Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,288
- 33,894
Kuna haja ya kutunga sheria ambayo itampa Rais uwezo wa kuteua watu kwenye nafasi mbali mbali za uteuzi, lakini uteuzi huo wa Rais ni lazima uthibitishwe na mamlaka nyingine (Bunge) na Rais asipewe nafasi ya kuwafukuza atakavyo badala yake viwekwe viwango vya kimaadili kisheria ambavyo watu hao wakivikiuka watakuwa wamejifukuzisha kazi.
Lakini pia kunaweza kuwa na mfumo ambao Kamati ya Bunge ya sekta husika inaweza kumhoji mteule wa Rais na kumshauri mteule husika kujiuzulu kwa kadri ya makosa yake. Lakini kama hakuna vigezo kunaleta mtafaruku wa kwa nini mteule huyu katenguliwa kwa kosa linaloonekana ni dogo wakati mteule mwingine anafanya kosa linaloonekana kubwa anaachwa.