Kuhusu umbali wa gari uliosafiri

Betason

JF-Expert Member
Feb 2, 2015
352
585
Wadau msaada wenu hapa unahitajika

Ni hivi...huwa najiuliza kuhusu umbali gari uliosafiri (km) unahusiana vipi na uimara wake?

Je ni lazima gari iliyosafiri umbali mrefu kuwa sio imara ama inategemea na huo umbali ni wapi imesafiri

swali la mwisho...unamshaurije mtu anaetaka kununua gari kuhusu umbali gari iliosafiri, maana unaweza pata gari nzuri economical lakini ishu ni km zipo juu

nawasilisha
 
Watu wamekariri kuhusu hio kitu. Gari kutembea km nyingi haina maana ni mbovu kuliko iliotembea pungufu. Kuna gari zimetembea 200,000 ndani ya miaka mitano au pungufu lakini ukiiona na uiendesha haina tofauti na mpya. Hizi huwa zinakuwa gari za kampuni[huko japana/US/Europe] ambazo huwa zinatembea highway sana kutoka mji hadi mji kila siku.

Kuna watu wanaishi na kufanya kazi km mpaka 100 na anaenda na kurudi kila siku na gari na anatrip nyingine. Lakini gari kama hii inakuwa maintained na dealer na baada ya miaka mitatu au mitani inauzwa ikiwa na km nyingi sana lakini kwenye hali nzuri sana. Kikubwa ni maintance tu wala sio odometer inaonesha nini.

Gari yenye km 200,000 za highway ni bora kuliko gari yenye km 100,000 inayotumika mjini kila siku.
 
Back
Top Bottom