Kuhusu Tatizo la Uchafu Dar, Madrassatul Abraar tuna wazo litakalokuwa suluhu ya kudumu

Abdul Ghafur

JF-Expert Member
Sep 18, 2017
610
733
Naomba kwanza tumsikilize Mkuu wa Mkoa.

1624007177168.png

Video clips zinachelewa kupanda lakini In shaa Allah tutazipandisha, ni muda tu.

Baada ya kumsikiliza mkuu wa mkoa na tatizo la uchafu na biashara kuwa kiholela mitaa ya Dar. AlhamduliLllah Madrassatul Abaraar darasa la vifaa vya ujenzi tumekuja na suluhisho la kipekee, la kudumu, na lisilo na gharama kubwa na kutakuwa na mvuto wa kipekee kwenye jiji la Dar na sehemu yoyote vitapotumika Abraar Kiosk.

Abraar maana yake ni Waja wema. Na ndio jina la tulivyovipa vinbanda vyetu kwa kuwa Mkuu wa Mkoa kaongea kwa hisia kubwa sana, hauna shaka kabisa kuwa Mkuu wa Mkoa ni Mja mwema na anaendana kabisa na fikra za waja wema. Kwani tunaamini kuwa usafi ni imani, asie na imani hafikirii usafi na asiye na imani hawi Mja Mwema aka Abraar.

Kuanzia viosk, vibanda vya walinzi wa usiku madukani, vibanda vya mawakala wa kampuni za simu, vinabda vya mawakala wa banks, vibanda vya ATM, vibanda vya wauza soda na juisi, vibanda vya vinyozi, vinabda vya sokoni. Mapipa ya taka ya kudumu. Vibanda vya matangazo ya biashara, vibanda vya stand za mabasi, vibanda vya stand za dala dala. Ni bidhaa ya ubunifu wa hali ya juu.

Vibanda vitatengenezwa kwa aina ya msonge (mduara) wa zege linalohamishika na hakuna sehemu au pahala ambapo havitahitajika. Kuanzia vibanda vya walinzi wa Mabenki, Maduka ya Fedha, Vituo vya mafuta. Vibanda vinaweza kuwa na ghorofa moja, juu na chini na vikahamishika kwa urahisi, vyote vitakuwa ni vya kuunganisha kiurahisi tu.

Havihitaji ufundi wa hali ya juu, vimeshapimwa mzunguko wa mduara kutoka vinapoundwa darasani kwetu. Ni kupanda tu zege letu kavu, hakuna kukosea vipimo kwani tayari tumeshavipima na aneviweka anavipachika tu.

Pia tumebuni aina kadhaa za kuviezeka kwa urahisi na kwa mvutio wa kipekee.

Vifaa hivyo vyote vinatengenezwa kwa asilimia zaidi ya 60 na akina mama, asilimia iliyobaki ni vijana wetu wanojifunza ujenzi hapa Madrassatul Abraar.

Vifaa hivyo kwa mzunguko mdogo (diameter ndogo) vinaweza kuwa mapipa ya kuudu ya taka, hakuna kuibiwa wala kuharibika na vinaweza kuwa maitained hapo hapo vilipo vikawa vinapendeza daima. Maisha ya Abraar Kiosk au Abraar Pipa vikiwa kazini ni miaka 50 mpaka 100 na vinahamishika ki wepesi bila hasara yoyote ya kuvibomoa itapohitajika kuhamishika kupisha maendeleo.

Kwa wawekezzaji wa kibiashara ni fursa hiyo kuleta mitaji yenu tuvizalishe kwa wingi gharama zipungue nanyi mpate faida mkiviuza. Vinaweza kutumika Tanzania nzima, si lazima iwe Dar Pekee.

Tumeshaanza kuviunda vya sample na kabla hatujavimaliza kuna mama lishe hapa Madrassatul Abraar kishaanza kukitumia, anasema yeye hangoji kiishe.

Wasiliana na Mzee Abdul Ghafur kwa maelezo zaidi 0625249605
 
Attachments

  • WhatsApp Video 2021-06-17 at 18.08.40.mp4
    17.3 MB
Tangu nimefika mbeya najiuliza Nani alifanya mbeya kuwa safi bila machinga wengi kama sehemu zingine? Kama ndo huyo mkuu wa mkoa dar mpya basi hongera zangu azipokee kweli ni kazi nzuri sana.
 
Ila sasa nina swali kuhusu hayo mapipa ya uchafu kama yanafaa kwa matumizi ya nyumbani na kuchomea uchafu ukikaribia kujaa?
 
Naomba kwanza tumsikilize Mkuu wa Mkoa.

View attachment 1822533

Video clips zinachelewa kupanda lakini In shaa Allah tutazipandisha, ni muda tu.

Baada ya kumsikiliza mkuu wa mkoa na tatizo la uchafu na biashara kuwa kiholela mitaa ya Dar. AlhamduliLllah Madrassatul Abaraar darasa la vifaa vya ujenzi tumekuja na suluhisho la kipekee, la kudumu, na lisilo na gharama kubwa na kutakuwa na mvuto wa kipekee kwenye jiji la Dar na sehemu yoyote vitapotumika Abraar Kiosk. Abraar maana yake ni Waja wema. Na ndio jina la tulivyovipa vinbanda vyetu kwa kuwa Mkuu wa Mkoa kaongea kwa hisia kubwa sana, hauna shaka kabisa kuwa Mkuu wa Mkoa ni Mja mwema na anaendana kabisa na fikra za waja wema. Kwani tunaamini kuwa usafi ni imani, asie na imani hafikirii usafi na asiye na imani hawi Mja Mwema aka Abraar.

Kuanzia viosk, vibanda vya walinzi wa usiku madukani, vibanda vya mawakala wa kampuni za simu, vinabda vya mawakala wa banks, vibanda vya ATM, vibanda vya wauza soda na juisi, vibanda vya vinyozi, vinabda vya sokoni. Mapipa ya taka ya kudumu. Vibanda vya matangazo ya biashara, vibanda vya stand za mabasi, vibanda vya stand za dala dala. Ni bidhaa ya ubunifu wa hali ya juu.

Vibanda vitatengenezwa kwa aina ya msonge (mduara) wa zege linalohamishika na hakuna sehemu au pahala ambapo havitahitajika. Kuanzia vibanda vya walinzi wa Mabenki, Maduka ya Fedha, Vituo vya mafuta. Vibanda vinaweza kuwa na ghorofa moja, juu na chini na vikahamishika kwa urahisi, vyote vitakuwa ni vya kuunganisha kiurahisi tu. Havihitaji ufundi wa hali ya juu, vimeshapimwa mzunguko wa mduara kutoka vinapoundwa darasani kwetu. Ni kupanda tu zege letu kavu, hakuna kukosea vipimo kwani tayari tumeshavipima na aneviweka anavipachika tu.

Pia tumebuni aina kadhaa za kuviezeka kwa urahisi na kwa mvutio wa kipekee.

Vifaa hivyo vyote vinatengenezwa kwa asilimia zaidi ya 60 na akina mama, asilimia iliyobaki ni vijana wetu wanojifunza ujenzi hapa Madrassatul Abraar.

Vifaa hivyo kwa mzunguko mdogo (diameter ndogo) vinaweza kuwa mapipa ya kuudu ya taka, hakuna kuibiwa wala kuharibika na vinaweza kuwa maitained hapo hapo vilipo vikawa vinapendeza daima. Maisha ya Abraar Kiosk au Abraar Pipa vikiwa kazini ni miaka 50 mpaka 100 na vinahamishika ki wepesi bila hasara yoyote ya kuvibomoa itapohitajika kuhamishika kupisha maendeleo.

Kwa wawekezzaji wa kibiashara ni fursa hiyo kuleta mitaji yenu tuvizalishe kwa wingi gharama zipungue nanyi mpate faida mkiviuza. Vinaweza kutumika Tanzania nzima, si lazima iwe Dar Pekee.

Tumeshaanza kuviunda vya sample na kabla hatujavimaliza kuna mama lishe hapa Madrassatul Abraar kishaanza kukitumia, anasema yeye hangoji kiishe.

Wasiliana na Mzee Abdul Ghafur kwa maelezo zaidi 0625249605
Ma shaa Allah, wazee wetu wa Madrassa huu ni mfano wa kuigwa. Sasa wakurugenzi wa Jiji la Dar washindwe wenyewe.

Tunasubiri graphics,
 
Bila picha ni kama umeandika mashudu tu, tunashindwa kufanya ulinganifu yakinifu kwa ulichoandika
Wewe ndio wale wa kuitikia chorus, mmoja kaanza "bila picha, jinsi usivyo na fikra na wewe ukakaurupuka. Kilichoandikwa umekisoma?
 
Tangazo gani halina picha watu wakaona unachokiongea?
Picha ya nini sasa?

Walikwambia ni tangazo hilo? Watu wanajibu hoja za usafi na maingira kwa ubunifu, nyie mmekazana picha, poicha. Picha wewe itakusaidia nini? Hujui kusoma?
 
Zinakuja usiwe na shaka. Tulishaweka indhari hapo juu na tukasema tunataka vijana wa graphics wajitokeze.
Abdul, achana nao hao wasikusumbue. Wakitaka picha wakufate vilipo waje wao kuvipiga picha.

Wana roho mbaya tu, hhawaamini wanachokisoma.

Keep it up, Mzee wa Madrassa Abrar.
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom