Kuhusu Utanganyika: Shetani Unayemjua ni Bora Kuliko Malaika Usiyemjua!

LordJustice1

JF-Expert Member
Jan 19, 2011
2,263
530
Wakuu,
Watanzania wengi wamezaliwa baada ya Aprili 26, 1964 kwa hiyo hawaijui Tanganyika, wanasoma tu kwenye makabrasha. Kama hiyo si sahihi sasa basi Watanganyika walioishi Tanganyika huru iliyodumu kwa miaka takriban 4 (1961-1964) wanaijua vizuri Tanzania kuliko Tanganyika iliyodumu muda mfupi!
Afterall, wanaoidai Tanganyika hawajui kwamba kuna Tanganyika za aina kadhaa:
1. Tanganyika ya kabla ya Mjerumani ambayo haikuwa na mipaka (Pre-1884),
2. Tanganyika ya Mjerumani ambayo ilikuwa na mipaka iliyojumuisha Rwanda na Burundi (1884-1919),
3. Tanganyika ya Mwingereza ambayo haijumuishi Rwanda na Burundi (1919-1961),
4. Tanganyika ya Nyerere ambayo ilidumu kwa muda mfupi (1961-1964),

Kwa hiyo wanaoipigania "Tanganyika" ni ipi hasa na kwa nini? Hiyo Tanganyika mpya ina siri gani ambayo itatukwamua kwenye lindi la umaskini? Sio tukiipata hiyo "Tanganyika mpya" tutakuta ufisadi bado unatutafuna kisawasawa kama kawaida? Hivi Watz tumekosa kabisa viongozi wa kutusaidia kujua matatizo ya kweli ya nchi yetu na kuyamaliza "once and for all" badala ya kutuletea "mvinyo wa zamani ndani ya chupa mpya" huku tukiacha matatizo halisi ya ufisadi, wizi, mikataba mibovu, ahadi hewa, udini, kututafuna?

Si afadhali kuendelea na shetani tunayemfahamu (Tanzania) kuliko kung'ang'ania malaika (Tanganyika) tusiyemfahamu? Maana tumeonjeshwa na WANAUAMSHO kwamba tatizo ni nyumba za Ibada, si Muungano!

Tukiwasikiliza hawa jamaa tutacheza ngoma tusyoijua, tutahenyeshwa kisawasawa kama Wakenya wanavyohenyeshwa na Al-Shabaab! Mambo haya yaluanza kama mchezo kama yanavyoendelea kwenye Utawala wa JK na bahati mbaya kuna mkono wa Serikali kwenye vuguvugu ya Uamsho! Sasa hivi wamehamia kwa Dr Ndalichako, Sensa, nk. Kesho utasikia mengine mengi! Tuiache Tanzania yetu kama ilivyo, tu-focus kwenye "real issues!!"
Nawasilisha!!
 
Shida ya "watanganyika" siyo "Tanganyika" kimsingi maana hurka ya watu wa bara ni wamoja zaidi kuliko hao wapiga mayowe. Bali shida ya " watanganyika" ni KUCHOSHWA NA KELELE ZISIZOISHA NA ZISIZO MANTIKI ISIPOKUWA UDINI TU! Bahati mbaya kwa wabara hawa viongozi wa serikali zote mbili ama ni ndumilakuwili, ama ni mazezeta ama hawana meno na matokeo yake wamechochea kwa namna nyingi uhasama huu wa udini.

Kwa kifupi hoja ya watanganyika ni kiitikio cha wimbo wa wazenji chenye maana hizi:
1. To let Zanzibar go kwa maana ya kuchoshwa na makelele yasiyoisha ya wazenji ili (watanganyika) watumie muda vizuri kuzungumza habari za maendeleo na siyo ujinga tu kila kukicha. .
2. To root away the seed of hate and conflict kwa maana kuwa upumbavu huu sasa umeanza kutudhuru tukizingatia kuwa nchi haina serikali kwa sasa.
 
Tatizo lako (sio la "Watanganyika" kama unavyodai) unafikiri mambo yataenda smooth na tutaishi raha mustarehe tuki-"let Zanzibar go!" Umesahau kwamba au hujui kwamba Wana-Uamsho ni watu wanaotumiwa na Waarabu wanaoumezea mate ukanda wa Afrika Mashariki (including DSM, Tanga, Mombasa, nk)! Sasa unapodai "to let Zanzibar go" you don't know the move behind the curtain, unafikiri kuwa ni "Movement ya Kisiasa" kumbe ni "ya Kidini!" Umefika wakati wa kuona mbele zaidi ya pua yako!
 
Nani unayemtaka aongelee hiyo Tanganyika ya kabla ya Mjerumani (German East Africa?)

hakukuwa na hiyo German East Africa. Baada ya Berlin Conference kulikuwa na Deutsche Ost Africa iliyojumuisha Tanganyika Rwanda na Burundi!
 
Hata pamoja na yote hayo kauli uliyoitumia ktk title siyo njema fanya kuiondoa
 
Suala hapa siyo kuvunja muungano wala kuidai Tanganyika.Hiyo Tanganyika itakuwa chini ya nani? Mara kadhaa kumekuwa na maneno kuwa wakristo bara ni wengi zaidi kuliko waislamu,sasa vp tena hiyo Tanganyika kwa upande wenye waislamu wengi watakapoleta madai ya kuanzisha mikoa maalum ya kiislam? Hivyo suala la udini siyo la Tanganyika na Zanzibar bali hata ndani ya Tanganyika litakuwepo. Mtazamo wa kuita ni kelele madai ya wazenj ni UTOVU NI NIDHAMU.Nchi hii ikigawanyika kipuuzi-kipuuzi tu nasi tukawa tunachukulia kawaida iko siku tutaukumbuka wakati huu muhimu,ambao tunaweza kukaa na kujadiliana kwa amani juu ya Muungano.Mkisema tatizo ni udini na zenj ikabainishwa kuwa ni nchi ya kiislam then,waislam walioko bara mtawataka waende Zanzibar? Kiini cha tatizo siyo udini tu bali pia UTAWALA ULIOCHOKA WA CCM.Badala ya kuweka mambo wazi ili wananchi wajadili namna ya kuuboresha muungano wao wakaunda cjui tume ya kushughulikia kero za muungano then muungano ukatafsiriwa kuwa KERO.
 
hoja yako ni hoja mfu kabisa; kuna kasoro nyingi za muungano ambazo mimi niliyezaliwa miaka ya sabini ninaziona na siwezi kuwa **** kwa kukumbatia makosa ya babu zangu. Waulize Sudan kusini waliozaliwa katika Sudan moja ni kwa nini waliamua kujiondoa, kisha uje tena na hoja yenye maana. Bora malaika nisiyemjua kwa kuwa siku zote malaika ni mwema, kulikoni shetani yoyote. Wewe na mashetani wenzakomnaopendelea muungano kwendeni zenu. Wana uamsho z'bar wana matatizo yao pamoja na njaa lakini sisi watanganyika una hoja za msingi kuidai Tanganyika yetu.
 
Inafuatana unamsema malaika yupi? 1? Mungu au wa shetani? Kama ni wa Mungu hata usipomjua ni bora kuliko shetani!
 
Tatizo lako (sio la "Watanganyika" kama unavyodai) unafikiri mambo yataenda smooth na tutaishi raha mustarehe tuki-"let Zanzibar go!" Umesahau kwamba au hujui kwamba Wana-Uamsho ni watu wanaotumiwa na Waarabu wanaoumezea mate ukanda wa Afrika Mashariki (including DSM, Tanga, Mombasa, nk)! Sasa unapodai "to let Zanzibar go" you don't know the move behind the curtain, unafikiri kuwa ni "Movement ya Kisiasa" kumbe ni "ya Kidini!" Umefika wakati wa kuona mbele zaidi ya pua yako!

Mkuu, kwa kawaida ukianzisha mada basi unajivika jukumu la kuratibu mjadala in a fair and objective manner. Kama mwanzishaji mada na kwa hiyo mwendeshaji majadiliano hukupashwa kuwa wa kwanza kurusha kauli za kashfa kwa wachangiaji. Hapo pekundu pamekutambulisha kama ifuatavyo:
  1. Una tabia ya udictator na unadhani uonavyo wewe basi ndiyo ukweli. Who are you hata ujidhani kuwa mtazamo wako ndiyo bora kuliko wa wengine?
  2. Wewe yumkini ni tunda na sehemu ya uozo ambao watanzania tunataka sasa kuuondoa. Mwenye akili timamu katu hawezi kukubaliana na kichwa cha habari ulivyokiweka: "Kuhusu Utanganyika: Shetani Unayemjua ni Bora Kuliko Malaika Usiyemjua!" Katika hili shetani ni nani na malaika ni nani? Unataka kusema kwa kuwa chama fulani (kwa mfano) ndo kimetawala miaka mingi hata kama kimepoteza dira na watu wanaona nchi inaenda vibaya tukiache kitawale milele kwa sababu ndiyo shetani tunayemjua? Infalibility ya muungno wa namna hii imeletwa na malaika yupi?

Kama niliyoandika juu yako hapo juu hayakuhusu basi napata mashaka sana kama wewe kweli ni mtanzania na unayeishi ndani ya mipaka ya nchi hii.
 
Kama umeshindwa kuuongelea Utanganyika kabla ya Mjerumani, jee, unaweza kutueleza maana ya Tanganyika? na jinaTanganyika limetoka wapi? kwani Tanzania tunajuwa ni Muhindi wa Tanga aliyetowa hilo jina. Tanganyika jee?
 
Tatizo lako (sio la "Watanganyika" kama unavyodai) unafikiri mambo yataenda smooth na tutaishi raha mustarehe tuki-"let Zanzibar go!" Umesahau kwamba au hujui kwamba Wana-Uamsho ni watu wanaotumiwa na Waarabu wanaoumezea mate ukanda wa Afrika Mashariki (including DSM, Tanga, Mombasa, nk)! Sasa unapodai "to let Zanzibar go" you don't know the move behind the curtain, unafikiri kuwa ni "Movement ya Kisiasa" kumbe ni "ya Kidini!" Umefika wakati wa kuona mbele zaidi ya pua yako!

kwani kanisa linatumiwa na nani ?? waafrika ??? kwani uarabu ni udini ??

wrong thought !!!wrong idea !!! wrong time!!! wrong place!!!
 
Yakhee inaposemwa Tanganyika ni hii Tanganyika tuliopatia Uhuru ya TANU na inaposemwa Zanzibar ni ileile waliyopata Uhuru ,maana kama utaihitaji hizo zingine basi mikoa ya Pwani yote itaenda Zanzibar ,angalia ukienda Mahakamani usije ukasema unaidai tanganyika ya Mjeru ,tutapoteza ukanda wapwani kwa kilomita kibao.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom