Jagina
JF-Expert Member
- Jan 29, 2019
- 5,676
- 2,350
Aliyesema kuwa watapewa mafuta na Oman ni mzanzibari sio mimi. Na ni kitu gani kinachowazuia wa Omani kuwamegea utajiri sasa hivi kama ambavyo wanawamegea waomani wenzao?
Unaposema kuwa Muungano umeshindwa kuwaletea faida Wazanzibari una maana kuwa mlitegemea watanganyika ndio wangewapelekea maendeleo? Shule, hospitali zote ziko chini ya serikali yao, JMT inahusika vipi? Kama wameuchoka kwa sababu walitegemea watanganyika wawabebe basi bora wauvunje watafute mjomba wa kuwabeba. Wazanzibari wanatakiwa wajitathmini wenyewe ili wajue wapi wanakosea. Waunguja wapime athari za kuwaminya wapemba kwa uchumi wao halafu wajirekebishe. Unadhani wapemba wamewekeza Bara kwa sababu wanawapenda sana machogo? La hasha, walifanya hivyo baada ya kunyimwa fursa na wazanzibari wenzao. Wazanzibari wajitahidi kujenga nchi yao wenyewe kama ambavyo Singapore na Mauritius walivyofanya. Wakiendelea wao na sisi tutaendelea ndio maana hatufurahii umasikini wao.
Amandla...