Kuhusu utaratibu Brigedia Jenerali na Kamishna Jenerali

nyumbamungu

JF-Expert Member
Mar 3, 2017
997
827
Ninaomba msaada kueleweshwa katika kutaja jina la Suleiman Mungiya Mzee, ambaye kwasasa ndio Kamishna Jenerali wa Magereza, aliyeapishwa na Mh Rais Dr John. P. Magufuli. Kabla ya kiapo alikuwa ni Brigedia Jenerali wa Jeshi la Wananchi Tanzania. Nitakuwa nimefanya kosa kuita Kamishna Jenerali wa Magereza, Brigedia Jenerali Suleiman Mzee?

Kabla ya kuapishwa kuna itifaki ilifanyika ambayo (kwangu ndio mara ya kwanza kuiona) Brigedia Jenerali Suleiman M. Mzee alibadilisha sare ya JWTZ na kuvaa sare ya JMT, swali langu ni Je! (siombei itokee.. ila kila nafsi itaonja mauti) ikitokea umauti ukamkuta akiwa bado ni Kamishna Jenerali wa Magereza, cheo cha Brigedia Jenerali ndio kitakuwa kimekoma?
 
Kamishna Jenerali ni cheo cha Uteuzi

Bregadier Generali ni cheo cha Muundo

Mf kuna RPCs ambao ni ACP, SACP na DCP

Mkuu wa Majeshi CDF ni cheo cha Uteuzi

Cheo cha Muundo anakuwa Generali

Mnadhimu Mkuu ni cheo cha uteuzi

Cheo cha muundo anaweza kuwa Luteni Generali

Umeelewa?

Mfano, Kamishna alietumbuliwa Kamishna Andengenye alikuwa na cheo cha Kamishna wa Jeshi la Polisi kabla ya kuletwa huku kwa Mkopo na alibaki na cheo chake cha Muundo akaongezewa cha Uteuzi cha Kamishna Generali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii nchi,Tunapenda sana kutajwa kwa vyeo vyetu,Kuanzia kwenye familia, Utasikia Baba Jesca, huyo baba Jesca anakuwa Mwalimu, unaongeza Mwalimu,anakuwa Diwani,anaongeza Mheshimiwa, anaongeza elimu anapata PHD ya mihogo, anakuwa Dokta, nk.

Mwisho wa siku nilikuwanachanganyikiwa na aliyewahi kuwa mkuu mkoa wa Shinyanga miakaya karibuni, ukitaka kutaja jvyeo vyake unaweza kutumia dakika, na tunavyopenda kupoteza muda kabla ya kutajaj ina, unapaswa kutaja vyeo vyake vyote: iikuwa hivi Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Dr Brigedia Jenerali.

Kwanini tusitaje: Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mabula Koboko, tukaendelea badalaya huu mtindo wa kutaja vyeomwanzomwisho
 
Alhaj, Sheikh, Doctor, Chief, Muadhaam, Sultwaan, Rais Yahya Jameer wa Niger

Hii ndio Africa
Hii nchi,Tunapenda sana kutajwa kwa vyeo vyetu,Kuanzia kwenye familia, Utasikia Baba Jesca, huyo baba Jesca anakuwa Mwalimu, unaongeza Mwalimu,anakuwa Diwani,anaongeza Mheshimiwa, anaongeza elimu anapata PHD ya mihogo, anakuwa Dokta, nk.

Mwisho wa siku nilikuwanachanganyikiwa na aliyewahi kuwa mkuu mkoa wa Shinyanga miakaya karibuni, ukitaka kutaja jvyeo vyake unaweza kutumia dakika, na tunavyopenda kupoteza muda kabla ya kutajaj ina, unapaswa kutaja vyeo vyake vyote: iikuwa hivi Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Dr Brigedia Jenerali....

Kwanini tusitaje: Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mabula Koboko, tukaendelea badalaya huu mtindo wa kutaja vyeomwanzomwisho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kamishna Jenerali ni cheo cha Uteuzi

Bregadier Generali ni cheo cha Muundo

Mf kuna RPCs ambao ni ACP, SACP na DCP

Mkuu wa Majeshi CDF ni cheo cha Uteuzi

Cheo cha Muundo anakuwa Generali

Mnadhimu Mkuu ni cheo cha Muundo

Cheo cha Uteuzi anaweza kuwa Luteni Generali

Umeelewa?

Mfano, Kamishna alietumbuliwa Kamishna Andengenye alikuwa na cheo cha Kamishna wa Jeshi la Polisi kabla ya kuletwa huku kwa Mkopo na alibaki na cheo chake cha Muundo akaongezewa cha Uteuzi cha Kamishna Generali

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante Kamanda lakini chenye mpunga wa kutosha bila shaka ni cha uteuzi
 
Nyerere ndo alikuwa Baba...hakuwa na Mambo mengi badala ya kutaja Mh Rais Baba Taifa mwalimu Kambarage Nyerere.

Unataja tu Mwalimu Nyerere na anaitika tunasonga.

Kujimwambafai kumeanza awamu ya nne awamu ya tano imezidi watu wanataka kuabudiwa sana.
Dr.Pombe John Joseph Magufuli Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tz..usipotaja hivyo unajiandaa kutumbuliwa.

Wenzetu wa Marekani wametuzid sana
Obama ana PhD,Clinton ana PhD,Ben Carson wana PhD,nadhani na Trump ana PhD lakni usomi wao sio status kubwa ila ukimuita tu Rais Trump anaitika.
 
Ninaomba msaada kueleweshwa katika kutaja jina la Suleiman Mungiya Mzee, ambaye kwasasa ndio Kamishna Jenerali wa Magereza, aliyeapishwa na Mh Rais Dr John. P. Magufuli. Kabla ya kiapo alikuwa ni Brigedia Jenerali wa Jeshi la Wananchi Tanzania. Nitakuwa nimefanya kosa kuita Kamishna Jenerali wa Magereza, Brigedia Jenerali Suleiman Mzee?

Kabla ya kuapishwa kuna itifaki ilifanyika ambayo (kwangu ndio mara ya kwanza kuiona) Brigedia Jenerali Suleiman M. Mzee alibadilisha sare ya JWTZ na kuvaa sare ya JMT, swali langu ni Je! (siombei itokee.. ila kila nafsi itaonja mauti) ikitokea umauti ukamkuta akiwa bado ni Kamishna Jenerali wa Magereza, cheo cha Brigedia Jenerali ndio kitakuwa kimekoma?
Sasa mnaanza kumuelewa Rpc Shana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika tukio la kifo lililotokea majuzi kule Arusha likimuhusisha mwanamke(marehemu)na askari wa JWTZ. Wakati RPC wa Arusha anaongea na waandishi wa habari alitoa kauli ambayo alisema kuwa ktk vyeo vya JWTZ anayemzidi kwa cheo ni Brigedia Jenerali kwenda juu!! Najiuliza ulinganifu huu amezingatia vigezo/muongozo upi?! RPC yeye ni Assistant Commissioner of Police(ACP).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyerere ndo alikuwa Baba...hakuwa na Mambo mengi badala ya kutaja Mh Rais Baba Taifa mwalimu Kambarage Nyerere.

Unataja tu Mwalimu Nyerere na anaitika tunasonga.

Kujimwambafai kumeanza awamu ya nne awamu ya tano imezidi watu wanataka kuabudiwa sana.
Dr.Pombe John Joseph Magufuli Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tz..usipotaja hivyo unajiandaa kutumbuliwa.

Wenzetu wa Marekani wametuzid sana
Obama ana PhD,Clinton ana PhD,Ben Carson wana PhD,nadhani na Trump ana PhD lakni usomi wao sio status kubwa ila ukimuita tu Rais Trump anaitika.
Wanaitwaga tu Mr President (Bwana Rais) na anajiskia fahari sana.
 
Yote hayo yanatokea Tanzania tu watu kulingia vyeo watunukiwavyo kiholela na wasiojua wanaostahili hizo nafasi, ila deep inside they don't know what it takes for real man to be honored in that position.
Promotion is not in uniform but what you have gone through to be honored.

Police hawezi leta mageuzi nchini..
Magereza hawezi leta mageuzi nchini..
Afisa usalama hawezi leta mageuzi nchini...
Ila mwanajeshi anaweza leta mageuzi nchi yoyote ile iwe ya kifalme, yakidemokrasia, ya kidikteta
All respect to soldiers who serve their countries in true heart...
 
Kamishna Jenerali ni cheo cha Uteuzi

Bregadier Generali ni cheo cha Muundo

Mf kuna RPCs ambao ni ACP, SACP na DCP

Mkuu wa Majeshi CDF ni cheo cha Uteuzi

Cheo cha Muundo anakuwa Generali

Mnadhimu Mkuu ni cheo cha uteuzi

Cheo cha muundo anaweza kuwa Luteni Generali

Umeelewa?

Mfano, Kamishna alietumbuliwa Kamishna Andengenye alikuwa na cheo cha Kamishna wa Jeshi la Polisi kabla ya kuletwa huku kwa Mkopo na alibaki na cheo chake cha Muundo akaongezewa cha Uteuzi cha Kamishna Generali

Sent using Jamii Forums mobile app
@Pohamba uko deep sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya mambo mengine Ya jenerali ua kamishnia hata siyajui.
Naomba tu kujua vipi ulaji utakuwa umepungua au kuongezeka?
Safi kabisa. Hapa Duniani sisi tulikuja kwa kazi moja tu kula! Mtu aanze tena kutletea sijui stori za SGR au Rufiji Hydropower, yanatuhusu nini sisi? Sisi tulikuja kula!
 
Katika tukio la kifo lililotokea majuzi kule Arusha likimuhusisha mwanamke(marehemu)na askari wa JWTZ. Wakati RPC wa Arusha anaongea na waandishi wa habari alitoa kauli ambayo alisema kuwa ktk vyeo vya JWTZ anayemzidi kwa cheo ni Brigedia Jenerali kwenda juu!! Najiuliza ulinganifu huu amezingatia vigezo/muongozo upi?! RPC yeye ni Assistant Commissioner of Police(ACP).

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo hajitambui,JWTZ maafisa wake wanaanza kupewa kamisheni(commissioned officer) kuanzia nyota moja(Luteni Usu).Kwa idara zingine kama Polisi,Magereza,Uhamiaji na Zimamoto wanaanzia nyota tatu (mrakibu msaidizi wa polisi au kwa kifupi ASP katika lugha ya kiingereza).Wenye kamisheni wote wanawajibika kwa Rais moja kwa moja.

Ulinganifu ni huu kwa maafisa wenye kamisheni(wanaowajibika kwa rais):
JWTZ Vs. POLISI
Jenerali(Gen). - -----------(neal)

Luteni jenerali. - ------(neeal)
Meja jenerali. - IGP(mkuu wa polisi)
Bregadia jen. - Kamishina wa polisi

Kanali(col). - Naibu kamishina(DCP)

Luteni kanali - kamishina msaidizi mwandamizi(SACP).
Meja - Kamishina msaidizi (ACP).

Kapteni - Mrakibu mwandamizi(SSP)
Luteni. - Mrakibu wa polisi(SP)
Luteni usu - Mrakibu msaidizi (ASP)

NB:
Maafisa wenye kamisheni katika JWTZ wananzia nyota moja(luteni usu),na polisi,magereza,uhamiaji na zimamoto ni kuanzia nyota ya tatu(ASP au ASI Kwa uhamiaji na ASF kwa zimamoto).

Kwa hiyo hao ndio maofisa wanaowajibika kwa rais na viapo vyao viko tofauti na askari wengine.
 
Back
Top Bottom