Leo kumetokea mlipuko katika ibada Kanisa Katoliki Olasiti, nianze kwa kutoa pole kwa wafiwa na majeruhi wote. Tukio hilo ni mlolongo wa matukio mbalimbali yaliyotokea yanayolenga makanisa na viongozi wa dini.
Ilianza mbagala-Dsm, Zanzibar na Mwanza, katika matukio haya hakuna hatua za dhati zilizochukuliwa zinazoonyesha kweli viongozi wetu wanakerwa na matukio hayo.
Kiongozi Mkuu wa nchi naye anahutubia kwa kulalamika badala ya kutoa tamko kali. Ebu angalia mtuhumiwa wa mauaji ya Padri huko Zanzibar anapelekwa mahakamani huku akicheka utafikiri kuna usanii unaendelea.
Sasa angalia issue nyingine Olasiti ndio kata ambayo diwani wake kahama kutoka CCM kuhamia Chadema na kata hiyo haijatangazwa kufanya uchaguzi. Wana JF ebu tuunganishe matukio haya yote ili tuone na juhudi za kuwakamata wahalifu katika tukio la leo zinawekwa uzito gani na tulinganishe na nguvu za Polisi waliotumika kumkamata Mbunge Lema.
Kingine kila matukio ya aina hii yanapotokea Mkuu wa kaya aidha yupo nje au anaenda nje ya nchi.
Hali hizi zote tuzitafakari halafu tuje na hitimisho baadaye. Mimi ninachokoza tuu, karibuni tudodoze masuala haya.