Ngonepi
JF-Expert Member
- Jun 2, 2013
- 1,872
- 1,200
Inanisikitisha sana na inaumiza ninaposoma habari kwamba kuna baadhi ya viongozi wa serikali wanaoishi mahotelini kwa sababu ya kukosa makazi. Uongozi wa Mwl Nyerere kwa makusudi kabisa ulijenga nyumba za kutosha kabisa kwa viongozi wa serikali kule Masaki na Oysterbay, Bila ya huruma wala uzalendo kwa taifa viongozi wa kileo wameamua kugawana nyumba zile kwa kuita kuwa wanauziana tena kwa bei ambayo hata ukienda Vingunguti hupati nyumba,matokeo yake leo serikali inaingia gharama kuubwa sana kwa kuwapangia viongozi mahotelini, hii ianumiza sana maana pesa ambazo zingetumika kutatua changamoto nyingi za wananchi zinapelekwa kwa kwenye matumizi ambayo hayakuwa ya lazma kama wasingegawana nyumba zile. Ajabu waliouziwa wanavunja nyumba zile na kujenga mahekalu makubwa kabisa!! SASA kwa taarifa yenu ninyi endeleeni tu kuwekeza kwenye hizo ploti na pia mwendelee kuombea hivyohivyo CCM iendelee kutawala LA SIVYO haki ya Mungu ninyi na watoto wenu mtalia machozi ya DAMU siku mchama wenu huu WAKIJANI tutakapoundoa madarakani. Nawamind sana walafi ninyi!!