Kuiba kura, kuchakachua matokeo ya uchaguzi ni UHAINI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuiba kura, kuchakachua matokeo ya uchaguzi ni UHAINI

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by NguchiroTheElde, Oct 29, 2010.

 1. N

  NguchiroTheElde Member

  #1
  Oct 29, 2010
  Joined: Jun 13, 2010
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuiba kura, kuchakachua matokeo ya uchaguzi ni kitendo cha uhaini kwani ni sawa na kupindua serikali. Serikali halali inachaguliwa na wananchi halafu vibosile vichache vinakaa na kula njama na kuamua kucheza na hizo namba ili aliyeshindwa aonekane kashinda na aliyeshinda aonekane kashindwa. Hilo ni jaribio la kupindua serikali na likifanikiwa mapinduzi yatakuwa yamefanyika.

  Kwa hiyo wizi wa kura na kubadilisha matokeo ya chaguzi za wapiga kura ni kitendo cha uhaini na adhabu yake kwa Tanzania inaanzia kifungo cha muda mrefu hadi kifo. Hadi sasa wamekuwa wakilindwa na washirika wao na wanaofaidika na uhaini huo lakini siku tutakayowapata itabidi wajibu shutuma hizo za uhaini na wakihukumiwa kifo tutawanyonga - hata kama watakuwa wameshakufa.

  Oliver Cromwel wa Uingereza alipindua serikali lakini baada yake kufa walipata mwanya wa kumshitaki kwa uhaini na alihukumiwa kunyogwa. Kwa hiyo walifukua mifupa yake na kuinyonga! Kwani kufa ndiyo kukukwepeshe kunyongwa?
   
Loading...