuja na mfumo tofauti ili kuleta mageuzi katika maendeleo ya nchi yetu. Mungu tusaidie.
 
Hili ni kweli kabisa mkuu. Tunahitaji watendaji wenye uthubutu.
 
Huu mradi ulishachunguzwa kiuchumi kuwa unafaida, ndio maana uliwekwa kwenye mpango wa serikali na mwekezaji alipatikana. Uwe unapitia mipango ya serikali.
Mradi uliowekwa kwenye mpango wa serikali ni LNG (Liquified Natural Gas) ambao kiwanda kitakuwa Lindi. Mradi wa kubadilisha gesi asilia kuwa mafuta sidhani kama upo katika mpango wa hivi karibuni.
Huyo mwekezaji aliyepatikana amefikia hatua ipi?
 
Kwa nini uhangaike kufanya reverse engineering wakati hiyo hiyo CNG inaweza kutumika kama nishati mbadala kuendesha injini ya gari..
Exactly, tena gharama za uendeshaji kwa umbali sawa gesi inakuwa nafuu.
Kinachotakiwa ni kuweka vituo vya kujazia gesi sambamba na vile vya mafuta, pia kupunguza gharama na kuondoa urasimu kwenye conversion ya magari kutumia gesi.
 
Tatizo kubwa la waafrika ni miradi yao yote kufanyika kwa kutumia wakandarasi wa nje kwa gharama kubwa na hivyo kuongeza umasikini badala ya kupunguza.
Mradi kama huo waweza kuongeza Bei ya mafuta.
Na wakati hata sisi tunaweza kufanya tena vizuri kwa gharama nafuu
 
Mradi uliowekwa kwenye mpango wa serikali ni LNG (Liquified Natural Gas) ambao kiwanda kitakuwa Lindi. Mradi wa kubadilisha gesi asilia kuwa mafuta sidhani kama upo katika mpango wa hivi karibuni.
Huyo mwekezaji aliyepatikana amefikia hatua ipi?
Hiyo LNG haitoenda kutatua tatizo la nishati nchini. Kwasababu lengo la mradi wa LNG ni kuisafirisha gesi nje ya nchi kwa meli. LNG ni means of transportation ya gesi kwa masoko yaliyo mbali ambayo hayawezi kufikiwa kwa bomba.
 
Kwa mujibu wa mr slow slow ile sio yetu ila sisi ni soko kwa mwenyewe.yaani tuliamua kukopa ili kumhakikishia soko mwenyewe.
 
Exactly, tena gharama za uendeshaji kwa umbali sawa gesi inakuwa nafuu.
Kinachotakiwa ni kuweka vituo vya kujazia gesi sambamba na vile vya mafuta, pia kupunguza gharama na kuondoa urasimu kwenye conversion ya magari kutumia gesi.
Tatizo uelewa ni shida, faida za kutumia mafuta unazijua lakini. Mafuta ni visible fuel kuyacontrol ni rahisi. Gesi ni invisible haionekani. Ndio maana hata kwenye kuyatafuta mafuta ardhini makampuni hufurahi sana yanapoyagundua. Gesi hugunduliwa kwa bahati mbaya tu wakati mafuta yanatafutwa.
 
Kuibadili gesi asilia kuwa petroli na dizeli kunaweza punguza gharama tunazotumia kuagiza mafuta kutoka nje
 
Kuibadili gesi asilia kuwa petroli na dizeli kunaweza punguza gharama tunazotumia kuagiza mafuta kutoka nje
 
Kuibadili gesi asilia kuwa petroli na dizeli kunaweza punguza gharama tunazotumia kuagiza mafuta kutoka nje
 
Tatizo uelewa ni shida, faida za kutumia mafuta unazijua lakini. Mafuta ni visible fuel kuyacontrol ni rahisi. Gesi ni invisible haionekani. Ndio maana hata kwenye kuyatafuta mafuta ardhini makampuni hufurahi sana yanapoyagundua. Gesi hugunduliwa kwa bahati mbaya tu wakati mafuta yanatafutwa.
Pamoja na uelewa wako, huna justifiable reasons za kubadilisha gesi asilia kuwa mafuta kwa Tanzania.
If wishes were horse, beggars could ride.
Baki na uelewa wako wa kubadili gesi iwe mafuta ili kupunguza gharama.
 
Wanaoelewa wameshaelewa. Ww tulia tu.
 
Back
Top Bottom