Kuhusu mgomo wa madaktari: Cabinet yatoa msimamo wake: | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuhusu mgomo wa madaktari: Cabinet yatoa msimamo wake:

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OSOKONI, Feb 9, 2012.

 1. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,788
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  MGOMO WA MADAKTARI: Mawaziri wapendekeza waziri wa Afya atoswe

  KUFUATIA mgomo wa madaktari unaoendelea nchini, Baraza la Mawaziri limependekeza Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Haji Mponda na Katibu mkuu wake, Blandina Nyoni, kuwajibishwa ili kurejesha imani ya madaktari kurudi kwenye meza ya mazungumzo.
  Katika kikao cha kazi kilichofanyika juzi chini ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, inadaiwa mawaziri hao walimweleza kuwa kutokana na hali ya mgomo wa madaktari kuchafuka kupindukia, hakuna budi Waziri, naibu wake na katibu mkuu wakawajibishwa.
  Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho, zilidai kuwa suala la mgomo lilipofikia haliwezi likashughulikiwa kimyakimya, lazima Serikali ikakubali kukaa na madaktari hao na kusikiliza malalamiko yao.
  “Tumemweleza Waziri Mkuu (Pinda) kwamba madaktari wanasema hawana imani na watu hawa (waziri na katibu mkuu), hivyo hakuna njia ya kuwarejesha meza ya mazungumzo hadi viongozi hawa wawe wameondolewa,” kilieleza chanzo chetu cha uhakika.
  Tayari, pendekezo hilo lilishatolewa na Kamati ya Wabunge wa CCM, ambao walitaka Dk Mponda, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Lucy Nkya na Nyoni wajiuzulu au wakikataa wawajibishwe.
  Pia, mawaziri hao walikubaliana kusaidia kushawishi wabunge kupitisha muswada wa mabadiliko ya katiba, ambao unapingwa na wabunge wa CCM, huku wengine wakitaka wabunge wasidhibitiwe kutoa dukuduku lao.
  Suala la mgomo wa madaktari ambalo hivi sasa linashughulikiwa na Kamati ya Bunge ya Huduma ya Jamii, halijapata ufumbuzi zaidi ya kuzidi kupanuka kila siku na kuathiri huduma za afya.
  Hata hivyo, wakati akikabidhi suala la mgomo huo wiki iliyopita kwa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, Naibu Spika, Job Ndugai, alionyesha wasiwasi na kauli ya Serikali iliyotolewa na Dk Mponda bungeni, ambayo haikujumuisha baadhi ya malalamiko ya madaktari.
  “Lakini pia, katika submission ya Mheshimiwa Waziri ya Kauli, ya madai yale yaliyodaiwa na Madaktari, hata Mheshimiwa Waziri Mkuu ambaye tunamshukuru sana alipolishughulikia suala hili alipoenda kule kukutana nao na wao hawakujitokeza, lilikuwepo dai moja ambalo sijalisikia likizungumzwa hapa na ni vigumu kuzungumziwa!” alisema Ndugai na kuongeza:
  “Nalo ni kwamba, hawa mabwana wanadai kwamba katika Wizara ya Afya kuna baadhi ya watendaji wakuu wenye uwezo mdogo wa utendaji na wa kiuongozi, wasiowajibika ipasavyo."
  Na hawa watendaji wana kauli za kashfa na dharau kwa Madaktari. Kwa kutegemea timu ile iliyoundwa na Serikali itakayoripoti kulekule, itakuwa ni vigumu vilevile kupata ukweli wa upande huu wa pili.”

  mwananchi
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Feb 9, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Hii ni hatari. Kama ni kweli mawaziri walishauri hivyo JK ni lazima avunje Baraza la Mawaziri kwani nawaziri wote waliapa "kutokutoa siri za baraza la mawaziri"
   
 3. c

  chama JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji,
  Kuvunja baraza la mawaziri sio tija, kinachotakiwa kufanywa na mh. Raisi ni kuweka maslahi ya Taifa mbele, baraza zima la mawaziri limetengenezwa kiushikaji ili kulinda maslahi ya CCM; inasikitisha sana karibu kila wizara inaongozwa kiubabaishaji matokeo yake ni haya tunayaona, wapo watu wengi wenye uwezo hawakupewa nafasi za uongozi kwasababu wapo kwenye upinzani au wapo kwenye mtandao tofauti na mh. Raisi; tunaoumia ni wananchi wa kawaida kibaya zaidi, tumewachagua baada ya kupewa ahadi na matumaini yaliyojaa uwongo.

  Chama
  Gongo la Mboto DSM
   
 4. M

  MIGNON JF-Expert Member

  #4
  Feb 9, 2012
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 2,586
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  Mwanakijiji naamini kwa katiba ya Tanzania hakuna uwezekano wa PM kuwa mwenyekiti wa baraza la mawaziri.
  Naamini huki kilikuwa ni kikao tu cha mawaziri na kiranja wao.I stand to be corrected.
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Feb 9, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  thanks, add this one.... "collective responsibility"!!!:alien:
   
 6. M

  Mwanamutapa JF-Expert Member

  #6
  Feb 9, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 499
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Baraza la mawaziri linatoa tamko gani hilo wakati kuna mawaziri wabovu na wameangamiza taifa na kufanya madudu mengi kama William Ngereja, Ezekiel Maige na Dk Sgukuru Kawambwa lakini hawajachukuliwa hatua yeyote leo hii madaktari wagome Mponda awajibishwe kwa misingi ipi wapo niliowataja bado wapo madarakani pamoja na uozo wao mwingi?
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Feb 9, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Kweli waliourudisha CCM madarakani sijui hata kama wanajisikia vibaya huko waliko.
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Feb 9, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,449
  Likes Received: 81,494
  Trophy Points: 280
  Mkjj, huyu hata akivunja Baraza la Mawaziri hatakuja na jipya lolote la kuinusuru nchi isiangamie. Ameshakuwa madarakani miaka 7 sasa hakuna hata kimoja ambacho Watanzania tunaweza kusema hichi Kikwete anastahili pongezi. Katika miaka yote saba aliyokuwa madarakani ni madudu tu mwaka nenda mwaka rudi. Kwa maoni yangu huyu ashinikizwe ili ajiuzulu tu maana kuna ushahidi wa kutosha kabisa kwamba kazi ya kuongoza nchi imemshinda.
   
 9. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #9
  Feb 9, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Kamata hii:

  54.-(1) Kutakuwa na Baraza la Mawaziri ambalo wajumbe
  wake watakuwa ni Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais wa
  Zanzibar na Mawaziri wote.
  (2) Rais atahudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri na ndiye
  atakayeongoza mikutano hiyo. Na endapo Rais hayupo basi
  mikutano itaongozwa na Makamu wa Rais na kama wote wawili
  Rais na Makamu wa Rais hawapo
  Waziri Mkuu ndiye ataongoza
  Mikutano hiyo.
   
 10. m

  mwabaluhi JF-Expert Member

  #10
  Feb 9, 2012
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hivi unaowaongoza wakikukataa tena waziwazi kwa nini ung'ang'anie madaraka? Nyoni, Mponda, Nkya na Mtasiwa mnasubiri nini kuondoka?
   
 11. Bitabo

  Bitabo JF-Expert Member

  #11
  Feb 9, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Mkuu MM, nchi yetu tukufu haina baraza la mawaziri. Kuna genge la walafi tu kwa hiyo hawawezi kuwa na siri yoyote. La msingi ni kuvunja serikali nzima including Mkuu wa Kaya ili tuanze upya. Wanakera hawa jamaa
   
 12. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #12
  Feb 9, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hayo ni maelekezo ya Katiba. Ukweli unabaki pale pale kwamba alichoongoza Pinda hakikuwa kikao cha Baraza la Mawaziri.

  Walikuwa wanapiga porojo tu, katika mgogoro huu wa sasa pamoja na kujikosha kote Pinda ni mtuhumiwa wa uchochezi wa mgomo kutokana na vitisho alivyotoa kwa Madaktari.
   
 13. T

  Tata JF-Expert Member

  #13
  Feb 9, 2012
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,729
  Likes Received: 645
  Trophy Points: 280
  Unawaongelea Judge Lewis Makame na Rajabu Kiravu au?
   
 14. T

  Tata JF-Expert Member

  #14
  Feb 9, 2012
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,729
  Likes Received: 645
  Trophy Points: 280
  Mimi naona wakiwafukuza Dr. Mponda na Blandina Nyoni peke yao watakuwa wanawaonea tu. Inabidi na yule aliyetoa "ultimatum" Jumapili moja kuwa kufikia kesho yake madaktari warudi kazini na wasiporudi wamejifukuzisha kazi naye ajiuzulu. Kwa mtazamo wangu huyu jamaa hakutumia busara wala hakuonyesha uongozi katika suala zima la mgomo huu na zaidi kauli yake ya vitisho ya kuwataka madaktari warudi kazini bila kwanza kushughulikia madai yao ya msingi ilichochea badala ya kupunguza makali ya mgomo.
   
 15. T

  Tata JF-Expert Member

  #15
  Feb 9, 2012
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,729
  Likes Received: 645
  Trophy Points: 280

  Ndugu yangu mambo ya kujiuzulu ni mambo ya kikoloni mamboleo ya wazungu sisi hatuna huo utamaduni wa kujiuzulu.
   
 16. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #16
  Feb 9, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  na waziri wa elimu pia atimuliwe
   
 17. K

  Kuntakint JF-Expert Member

  #17
  Feb 9, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,110
  Likes Received: 468
  Trophy Points: 180
  Na bado wanavaa sare na kushangilia, kuimba chama chao cha mafisadi yajenga nchi.. chama chao cha mafisadi yajenga nchi.. mafisadi ooh..mafisadi yajenga nchi. na wengi wao wapo humu.
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Feb 9, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Makamo wa rais yupo wapi hata asiongoze kikao cha baraza la mawaziri?
   
 19. k

  kiche JF-Expert Member

  #19
  Feb 9, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Siri gani unayoongelea hapa mkuu!!kumbuka baraza la mawaziri limegawanyika sehemu tatu,sasa endapo upande ule unaonufaika na mgogoro huu unaonekana kushinda ni lazima watoe furaha yao hiyo kwa wapambe wao!!!si ajabu kuna siku tutasikia wametwangana mangumi kwenye hicho kikao chao!!
   
 20. GY

  GY JF-Expert Member

  #20
  Feb 9, 2012
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Kweli kufa kufaana, kama namuona Ngeleja vile jinsi anavyopona kung'oka sakata la Jairo kupitia mgongo wa mgomo!
   
Loading...