Nyenyere
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 14,769
- 10,649
Wakuu heshima mbele. Hii ni post yangu ya kwanza kwenye hii forum. Nimekuwa nikisikia kitu kinachoitwa VIKOBA. Ni kama cooperation fulani hivi lakini siielewi vema. Kama kuna mdau anaufahamu na hiki kitu naomba anijuvye. Salute.
====================================================
Chimilemwiyega said
Mkuu siyo kweli kwamba VIKOBA ni kwa ajili ya wanakijiji tu, hata watu wa mijini aidha wafanyabiashara au waajiriwa wanaweza kuanzisha kikundi chao na kuanza kuweka fedha na baada ya muda mfupi mkakopeshana kwa mfumo wa VIKOBA.
Mfumo wake ni kwamba mnakuwa na kikundi cha watu 10 hadi 15 na kujiwekea kiwango cha HISA ambapo kila wiki mnakutana mara moja na kila mmoja ananunua HISA moja kwa mwezi mnakutana mara Nne. Kama HISA mnajipangia sh 25,000 kwahiyo kwa mwezi mtakuwa mmekusanya sh 25,000 mara 10 mara 4, mnaweza kuanza kukopeshana kwa zamu kama mtakavyo kubaliana nani waanze kukopa, na kukopa ni mara 3 ya HISA zako.
Na marejesho yanaanza baada ya mwezi mmoja, na mkopo unarejeshwa kwa miezi 3 hadi 6. wakati wa kurejesha na members wengine wanaweza kukopa na mzunguuko ukaendelea. Any way naweza kuwa siwezi kueleza vizuri ila ni kitu kizuri sana kwa uchumi. tena kwa watu wa mjini mnaweza kujianzishia kwa HISA kubwa zaidi na kunufaika kwa haraka kuliko wa vijijini ambao wanakuwa na hisa za sh elfu moja moja.
==================================================
Nyenyere said
Wakuu niliamua kufanya home work yangu. Baada ya kuingia mtaani nilibahatika kukutana na mama mmoja ambaye ni member wa VICOBA huko kigamboni. Yeye alinieleza kuwa VICOBA ya mwanzo kabisa ilianzia Ukonga mwaka 2002.
Maelezo ya Chimilemwiyega na sahihi kabisa isipokuwa tu kuna chombo ambacho kinavisimamia VICOBA kupata usajili na mikopo kutoka katika mabenki. Pia kinasaidia kuibua miradi mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya VICOBA husika. Mfano ni VICOBA aliko huyu mama imeundwa miezi mitatu tu iliyopota.
Lakini wakati wa kukutana wiki iliyopita hiyo taasisi inayowasimamia ikawaletea proposal ya kuendesha mradi wa uvuvi na kwamba boti nne zimepatikana ambazo watakuwa wanazilipia kadri wanavyozalisha. Alinipa mifano mingi tu ya mafanikio ya VICOBA kama pale Mwenge ambapo wamepatiwa coaster nne kama mradi. Wale wa Ukonga wanakamilisha ujenzi wa jengo la ghorofa nne kama kitega uchumi chao.
Nilichojifunza:
1. Kikundi kinaundwa na watu katiya 15 - 30.
2. Kila member ananunua HISA 1 mpaka 5 tu kila wiki
3. Bei ya hisa mnapanga wenyewe (wengi wanafanya 2000 - 3000)
4. Baada ya mfuko kutuna mnaanza kukopeshana kwa riba.
5. Wakati wote huo tayari taasisi inayosimamia VICOBA itawaletea miradi mbalimbali kadri wafadhili wanavyopatikana.
6. Mnachagua miradi ambayo mnaweza kuisimamia.
7. Baada ya kuweka vitega uchumi faida inayopatikana inagawanya kwa wanachama.
8. VICOBA HAIFI kwa vile inawekeza kwenye assets. Inarithishwa. Lengo ni kumilikisha wananchi assets.
9. VICOBA inapewa usajili kamili serikalini na akaunti ya kikundi na zile za wanachama zinasimamiwa na TWIGA BANCORP.
10.Itazame Vicoba kama long term investment. kadri unavyo kuza mtaji wako (Hisa) ndivyo unayopata gawio kubwa.
Bado naendelea kuchimba zaidi. Nafaha juhudi niweze kuwapata hawa jamaa wa Ukonga nipate kujifunza zaidi. Nitapost hapa kama mtakuwa interested.
Salute wakuu.