Kuhusu Shibuda CHADEMA inastahili pongezi

mwinukai

JF-Expert Member
May 3, 2011
1,447
630
Toka apite na kuwa mbunge wa Maswa Mashariki Shibuda alionekana wazi kutaka mgogoro na viongozi wa CHADEMA, kwa busara na hekima walizonazo viongozi wachadema hawakujiingiza katika mtego huu dhaifu wa SHIBUDA.

Kauli alizokuwa akitoa dhidi ya CHADEMA, viongozi wa CHADEMA walichukulia kama ni kauli toka kwa mwendawazimu ambazo hazipaswi kujibiwa na sasa SHIBUDA amenasa katika mtego dhaifu aliojitegea mwenyewe, Na sasa kila mtu mwenye akili timamu anajua kuwa SHIBUDA si mwana CHADEMA.

Hivyo halali yake kufukuzwa, watanzani nao wanachukulia maneno ya shibuda kama hoja za mwendawazimu ambazo si busara na hekima kuzijadili.

viongozi wa CHADEMA wanastahili pongezi kwa jinsi walivyokabiliana naye mpaka ananasa kirahisi katika mtego wake, japo kuwa MPENDAZOE alishatahadharisha hili hata kabla ya uchaguzi wa mwaka 2010 akapuuzwa.

 
Nami nimeliona hili. Viongozi wa CDM waendelee kumpuuza Shibuda kwa sababu nasikia huwa ni mwendawazimu wa kufungwa kamba kabisa. Hakuna haja ya kuingia kwenye mgogoro na mwehu.
 
[FONT=times new
roman]Toka apite na kuwa mbunge wa Maswa Mashariki Shibuda
alionekana wazi kutaka mgogoro na viongozi wa CHADEMA, kwa busara na
hekima walizonazo viongozi wachadema hawakujiingiza katika mtego huu
dhaifu wa SHIBUDA, Kauli alizokuwa akitoa dhidi ya CHADEMA, viongozi wa
CHADEMA walichukulia kama ni kauli toka kwa mwendawazimu ambazo
hazipaswi kujibiwa na sasa SHIBUDA amenasa katika mtego dhaifu
aliojitegea mwenyewe, Na sasa kila mtu mwenye akili timamu anajua kuwa
SHIBUDA si mwana CHADEMA. Hivyo halali yake kufukuzwa, watanzani nao
wanachukulia maneno ya shibuda kama hoja za mwendawazimu ambazo si
busara na hekima kuzijadili.

viongozi wa CHADEMA wanastahili pongezi kwa jinsi walivyokabiliana naye
mpaka ananasa kirahisi katika mtego wake, japo kuwa MPENDAZOE
alishatahadharisha hili hata kabla ya uchaguzi wa mwaka 2010
akapuuzwa.
[/FONT]

Gamba Shibuda afukuzwe tufunge chapter vinginevyo ataendelea kuwa a drain on our leaders time and resources of our young party.
 
mkuu tukiwambia watu CHADEMA ni chama makini wanakua wagumu kumlewa vigezo ni kama hivyo mjifunze nyie akina ritz1 , Rejao na magamba wengine humu jamvini
 
Last edited by a moderator:
Gamba Shibuda afukuzwe tufunge chapter vinginevyo ataendelea kuwa a drain on our leaders time and resources of our young party.

huyu kwanza tutamuonesha kuwa CHADEMA tupo makini ili akiri vizur na kutuweka kwenye kumbukumbu yake hadi walio mtuma wata broo mapigo! Chezea M4C wewe
 
Huyu jamaa "aliletwa" CDM na Usalama wa Taifa kwa project maalum. Lakini kwa umakini wa CDM, hawakumruhusu kabisa kuingia "Jikoni" akabaki anachungulia tu kwa nje. Kwa hiyo ile mission yake ikawa ime-fail. Kwa kuwa alishajigamba kwamba ni lazima ataimaliza CDM, na kutokana na Ugumu alioukuta, sasa amebaki kama Mchawi ambaye ametunguliwa na Ungo wake mbele ya kadamnasi ya watu anatweta, mara azungumze hili mara lile na yote yanakuwa hayana mashiko zaidi ya kuendelea kuonekana Kiroja mbele ya jamii. RIP Shibuda.
 
namchukia sana shibuda kwa ngonjera za kinafiki dhidi ya CHADEMa, inapaswa akumbuke kuwa wananchi walimchagua ili asimamie sera safi za M4C na si ngonjera za kina bi kidude tena za matusi kwa wananchi wanaoiamini CHADEMA.
 
kuna hawa watoto vijana wa chadema niliona wamekurupuka wamejifanay eti kutoa tamko..hawa walikurupuka na inabidi wajirekebiseh .. mwendawazimu akioongea na wewe ukaja ukatoa tamko nani anaonekana mwendawazimu?
 
Shibuda anajua fika kuwa hakubaliki CCM wala CHADEMA, hivyo hivi sasa anatafuta njia ambayo ataonewa huruma endapo atachukuliwa hatua za kinidhamu!
 
Shibuda sijawahi kumwona kwenye mikutano ya cdm inayoendelea nchi nzima,sikuwahi kumwona igunga,meru wala popote akiamasisha mabadiliko,ila ameonekana ccm huko ndiko panamfaa na akiendelea kubaki cdm nimeshasema siku nikikutana nae ana kwa macho lazima nimtemee mate usoni na matakuja sikia
 
Shubuda Sijui she-bhudha au shibuda jameni mwoneeni huruma.. Ukigombana Na mgonjwa nani ataonekana mgonjwa..!!
 
mkuu tukiwambia watu CHADEMA ni chama makini wanakua wagumu kumlewa vigezo ni kama hivyo mjifunze nyie akina ritz1 , Rejao na magamba wengine humu jamvini

Kwa hiyo na CCM ni chama makini kwa kuwapuuza kina SITTA, MWAKYEMBE na recently Lowasa na slogan yake ya Youth time bomb?
 
Maskini Shibuda wa watu!
CCM walimtumia wakamtupa ka Condom iliyotumika.
Sasa the peoplez wakimtoa baru atakimbilia wapi tena?
 
Back
Top Bottom