Window7
JF-Expert Member
- Sep 17, 2013
- 4,098
- 3,038
Wakuu kuna taarifa nilizipata kwamba muda si mrefu serikali itaanza utaratibu wakutoa kipaumbele kwa wale waliopitia JKT kwenye ajira zake.
Kupitia ajira zilizotangazwa na TPA naweza kusema jambo hilo linaweza kua la kweli.
Mfumo uliotumika kupeleka watu JKT wa mujibu wa sheria haukuweza kuwapeleka wote wenye sifa za kujiunga na chuo kwa kisingizio kwamba serikali imekosa bajeti.. Sasa iweje kukosa bajeti kupeleka mtu JKT mwenye sifa kujiunga chuo kikuu leo uje umuambie bila cheti cha JKT hatapewa kipaumbele?
Kosa la mhitimu au la serikali kukosa bajeti kumpeleka huyu mwanafunzi JKT?
Serikali ifikirie upya jambo hili, huu ni ukatili mkubwa kwa wakati huu wa ajira za kiushindani.