Kuhusu Zika Na Taharuki Isiyo Ya Lazima..

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Ndugu zangu,

Nchi yetu imekumbwa na taharuki isiyo ya lazima yenye kutokana na matamshi yaliyokuja bila waliyoyataamka kuwa na umakini wa wanachokitamka.

Hili sasa limekuwa tatizo kubwa kwenye nchi yetu. Kuna wakati aliyekuwa RC wa Dar Es Salaam, Meck Sadick alishutumu sana media kwa kuchagiza taharuki ya Ebola kuingia nchini bila kuwauliza kwanza wenye authority ya kuthibitisha hilo.

Mengine katika nchi yanahusu Usalama wetu kama Taifa. Si ya kukurupuka tu. Athari na gharama za kukarabati kilichotamkwa kwa makosa ni kubwa sana na hususan makosa ya matamshi au taarifa yanapofanywa na walioaminiwa kuwa ni watalaam wakwemo wanahabari. Maana, umma unaamini sana watu hao.

Hili la Zika tayari demage imeshatokea. Serikali ijitahidi kwa kuweka channels rasmi za mawasiliano hususan kwenye masuala muhimu yenye kuhusu Wananchi na sensitive kama hili la afya ya jamii.

Ni hatua sahihi kabisa kwa muhusika mkuu kwenye kutoa taarifa iliyozuia taharuki kuwekwa kando. Alipaswa, kwa taratibu kufanya mawasiliano kwanza na Wizara yenye dhamana.

Ni ujinga kuamini, kuwa Serikali inaweza kunyamaza kimya kama kuna virusi vya maradhi yenye madhara kwa watu wake vimeingia nchini na watu wake wanaathirika. Hiyo haiwezi kuwa Serikali kwa maana ya Serikali.

Na katika dunia hii, ukweli taarifa za virusi vya maradhi kama Zika huzifikia taasisi kubwa za afya za dunia kama vile WHO na ECDC- European Centre For Desease Control. Zika ni global issue. Sasa unapotembelea wenbsite, mathalan ya ECDC ambayo wame-update juzi tu, http://ecdc.europa.eu/…/Zika-countries-with-transmission.as… na huoni taarifa mpya za nchi kama Tanzania kuwa na hatari ya virusi vya zika, unashangaa na kujiuliza, taharuki hii ya hapa Tanzania imechagizwa na nini?

Na ukweli, kama virusi vyovyote vya hatari vinaingia hapa nchini kwetu, Tanzania ni moja ya nchi za dunia, zenye uwezo mkubwa wa ku-mobilize watu wake katika kujipanga, kupambana na kudhibiti.

Badala ya kusambaza taharuki, tusambaze sasa ukweli ulio rasmi kitaifa na kimataifa, kuwa Nchi Yetu Ni Salama dhidi ya tishio la ZIKA.

Maggid Mjengwa,
0688 37 36 52 ( Whatsapp)
0754 678 252
Iringa.


http://ecdc.europa.eu/en/healthtopi...k/Pages/Zika-countries-with-transmission.aspx
 
image.jpeg
 
Tumwamini nani Kati ya Mwanasayansi na mpiga domo la siasa?

Ndo amesha ropoka hiyo siri mliyotaka kuficha na wenye Akili tumesha jua na tunachukua tahadhari dhidi ya Zika
 
Back
Top Bottom