Kuhusu Rais Magufuli Kushika Uenyekiti wa SADC, zamu yetu tena itafika miaka 16 ijayo

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
29,423
29,084
Kwanza nimpongeze Rais John Pombe Magufuli kwa 'kurithi' kiti cha Uenyekiti wa SADC. Pili nitoe elimu kidogo kuhusu Mwenyekiti wa SADC anavyopatikana, maana kumekuwa na upotoshaji wa makusudi kwamba amechaguliwa kwa sababu ya uchapakazi wake. 🤣

Protocol ya SADC inaeleza kuwa Uenyekiti wa jumuiya hiyo utakuwa wa mzunguko kila mwaka, na nchi inayohost mkutano mkuu, Mkuu wake wa nchi ndiye atakuwa Mwenyekiti.

SADC ilianzishwa 17 August 1992 ikiwa na nchi wanachama 9 tu, lakini mpaka sasa ni 16. Kwahiyo kutokana na protocal ni lazima nchi zote 16 zipokezane kwenye kuandaa mkutano mkuu na kurithi nafasi ya uenyekiti.

Mara ya kwanza Tanzania kuhost mkutano wa SADC ilikua mwaka 2003 na Mkuu wa nchi wakati huo Benjamin Mkapa alirithi kiti cha Uenyekiti wa Jumuiya hiyo. Akaongoza hadi mwaka 2004.

Miaka iliyofuata mkutano mkuu wa SADC ukaenda nchi zingine, na wenyeviti wakawa wakuu wa nchi hizo kwa kupokezana.

Tangu 2003 tulipoandaa mkutano mkuu wa SADC, miaka 16 imeisha mwaka huu. Kwahiyo mwaka huu ni zamu yetu. Si kwa sababu ya utendaji wa Rais JPM au uzuri wa Wema Sepetu. Ni kwa sababu zamu yetu imefika.

Na kwa sababu tumekuwa waandaaji, automatically Rais aliyeko madarakani anarithi uenyekiti wa jumuiya hiyo.

Kwahiyo Magufuli amekuwa Mwenyekiti kwa sababu ndiye Mkuu wetu wa nchi aliyepo madarakani kwa sasa. Hata kama Piere Liquid ndo angekuwa mkuu wa nchi, basi angerithi nafasi ya Uenyekiti wa SADC.

Kwahiyo Uenyekiti wa SADC hauhusiani kwa vyovyote na kuchapa kazi wala kucahapa maji. Tumepata fursa ya kuhost mkutano wa SADC mwaka huu kwa sababu ni zamu yetu katika mzunguko, na Rais wetu amerithi nafasi ya Uenyekiti kwa sababu ni zamu yetu. Period.

Achaneni na maneno ya 'vishohia' waliofeli Civics ya form one wanaosema eti uchapakazi wa JPM ndo umempa uenyekiti. Tuwasamehe bure. Tumpongeze Rais lakini tusitumie nafasi hiyo kupotosha.

Kama nchi wanachama hazitaongezeka au kupungua, zamu yetu tena itafika miaka 16 ijayo (mwaka 2035) na Rais atakayekuwepo madarani wakati huo atachaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa SADC bila kujalisha kama ni mchapakazi au mchapa maji.

Malisa GJ
 
Kwani kuna mtu alikuwa hajui kuwa uenyekiti wa SADC ni wa kupokezana kijiti???
Ni utoto kuandika kinachojulikana kwa wote nani hajui jambo hilo? Tatizo kubwa mahater wa Magufuli wanapata shida sana na mwisho wanafanya utoto
Wapo waliodhani amechaguliwa kwa sababu ya uchapakazi, ndio hao aliowaelewesha.
 
Hilo bandiko angelipeleka Facebook lika kaa hukohuko ndoo kunakokolo la kila aina ya maoni ya wachanguaji
 
55 Reactions
Reply
Back
Top Bottom