Kuiba umeme katika mazingira haya itakuwa kosa?

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Siku ya Jumamosi kaka yangukatika nyumba tunayoishi alikwenda kwa wakala wa Tanesco kama ilivyoorodheshwa na tangazo la shirika hilo na kununua umeme wa jumla ya uniti 35.

Akapewa karatasi yenye seti tatu za namba na akaziingiza kwenye mita kama ilivyoelekezwa. Cha ajabu ni kwamba baada ya kuingiza zile seti mbili za Change token, namba za malipo ya umeme ziligoma kuingia.

Tulijaribu jana kutwa na leo bila mafanikio na tumelala giza kuamkia leo na pia tutalala giza kuamkia kesho.

Tukawa tunajadili. Kaka yangu akasema, jee 'nikifanya maarifa kuunganisha miwaya ili kupata umeme itakuwa ni kosa la wizi wa umeme? Kwani si tumeshalipia umeme?'

Nikashindwa kumpatia jibu na ndiyo maana nimeliweka swali humu JF ili kupata jibu. Utaibaje huduma ambayo tayari umeshailipia?

Tanesco wenyewe wanasemaje?
 
Nadhani itakuwa ni kosa la jinai kufanya hivyo kwamba ingawa mmeshailipia hiyo huduma, lakini bado hamjaruhusiwa kuitumia kihalali.
 
lakini hili suala linaleta usumbufu kweli kweli... hata mimi yamenitokea hayohayo, lakini nimeamua leo nitakwenda pale tanesco makao makuu kuzungumza nao
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom