TandaleOne
JF-Expert Member
- Sep 4, 2010
- 1,644
- 709
Ndugu zangu wanajamvi.,nimekuwa kimya sana kwa muda mrefu..ukimya wangu ulisababishwa na mambo mengi kama ambavyo baadhi mnayajua na mengine makubwa hamyajui na hayatajulikana.
Lipo jambo linaendelea nchini, jambo hili kwa kiasi chake limecatch attention ya Taifa labda hata kuzidi Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, nalo ni uchaguzi wa Mwenyekiti wa CHADEMA. Hii ni kwasababu CHADEMA kwasasa limekuwa ni jiwe la pembeni ambalo wengi wanalitazama kama JIWE KUU la baadae. Maisha ya Watanzania hasa wanasiasa walio wengi hata wale walio katika vyama vingine vya siasa hata Chama changu CCM tunaitazama CHADEMA kama alternative ya siasa zao mambo yakienda mrama...naam baadhi wamefanya hivyo..,ingawa mimi siamini na sitakuwa miongoni mwa wenye mtazamo huo, ila nasema wapo, tena wapo wa kutosha.
Linapokuja suala la kumpata Nahodha wa kuendesha chombo hicho kilichobeba ndoto na matumaini ya wengi, hata siku moja suala hilo haliwezi kuwa jambo la kupuuzwa na ndio maana nimeamua kuvunja ukimya, nimeona niseme kama ambavyo nimekuwa nikisema hapo nyuma.
Mpaka sasa katika waliojitokeza kugombea nafasi hiyo wapo;
1:MBOWE Freeman AIkaeli
2:MWAMBE Cecil
3:SUMAYE Fredrick
Wawili kati ya watatu hao wamejiunga ndani ya Chama hicho ndani ya miaka minne iliyopita na sababu ikiwa ni dhoruba iliyowakumba wakiwa CCM, wakahamia CHADEMA sio kwa Imani ya Itikadi, sio kwa mapenzi ya Siasa zake bali kwa msukumo na ulazima wa kukosa nafasi CCM, ndiko kulikowasukuma kujiunga na CHADEMA as an alternative platform ya kuendelea kufanya siasa zao. Hawaamini katika itikadi, sera wala mfumo wa siasa za CHADEMA, hawafurahishwi na muundo wala mtindo wa siasa za uhanaharakati. Wao si waumini wa siasa za u-liberali.
Lakini, lipo jambo lazima wapiga kura wanaoenda kumchagua nahodha wa chombo hicho walifahamu kuwa yupo mtu ambae ameasisi, ameamini na ameiishi misingi ya siasa za uhanaharakati na uliberali za chama hicho, na kwa uongozi wake Chama kimepata mafanikio makubwa, hakuna ubishi leo hii kuwa uimara na ukubwa wa CHADEMA na hata umaarufu wake duniani unafungamana na utendaji uliotukuka wa Mwamba, Freeman Aikaeli Mbowe.(Lazima nieleweke, mimi sio mpiga kampeni wala sio mwanachama wa CHADEMA ila nawasaidia maarifa.) Mtu huyu amepoteza heshima, hadhi na kuharibikiwa na mambo yake mengi kwa sababu ya kuifikisha CHADEMA ilipofika, amevuja machozi, jasho na damu kuiingiza CHADEMA katika mioyo ya Watanzania, haikuwa kazi rahisi....mimi nasema hayo nikiwa nafahamu namna ambavyo tulipambana nae kama CHAMA na nakumbuka mpambano wangu binafsi dhidi yake...mnyonge mnyongeni lakini sifa zake apewe, amenisumbua, ametusumbua na anaendelea kusumbua ndio maana watu wenye akili wanataka kuondokana na usumbufu huo.
Ndugu zangu wanachadema, nendeni mkafanye maamuzi, nendeni mkachague MWENYEKITI lakini abadani msiruhusu Oil CHAFU kushika hatamu ya uongozi wenu, hamtafika salama...nawaambieni msikie. Mnapita katika njia yenye miba, mwenye akili atabaki na mitalawanda yake na sio safariboot za kuazimwa, hazitawavusha. MSIOGOPE KUUSEMA UKWELI HUU, tena tuuseme kwa kuangaliana usoni bila tashwishi.
Nawatakia kila la heri...
#TufanyeSiasaZisizoumiza