Kuhusu ongezeko la kutuma na kupokea pesa kwenye mihamala ebu tuache kulialia jamani

Kwenye hili la ongezeko la hela ya tozo kwenye mihamala ebu watanzania tuache kulia kulia ayo ndio maendeleo na kwani kabla azijakuwepo hii huduma tulikuwa tunatumia huduma gani ebu tuache serikali ifanye kazi ituletee maendeleo sio kila jambo kulalama tu .serikali mpk kuweka hili imeshakaa na kufanya uchunguzi sio kama imekurupuka tusipende kupinga tu uku tunataka dawa hospital.watoto wasome bure wewe mtanzania unachangia nini yangu leo ni hayo
Fahari yetu nchi yetu mungu bariki
Hela Moja inakatwa Kodi Mara mbili hivi hawajui mtumaji pesa ndo hua anatuma na ya kutolea waache aiseee hii Kodi ya miamala ya simu inatakiwa ijadiliwe upya lasivyo hawatapata Hata cent labda kwa wafanyabiashara wakubwa ila sisi wa online business kwa kweli hawatatuona
 
Nchi yenye Gesi ya asili kwa matrilioni huko ardhini.
Nchi yenye Wakayama wengi ambao tukianzisha mabucha ya kuuza nyama nje tutapata fedha nyingi sana mana kwa sasa Wakayama ni wengi na wanadhuru watu Mpaka Mungu akiyewaumba anatushangaa. Wanyama wanawaua watu badala ya watu kuwakamata na kuwafuga ili wawaletee maisha bora.

Nchi yenye Madini ya kila namna lakini viataku vingi wameshika makada wa CCM na matapeli wengine.

Nchi yenye bahari iliyosheheni Samaki wa kila aina walioumbwa na Mungu ili wampe mwanadamua maisha mazuri na chakula bora lakini leo hata bei ya samaki binadam anayekatwa bando kwenye mitandao iliyotengenezwa na mabeberu ananyonywa wakati Mungu amempa mwafrika utajiri mkubwa ili mwafrika asitaabike zaidi ya kumwajiri Mzungu aje kuwa kibarua wa kuchimba madini .

CCM ya awamu ya tano imewapofusha watawala macho ndio maana walitaka kumkweza na kumtukuza mtu kuwa ndiye mwenye nchi na ameumba kila kilichoko juu ya ardhi ya Tanzania wakati Mungu ametupa utajiri mkubwa wa kuwafanya watanzania kuishi kama Waarabu wa Dubai.

Nchi yenye maziwa makubwa na samaki wa kutosha.
Nchi yenye ngombe mamilioni wa kienyeji wasiohitaji gharama kubwa kuwatunza.

Nchi yenye Tembo wanaokufa kifo cha asili na kuacha utajiri mkubwa wa Pembe na Meno lakini sheria mbovu za Watawala na wabunge waroho wa CCM na mawaziri wao wanazikusanya na kuziuza kimagendo na kuziweka ghalani wakijadili eti wazichome moto na mtu akikutwa na pembe moja tu anaweza akauawa wakati tembo amezeeka akafa. Na kuna wachena wanaotaka kununua ili tupate fedha za bure kutokana na uumbaji wa Mungu.

Nchi yenye mawaziri na wabunge wasioweza kutafsiri uumbaji wa Mungu na madhumuni ya utajiri mkubwa aliowapa waafrika wanaoishi Tanzania kamwe hawezi kutuletea maendeleo zaidi ya laana.
Mawaziri na makada wa CCM wanawafanya Watanzania kuwa ni watumwa na wao ni Mabwana au wakoloni weusi , ndo maana wanatumia sheria ,kanuni,mitizamo,mifumo ,katiba na hulka za mkoloni huku wao wakiishi Maisha ya anasa na utajiri uliopitiliza kwa migongo ya maskini iliyovunjika kwa kazi ngumu.

Nchi yenye ardhi kubwa yenye rutuba kutegemea uchumi uendeshwe kwa mafuta yanayotoka kwa waarabu na mitandao ya wazungu ni ajabu na kuwaumiza wau.

Tukitegemea nchi ipate mapato kutokana na kuzalisha mazao kama Michele,korosho, katani,Mahindi, maharage,ngombe,nguruwe, madini ,misitu,samaki wanayama pori ,kuongeza uzalishaji wa Sukari na kuuza nje, kuongeza uzalishaji wa sementi na kuuza nje ,kuongeza ufanisi kwenye bandari na kudhibiti wizi unaofanywa na wafanyakaizi wa bandari kwa kudhibiti Mali za wizi walizo nazo.
Kudhibiti wizi na rushwa kwa wafanyakazi wa TRA. Mtu anafanya kazi kwenye idara ya serikali kama bandari anakua bilionea.

Wameshindwa Kudhibiti wizi unaofanywa na wafanyakazi wa Taasisi za umma.
Mana wizi wa Mali ya umma ni mtandao uliojengwa kwa muda mrefu ndani ya serikali ya CCM isiyotaka katiba itakayowakamata majizi kisheria na kuwanyima uongozi wezi na familia zao zinazopata heshima kutokana na Mali za wizi walizokwapua walipokua wanasimamia mashirika ya umma,madaraka n.k.Matokeo yake wanawaumiza watu wanaojitafutia mlo wa kila siku.
Hivi mtu kama waziri anashida gani na ongezeko la gharama za mtandao wakati anapewa ,mafuta ya gari Bure,gari LA serikali,nyumba ya serikali,pesa ya umeme,pesa ya mawasiliano yaani simu ,pesa ya jimbo, mlinzi wa serikali,

Waziri Kodi atailipa wapi wakati pesa ya mawasiliano anapewa naserikali. Mafuta anapewa na serikali na service ya gari.

Ni Bora mkoloni alikua na kazi moja tu ya kujenga nchi na sio kujijenga binafsi kuliko wakoloni weusi wanaotawala leo ambao wanawaza kujijengea Mali binafsi kama vile majumba,mahoteli ,mabasi ,malori na mashule kupitia ofsi za umma.

Hapa watanzania tutambue kuwa tunatawaliwa na watu wanaowaza ufahari wao binafsi bila kuumiza familia zao ndio maana wanawaza kujenga masanamu kama yale yaliyovunjwa enzi za Mtume Muhommad yaliyokuwa yanaabudiwa na kutukuzwa kama yale ya Firauni. Watawala hawajui kuwa kuna shule hazina maji wala vyoo vya shimo. Watoto wanatumia makaratasi vichakani. Wao wanawaza masanamu ya miungu iliyowapa madaraka na kuwapitisha kwenye ubunge bila kushinda kura kihalali
Umeongea ukweli halisi.
 
Kwenye hili la ongezeko la hela ya tozo kwenye mihamala ebu watanzania tuache kulia kulia ayo ndio maendeleo na kwani kabla azijakuwepo hii huduma tulikuwa tunatumia huduma gani ebu tuache serikali ifanye kazi ituletee maendeleo sio kila jambo kulalama tu .serikali mpk kuweka hili imeshakaa na kufanya uchunguzi sio kama imekurupuka tusipende kupinga tu uku tunataka dawa hospital.watoto wasome bure wewe mtanzania unachangia nini yangu leo ni hayo
Fahari yetu nchi yetu mungu bariki
We popoma TOZO YA MIAMALA YA PESA NI REGRESSIVE Tatizo la tozo hii ni kwamba watu wa kipato cha chini wanalipa tozo at a higher rate (ya kipato chao) kuliko mataajiri.

Tozo hii inawakamuana sana masikini.
 
Kwenye hili la ongezeko la hela ya tozo kwenye mihamala ebu watanzania tuache kulia kulia ayo ndio maendeleo na kwani kabla azijakuwepo hii huduma tulikuwa tunatumia huduma gani ebu tuache serikali ifanye kazi ituletee maendeleo sio kila jambo kulalama tu .serikali mpk kuweka hili imeshakaa na kufanya uchunguzi sio kama imekurupuka tusipende kupinga tu uku tunataka dawa hospital.watoto wasome bure wewe mtanzania unachangia nini yangu leo ni hayo
Fahari yetu nchi yetu mungu bariki
kwa nini wabunge hawaatwi kodi?
 
Back
Top Bottom