Kuhusu nyumba za serikali za Oysterbay na M asaki Daressalaam.

Ngonepi

JF-Expert Member
Jun 2, 2013
1,872
1,200
Inanisikitisha sana na inaumiza ninaposoma habari kwamba kuna baadhi ya viongozi wa serikali wanaoishi mahotelini kwa sababu ya kukosa makazi. Uongozi wa Mwl Nyerere kwa makusudi kabisa ulijenga nyumba za kutosha kabisa kwa viongozi wa serikali kule Masaki na Oysterbay, Bila ya huruma wala uzalendo kwa taifa viongozi wa kileo wameamua kugawana nyumba zile kwa kuita kuwa wanauziana tena kwa bei ambayo hata ukienda Vingunguti hupati nyumba,matokeo yake leo serikali inaingia gharama kuubwa sana kwa kuwapangia viongozi mahotelini, hii ianumiza sana maana pesa ambazo zingetumika kutatua changamoto nyingi za wananchi zinapelekwa kwa kwenye matumizi ambayo hayakuwa ya lazma kama wasingegawana nyumba zile. Ajabu waliouziwa wanavunja nyumba zile na kujenga mahekalu makubwa kabisa!! SASA kwa taarifa yenu ninyi endeleeni tu kuwekeza kwenye hizo ploti na pia mwendelee kuombea hivyohivyo CCM iendelee kutawala LA SIVYO haki ya Mungu ninyi na watoto wenu mtalia machozi ya DAMU siku mchama wenu huu WAKIJANI tutakapoundoa madarakani. Nawamind sana walafi ninyi!!
 
nakumbuka hata enzi za nyerere kuna viongozi wengi tu walikua wanakaa kwenye mahoteli yetu e.g. kilimanjaro hotel enzi hizo hadi kufikia hoteli kufilisika

pia sisahau bosi mmoja alihamishiwa new africa hotel enzi za mwalimu na kukaa pale for years huku nyumba za serikali zipo

the bottom line is, we do have a bigger problem, nalo ni accountability
 
Inanisikitisha sana na inaumiza ninaposoma habari kwamba kuna baadhi ya viongozi wa serikali wanaoishi mahotelini kwa sababu ya kukosa makazi. Uongozi wa Mwl Nyerere kwa makusudi kabisa ulijenga nyumba za kutosha kabisa kwa viongozi wa serikali kule Masaki na Oysterbay, Bila ya huruma wala uzalendo kwa taifa viongozi wa kileo wameamua kugawana nyumba zile kwa kuita kuwa wanauziana tena kwa bei ambayo hata ukienda Vingunguti hupati nyumba,matokeo yake leo serikali inaingia gharama kuubwa sana kwa kuwapangia viongozi mahotelini, hii ianumiza sana maana pesa ambazo zingetumika kutatua changamoto nyingi za wananchi zinapelekwa kwa kwenye matumizi ambayo hayakuwa ya lazma kama wasingegawana nyumba zile. Ajabu waliouziwa wanavunja nyumba zile na kujenga mahekalu makubwa kabisa!! SASA kwa taarifa yenu ninyi endeleeni tu kuwekeza kwenye hizo ploti na pia mwendelee kuombea hivyohivyo CCM iendelee kutawala LA SIVYO haki ya Mungu ninyi na watoto wenu mtalia machozi ya DAMU siku mchama wenu huu WAKIJANI tutakapoundoa madarakani. Nawamind sana walafi ninyi!!

Usichokijua ni kwamba hata Upinzani wakishinda Uchaguzi ujao hakuna mwenye jeuri ya kunyang'anya hizo Nyumba, Wanasiasa wanaongea tu Majukwaani na kudanganya watu ili wapate kura, lkn swala la kuuza Nyumba lilikuwa ni lazima kwa sababu ya Gharama za uendeshaji na halikuwa wazo ya Serikali ya JMT bali lilikuwa ni wazo au shinikizo kutoka kwa wahisani (IMF na Benki ya Dunia, Umoja wa Ulaya n.k) kwamba ili Serikali iweze kupata Misaada ni lazima ipunguze gharama za uendeshaji ikiwa ni pamoja na kuuza nyumba zote za Serikali, viwanda ambavyo vinapata ruzuku toka serikalini n.k!

Sasa kama Wapinzani wataenda kinyume na wahisani, siamini, kwa sababu hata leo hii Bw.Slaa yuko Ujerumani, kufanya nini? Ujerumani ni moja ya Wahisani wakubwa, hivyo ili Upinzani washinde na kuongoza kwa amani ni lazima wasiwakasirishe Wahisani, hapo ndipo shughuli ilipo!
 
Rasilimali zetu zikisimamiwa vizuri, haina haja ya kuwapigia magoti wahisani zaidi ya ushirikiano wa maendeleo
 
Back
Top Bottom