Kuhusu ongezeko la kutuma na kupokea pesa kwenye mihamala ebu tuache kulialia jamani

ommytk

JF-Expert Member
Jul 30, 2015
482
1,053
Kwenye hili la ongezeko la hela ya tozo kwenye mihamala ebu watanzania tuache kulia kulia ayo ndio maendeleo na kwani kabla azijakuwepo hii huduma tulikuwa tunatumia huduma gani ebu tuache serikali ifanye kazi ituletee maendeleo sio kila jambo kulalama tu .serikali mpk kuweka hili imeshakaa na kufanya uchunguzi sio kama imekurupuka tusipende kupinga tu uku tunataka dawa hospital.watoto wasome bure wewe mtanzania unachangia nini yangu leo ni hayo
Fahari yetu nchi yetu mungu bariki
 
Serikali hii uwa inakurupuka kila mdaa

Viongozi hawana uelekeo kila kauli yao leo kesho ni tofautii

Bunge la rangi moja

Vitu kama hivi tuvitarajie sana

Ni muda sasa kila mwananchi awekeze bank tu

Ili waje na uko tutajua cha kufanya
 
Kwangu mimi kodi,michango ni muhimu ispokuwa kuna vijamaa kazi yao kula michango na kodi za watanzania.
Fuatilia michango vijijini, inaliwa na watendaji na wenyekiti wa vijiji. Shida ipi hapo.
 
Hili la kodi/tozo kuwa kubwa kuliko fee ya kampuni ya simu lina ukakasi sana. Technically, wamegeuza core business ya kampuni za simu ni kukusanya kodi....na hiyo fee yao ni kama commission tu ya kuisaidia serikali kukusanya kodi.

Halijakaa sawa kabisa. Kuna mtu/watu watalipa gharama kubwa sana kwa haya maamuzi yao. Ipo nafasi ya kurekebisha, waitumie haraka.

Wanaweza kupunguza viwango vya hizo tozo na kupunguza matumizi (e.g. wapunguze mishahara/malipo ya wabunge, wapunguze ukubwa wa serikali, wapunguze magari ya gharama kubwa, wasianzishe miradi mikubwa mipya kabla ya iliyopo kukamilika, etc.)
 
Kwenye hili la ongezeko la hela ya tozo kwenye mihamala ebu watanzania tuache kulia kulia ayo ndio maendeleo na kwani kabla azijakuwepo hii huduma tulikuwa tunatumia huduma gani ebu tuache serikali ifanye kazi ituletee maendeleo sio kila jambo kulalama tu .serikali mpk kuweka hili imeshakaa na kufanya uchunguzi sio kama imekurupuka tusipende kupinga tu uku tunataka dawa hospital.watoto wasome bure wewe mtanzania unachangia nini yangu leo ni hayo
Fahari yetu nchi yetu mungu bariki
Boya sana
 
Utakuwa Job Ndugai wewe sio bure au Waziri wizara nyeti.

HAKUNA MTANZANIA WA KAWAIDA ANAYETETEA HUU UPUUZI.
 
Kwenye hili la ongezeko la hela ya tozo kwenye mihamala ebu watanzania tuache kulia kulia ayo ndio maendeleo na kwani kabla azijakuwepo hii huduma tulikuwa tunatumia huduma gani ebu tuache serikali ifanye kazi ituletee maendeleo sio kila jambo kulalama tu .serikali mpk kuweka hili imeshakaa na kufanya uchunguzi sio kama imekurupuka tusipende kupinga tu uku tunataka dawa hospital.watoto wasome bure wewe mtanzania unachangia nini yangu leo ni hayo
Fahari yetu nchi yetu mungu bariki
Nchi yenye Gesi ya asili kwa matrilioni huko ardhini.
Nchi yenye Wakayama wengi ambao tukianzisha mabucha ya kuuza nyama nje tutapata fedha nyingi sana mana kwa sasa Wakayama ni wengi na wanadhuru watu Mpaka Mungu akiyewaumba anatushangaa. Wanyama wanawaua watu badala ya watu kuwakamata na kuwafuga ili wawaletee maisha bora.

Nchi yenye Madini ya kila namna lakini viataku vingi wameshika makada wa CCM na matapeli wengine.

Nchi yenye bahari iliyosheheni Samaki wa kila aina walioumbwa na Mungu ili wampe mwanadamua maisha mazuri na chakula bora lakini leo hata bei ya samaki binadam anayekatwa bando kwenye mitandao iliyotengenezwa na mabeberu ananyonywa wakati Mungu amempa mwafrika utajiri mkubwa ili mwafrika asitaabike zaidi ya kumwajiri Mzungu aje kuwa kibarua wa kuchimba madini .

CCM ya awamu ya tano imewapofusha watawala macho ndio maana walitaka kumkweza na kumtukuza mtu kuwa ndiye mwenye nchi na ameumba kila kilichoko juu ya ardhi ya Tanzania wakati Mungu ametupa utajiri mkubwa wa kuwafanya watanzania kuishi kama Waarabu wa Dubai.

Nchi yenye maziwa makubwa na samaki wa kutosha.
Nchi yenye ngombe mamilioni wa kienyeji wasiohitaji gharama kubwa kuwatunza.

Nchi yenye Tembo wanaokufa kifo cha asili na kuacha utajiri mkubwa wa Pembe na Meno lakini sheria mbovu za Watawala na wabunge waroho wa CCM na mawaziri wao wanazikusanya na kuziuza kimagendo na kuziweka ghalani wakijadili eti wazichome moto na mtu akikutwa na pembe moja tu anaweza akauawa wakati tembo amezeeka akafa. Na kuna wachena wanaotaka kununua ili tupate fedha za bure kutokana na uumbaji wa Mungu.

Nchi yenye mawaziri na wabunge wasioweza kutafsiri uumbaji wa Mungu na madhumuni ya utajiri mkubwa aliowapa waafrika wanaoishi Tanzania kamwe hawezi kutuletea maendeleo zaidi ya laana.
Mawaziri na makada wa CCM wanawafanya Watanzania kuwa ni watumwa na wao ni Mabwana au wakoloni weusi , ndo maana wanatumia sheria ,kanuni,mitizamo,mifumo ,katiba na hulka za mkoloni huku wao wakiishi Maisha ya anasa na utajiri uliopitiliza kwa migongo ya maskini iliyovunjika kwa kazi ngumu.

Nchi yenye ardhi kubwa yenye rutuba kutegemea uchumi uendeshwe kwa mafuta yanayotoka kwa waarabu na mitandao ya wazungu ni ajabu na kuwaumiza wau.

Tukitegemea nchi ipate mapato kutokana na kuzalisha mazao kama Michele,korosho, katani,Mahindi, maharage,ngombe,nguruwe, madini ,misitu,samaki wanayama pori ,kuongeza uzalishaji wa Sukari na kuuza nje, kuongeza uzalishaji wa sementi na kuuza nje ,kuongeza ufanisi kwenye bandari na kudhibiti wizi unaofanywa na wafanyakaizi wa bandari kwa kudhibiti Mali za wizi walizo nazo.
Kudhibiti wizi na rushwa kwa wafanyakazi wa TRA. Mtu anafanya kazi kwenye idara ya serikali kama bandari anakua bilionea.

Wameshindwa Kudhibiti wizi unaofanywa na wafanyakazi wa Taasisi za umma.
Mana wizi wa Mali ya umma ni mtandao uliojengwa kwa muda mrefu ndani ya serikali ya CCM isiyotaka katiba itakayowakamata majizi kisheria na kuwanyima uongozi wezi na familia zao zinazopata heshima kutokana na Mali za wizi walizokwapua walipokua wanasimamia mashirika ya umma,madaraka n.k.Matokeo yake wanawaumiza watu wanaojitafutia mlo wa kila siku.
Hivi mtu kama waziri anashida gani na ongezeko la gharama za mtandao wakati anapewa ,mafuta ya gari Bure,gari LA serikali,nyumba ya serikali,pesa ya umeme,pesa ya mawasiliano yaani simu ,pesa ya jimbo, mlinzi wa serikali,

Waziri Kodi atailipa wapi wakati pesa ya mawasiliano anapewa naserikali. Mafuta anapewa na serikali na service ya gari.

Ni Bora mkoloni alikua na kazi moja tu ya kujenga nchi na sio kujijenga binafsi kuliko wakoloni weusi wanaotawala leo ambao wanawaza kujijengea Mali binafsi kama vile majumba,mahoteli ,mabasi ,malori na mashule kupitia ofsi za umma.

Hapa watanzania tutambue kuwa tunatawaliwa na watu wanaowaza ufahari wao binafsi bila kuumiza familia zao ndio maana wanawaza kujenga masanamu kama yale yaliyovunjwa enzi za Mtume Muhommad yaliyokuwa yanaabudiwa na kutukuzwa kama yale ya Firauni. Watawala hawajui kuwa kuna shule hazina maji wala vyoo vya shimo. Watoto wanatumia makaratasi vichakani. Wao wanawaza masanamu ya miungu iliyowapa madaraka na kuwapitisha kwenye ubunge bila kushinda kura kihalali
 
Hatuna raisi tumepigwa acheni kuyumbisha
Tatizo sio Rais ,tatizo ni wale aliowabeba na kuendelea nao.
Amekosea sana kutovunja baraza la mawaziri na kuunda baraza lake jipya lenye mtizamo wa serikali yake sio mtizamo wa mtu akiyewahi kutawala kwa namna ya inayopelekea kauli ya Dr. Antony.

Kama ummaskini ungepungua basi Fungu la Tasaf lingepungua badala yake limeongezeka na wahitaji wameongezeka.

Mawaziri wengi ni zao la dhulma kwenye uchaguzi wa mwaka jana 2020 hivyo hawana haja ya kuwatendea wema wananchi .

Mpaka zao hili la dhulma litakapotupwa nje ndipo watanzania watakapopata viongozi wanaoguswa na ugumu wa maisha wa wapiga kura zaidi ya kukamuliwa pesa za kununua magari ya kifahari na misafara mikubwa huku wakiongeza bei ya mafuta.
 
Kwahiyo unaamini Yanayotokea raisi Hana baraka zake.

Ndio maana watanzania ni vichwa maji , Yani hujui nafasi ya raisi kwenye miswaada inayenda bungeni na kuwa sheria.

Endeleeni kupigwa Hadi akili ziwakae sawa
 
Kwenye hili la ongezeko la hela ya tozo kwenye mihamala ebu watanzania tuache kulia kulia ayo ndio maendeleo na kwani kabla azijakuwepo hii huduma tulikuwa tunatumia huduma gani ebu tuache serikali ifanye kazi ituletee maendeleo sio kila jambo kulalama tu .serikali mpk kuweka hili imeshakaa na kufanya uchunguzi sio kama imekurupuka tusipende kupinga tu uku tunataka dawa hospital.watoto wasome bure wewe mtanzania unachangia nini yangu leo ni hayo
Fahari yetu nchi yetu mungu bariki
Athari yake ni kuuwa ajira na uchumi.
Toka lini mswahili aliyeshiba akawa na fikra.Kama kubana matumizi kwann wasianze wao wauze v8 wanunue ist,wabunge walipwe kupitia simu zao.
 
Kwenye hili la ongezeko la hela ya tozo kwenye mihamala ebu watanzania tuache kulia kulia ayo ndio maendeleo na kwani kabla azijakuwepo hii huduma tulikuwa tunatumia huduma gani ebu tuache serikali ifanye kazi ituletee maendeleo sio kila jambo kulalama tu .serikali mpk kuweka hili imeshakaa na kufanya uchunguzi sio kama imekurupuka tusipende kupinga tu uku tunataka dawa hospital.watoto wasome bure wewe mtanzania unachangia nini yangu leo ni hayo
Fahari yetu nchi yetu mungu bariki
Kwani hizi ndizo tozo za kwanza kuambiwa kuwa ni kwa ajiri ya kuleta maendeleo fulani?je yaliletwa? Bajeti ya 2020/2021, waliongeza tozo kwenye mafuta kuwa pesa hizo zingetumika kwenye ujenzi wa barabara za mjini na vijijini, kupitia TARURA, hizo pesa zilifika huko kila mbunge alikuwa ni kupiga kelele tu mbona tarura ipo hoi?!!huwezi kuongeza mapato wakati pesa nyingi inapotea tu bila maelezo, unaweza ukaleta maendeleo kwa kutumia pesa ipasavyo hiyo unayokusanya tu, na maendeleo yakawepo, vile vile unaweza ukawakamua wananchi ile mbaya na bado maendeleo yasiwepo.
 
Back
Top Bottom